Ni wakati gani Lissu alipoanza kuwa liability kwenye chama cha CHADEMA?

Ni wakati gani Lissu alipoanza kuwa liability kwenye chama cha CHADEMA?

cencer09

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2012
Posts
4,554
Reaction score
2,732
Kuna mijadala mingi imeshika kasi kuelekea uchaguzi wa CHADEMA hususan nafasi ya mwenyekiti na makamu mwenyekiti, kuna kambi kuu mbili ya mwenyekiti anayeenda kutetea uenyekiti wake mwamba Freeman Mbowe na ya makamu mwenyekiti Tundu Antipas Lissu anayegombea uenyekiti safari hii.

Kwanza nadhani kwa katiba ya CHADEMA wote hao wanaruhusiwa kugombea, na katika kugombea huko hawatokuwa wamevunja au kukiuka katiba yao. Ukakasi ninaouona ni pale wengi wa wakosoaji wanaopinga Lissu kugombea uenyekiti madai yao kwamba hafai. Na sababu zao ni hana humility, hana hekima ya uongozi, mropokaji, mtukanaji nk. Ingawa ushahidi wao hauna nguvu, mfano mmoja wao anasema kumwita kiongozi wako muongo hata kama muongo ni kosa.

Hoja yangu kubwa kuwa wakosoaji wa Lissu ndani ya CHADEMA na wengi CCM wanaotoa hoja hizi wanafikirisha mno.

Sababu:
Lissu hii si mara ya kwanza kuongoza, alikuwa chief whip bungeni, kumbuka hata mjadala wa Escrow enzi za spika Ana Makinda. Je wakati ule alikuwa hana uwezo wa kuongoza?

Aligombea na kushinda kwa kishindo uchaguzi wa chama cha wanasheria TLS mwaka 2016, note chama hiki ni cha wasomi siyo kama akina Paulo Ntobi na Yericho Nyerere. Hawa walikuwa ni vichaa au wakati ule Tundu Lissu alikuwa bado hajapata kichaa?

Mwaka 2020 CHADEMA walimteua kuwa mgombea urais, na wakazunguka nae nchi nzima kufanya nae kampeni, na ni hao waliotuaminisha kwamba alipata kura nyingi ila aliporwa. Tujiulize hawa akina Ntobi na Yericho Nyerere na akina Wenje walikuwepo mbona hatukusikia mgombea wao wa urais ni mropokaji na hafai?

Hizi kelele hata humu jukwaani jf tumeanza kuzisikia baada ya kutoka na kumkabili Mbowe kwenye uchaguzi wa uenyekiti wa CHADEMA. Je kugombea uenyekiti na Mbowe ni ukichaa na ndipo sifa za uropokaji zimeanza?

Naomba mtueleze lini sifa za uropokaji na kutokuwa leader material zilianza kabla hamjaendelea kuonyesha udhaifu wenu kichwani.
 
Back
Top Bottom