Ni wakati dhahiri wa kutafakari maendeleo ya sayansi na teknolojia katika nchi yetu

Ni wakati dhahiri wa kutafakari maendeleo ya sayansi na teknolojia katika nchi yetu

Hamza Nsiha

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2022
Posts
221
Reaction score
197
Ndugu wanaJamiiForums ni matumaini yangu mu bukheri wa afya. Siku chache tumepokea na kushuhudia ajali mbaya iliyotokea mjini Bukoba. Suala ni kuwa mpaka sasa tumekuwa katika harakati za kuijenga nchi yetu katika misingi bora ya sayansi na teknolojia ya hali ya juu kwa kuandaa miradi mbalimbali yenye tija kwa ajili ya kufanikisha zoezi hili.

Binafsi ninapenda sana na pia huwa ninafurahishwa pindi nionapo miradi mbalimbali ihusishayo ukuaji wa sayansi na teknolojia mfano mzuri ni kama vile miradi ya reli ya kisasa, mabwawa makubwa ya kuzalisha nishati ya umeme, maboresho ya vifaa vya kisasa katika huduma za afya.

La hasha, hususani na yote yafanyikayo nchini ili kutengeneza nchi bora yenye maendeleo makubwa ya sayansi na teknolojia hofu yangu kubwa imeibuka mara baada ya ajali ya ndege iliyotokea siku chache nyuma.

Ni ukweli usiopingika kuwa, mpaka sasa ni lazima tutafakari kwa kina juu ya maendeleo makubwa kwa kuzingatia upande wa pili wa sarafu, yaani (nini kifanyike kama kikitokea hiki......). Siku kadhaa hapo nyuma tumeshuhudia katika vyombo vya habari juu ya mafunzo yenye uhalisia juu ya uokoaji wa abiria katika ndege iliyopata ajali ambapo maonesho hayo yalifanyika huku ndege kubwa yenye abiria zaidi ya 300 wakihusishwa. Hakika walifanikiwa kuonesha ufanisi mkubwa katika uokoaji, zimamoto, vyombo vya ulinzi na hata huduma ya kwanza kwa majeruhi.

Hivyo basi, kama tulifanikiwa kuonesha ufanisi katika maonesho hayo ni wazi kuwa tunahitaji mafunzo zaidi ya (kama ikitokea katika maeneo mengine.......)

Ni wakati sasa wa kutathimini juu ya miundombinu mbalimbali inayoanzishwa pamoja na njia mbalimbali za utatuzi wa matatizo kama shida yoyote itajitokeza.

Mfano dhahiri, juu ya uanzishwaji wa reli ya kisasa ni lazima pia kuwepo na tahadhari endapo shida zingine zinapojitokeza kwani ni kweli kuwa Ajali haina kinga lakini tahadhari na njia bora za utatuzi wa matatizo zinaweza kuwa na msaada mkubwa.

Tuendelee kuiombea nchi yetu, lakini pia mamlaka husika katika sekta mbalimbali itazame mambo haya kama changamoto ambazo zinaweza kutathminiwa katika maendeleo ya sayansi na teknolojia kwani kwa ajali hii imeonesha dhahiri bado tupo katika zama za mwanzo za kale na si katika zama zile tunazosema kila siku kuwa hii ni Tanzania ya viwanda.​
 
Huduma ya upatikanaji wa maji (bila kujali ni safi au salama) imetushinda, teknolojia tutaiwezea wapi? Hapo bado huduma ya afya, chakula, elimu, umeme.

Au nchi yetu inapiga hatua kurudia nyuma, ila hatuambiwi?
 
Tanzania ni losers,vazi la taifa tu limetushinda sembuse hayo mengine.

Tatizo linalotusumbua ni umimi na kujifanya mtu mmoja anajua kila kitu, nchi haina dira ya taifa kila rahisi akija anakuja na mbwembwe zake ilikutafuta sifa zake tu (umimi huo)

#wearelosers
 
Huduma ya upatikanaji wa maji (bila kujali ni safi au salama) imetushinda, teknolojia tutaiwezea wapi? Hapo bado huduma ya afya, chakula, elimu, umeme.

Au nchi yetu inapiga hatua kurudia nyuma, ila hatuambiwi?
Taratibu tutafika mkuu, lakini inabidi nchi ituaminishe kwanza katika masuala kama haya ili kujenga imani juu ya masuala mengine ya baadae...
 
Tanzania ni losers,vazi la taifa tu limetushinda sembuse hayo mengine.

Tatizo linalotusumbua ni umimi na kujifanya mtu mmoja anajua kila kitu, nchi haina dira ya taifa kila rahisi akija anakuja na mbwembwe zake ilikutafuta sifa zake tu (umimi huo)

#wearelosers
[/QUOTE
Anyway, hii ndio nchi yetu hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania tuzidi kuiombea izidi kufanya yaliyobora zaidi....
 
Taratibu tutafika mkuu, lakini inabidi nchi ituaminishe kwanza katika masuala kama haya ili kujenga imani juu ya masuala mengine ya baadae...
Najua tutafika. Lakini siyo ndani ya miaka mingi ijayo. Hatua yetu ya maendeleo kama taifa inasikitisha na kutisha at the same time.

Nadhani hakuna nia na juhudi za dhati kuleta maendeleo kwenye nchi.
 
Nchi ishaombewa hii na manabii wakutosha ulimwenguni na misa na ibada za kila siku inaonbewa, lakini mabadiliko hakuna. Ina waganga kila kona hadi ikulu, masheikh, wachungaji, mapadri n.k.

#wearelosers wananchi hadi viongozi wa nchi hii. Tupo duniani bora liende tu.
 
Umeme na Maji bado vinatushinda,,Halafu unasema sayansi na teknolojia ipo hiyo?
Miaka 62 ya uhuru bado tu umeme na maji ni shida..hiyo sayansi na teknolojia labda vya mchongo.
 
Back
Top Bottom