1. Mimi Freeman Aikaeli Mbowe, ni miongoni mwa waasisi wa hiki chama, nimekitumikia kwa jasho, damu na kwa mali zangu binafsi,
Nimekamatwa na serikali na kushitakiwa mara nyingi, nawezaje kukisaliti chama chetu hiki ndugu wanahabari na wananchi?
2. Mimi nimezaliwa na kukulia kwenye familia ya wafanyabishara, na biashara hizo nimeziendeleza na familia yetu ktk matajiri Tanzania kwenye list ya 20 bora tumo, nawezaje kuwa dalali wa chama kwa ukwasi tulio nao binafsi?
3. Ndugu wanahabari na watanzania jaribu kuwaambia hao wanaosema kwamba mimi chama nilikingeuza na kuwa kama mali binafsi au kukidalalia, je wana udhibitisho gani wa kuweza kudhibitisha kwa umma?
4. Ndugu wanahabari Mimi nimekitumikia chama changu kwa moyo, akili na nguvu Zangu zote, mimi ni Mwana Chadema na nitaendelea kuwa mwanachadema,
Wakihitaji ushauri wangu juu ya chama mimi niko tayari kushauri wakati wowote ule.
5. Huko mitandaoni wanasema mimi ni mtu wa Tiss (System) je kuna mwanasiasa gani wa rank za juu wa vyama vya upinzani asiye mutu ya System hapa nchini?