Ni Wakati Gani Mtu Anapaswa Kufa?

Ni Wakati Gani Mtu Anapaswa Kufa?

OnTheEarth

Member
Joined
Jan 1, 2023
Posts
75
Reaction score
67
Ni wazi kwamba kifo kipo na kitatokea kwa kila mtu. Kwa asili, kifo sio jambo baya; ila jambo baya ni, namna kifo kinavyotokea na pia kushindwa kujua kwa uwazi nini kinaendelea baada ya mtu kifo.

Tunapata uchungu na huzuni mkubwa ndugu zetu wanapokufa si kwa sababu ya kifo chenyewe isipokuwa kwa namna kifo hicho kilivyokea na pia hofu tuliyonayo kwa sababu ya kutokujua nini huja baada ya mtu Kufa.

Kuna jambo moja hapa nalo ni hili: wanaokufa siku zote ni watu tunaowategemea.

Hawa wanaofikwa na kifo tunawategemea kwa mambo makuu matatu. Jambo la kwanza tunawategemea kwa upendo; kwamba ni ndugu zetu, ni watu wa damu moja. Jambo la pili ni la kiakili; kwamba tunawategemea kwa mafundisho ya imani, malezi, elimu na Jambo la tatu ni la kimwili: ndio kusema tunawategemea kiuchumi, mamlaka au nguvu.

Kwa jinsi kifo kinavyotokea pamoja na hofu yetu ya kutokujua nini hufuata baada ya mtu kufa, mambo haya mawili kwa kweli huzidisha huzuni na uchungu kuliko kifo chenyewe.

Swali kwamba ni Wakati Gani Mtu Anapaswa Kufa haliwezi kuwa na maana kwa sababu ya mambo matatu haya yafuatayo: upendo, kutegemea kiakili na kutegemea kimwili. Baba au mama kwa mfano, wanategemewa kiakili, kimwili na kiupendo na watoto wao na kinyume chake ni sahihi.

Kusema wakati gani mtu anapaswa Kufa si tu jambo la umri au kwamba kila kitu kiko sawa kiuchumi: sasa ninaweza kuondoka! Kwa kweli hili sio suala tu la kuweka sawa kila kitu kihusuyo uchumi au kwamba ni afadhali mtu akifa akiwa tayari ana zaidi ya umri wa miaka 80; bali ni suala la mfumo unaotakiwa kiakili.

Hofu yetu juu ya nini hutokea baada ya kufa ni, ya bure kwa sababu ukweli wa hayo yote tunao ndani yetu. Aidha juu ya wakati gani mtu anapaswa kufa ni, wazi kwamba tunaweza kukabiliana na Jambo hili kwa kufuata utaratibu unaotakiwa.

Watu uhuzunika na kuwa na uchungu baada ndugu kufa kwa sababu wanahofia maisha yatakuwaje. Hii ni kwa sababu mfumo uliopo wa maisha unaofanya kazi hauko jinsi unavyotakiwa kuwa.

Pamoja na ukweli kwamba kuna huzuni ya upendo na uchungu wa upendo, ni hivyohivyo kwamba mambo hayo yote ni sabubu ya huzuni na uchungu.

Kifo ni jambo la huzuni kwa sababu ya upendo, na kwa kweli kwa sababu ya mifumo yetu mibaya ya maisha ni jambo la kutarajia wakati wowote kila mtu. Kwetu, kwa sababu ya mifumo ya maisha tunayoishi, kifo hakiwezi kuwa kitu cha gafula au kitu ambacho hakikutarajiwa: kwa hiyo ni kitu cha wakati wowote.

Tunaweza kushughulikia wakati gani mtu anapaswa kufa kwa kukarabati upya mfumo wetu wa maisha; ndio kusema Imani: tamaduni, elimu na mafundisho, uchumi na utawala.

Jambo moja na la muhimu zaidi kuliko mengine yote katika hili ni, "Imani". Imani kwa yenyewe ndio msingi wa mengine yote ya elimu, tamaduni, malezi, mafundisho, uchumi, maadili, uongozi na utawala pia ndio huonyesha hatima ya mtu baada ya kufa.

Mambo yote: mema au maovu, mazuri au mabaya, yanafafanulia kama Imani ya kweli au isio ya kweli.
 
Nikajua Ni swali unauliza?
Kumbe umeamua kutoa mahubiri[emoji848]
 
Akiwa tayari tu afe
 
Back
Top Bottom