#COVID19 Ni wakati kwa Marekani kuelekeza nguvu kupunguza pengo la chanjo

#COVID19 Ni wakati kwa Marekani kuelekeza nguvu kupunguza pengo la chanjo

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
VCG31N1231430235.jpg

Hivi karibuni, shirika la ujasusi la Marekani lilitoa ripoti kamili kuhusu chanzo cha virusi vya Corona, ambayo ilishindwa kujibu swali kuwa ni jinsi gani virusi hivyo vya ugonjwa wa COVID-19 vilimwambukiza mtu wa kwanza.

Baada ya kupoteza nusu mwaka ambao ni fursa muhimu kwa dunia nzima kupambana na ugonjwa huo, sasa ni wakati kwa Marekani na washirika wake kuelekeza nguvu zote katika ushirikiano wa kimataifa wa chanjo.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani WHO, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Septemba, zaidi ya asilimia 70 ya nchi tajiri zilikuwa zimetimiza lengo la kuchanja asilimia 40 ya wananchi wao. Lakini katika nchi 54 za Afrika, ni tano tu yaani chini ya asilimia 10 zimetimiza lengo hilo. Pengo kubwa la kiwango cha utoaji chanjo kati ya nchi tajiri na maskini halikubaliwi katika siku ya leo inayojenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

Kwenye mkutano wa 16 wa wakuu wa nchi za kundi la G20 uliomalizika hivi karibuni, rais Xi Jinping wa China aliahidi kuwa nchi yake itatoa chanjo zaidi kwa nchi zinazoendelea, na kuunga mkono kampuni kushirikiana na nchi zinazoendelea kutafiti na kuzalisha chanjo.

Katika mkoa wa Constantine, mashariki mwa Algeria, chanjo ya Sinovac ya China inazalishwa kwa ushirikiano na kampuni ya dawa ya Algeria Saidal, na uwezo wa uzalishaji unatarajiwa kufikia dozi milioni 5 ifikapo mwezi Januari mwakani.

Mwezi Aprili mwaka huu, kampuni ya Sinovac ilisaini makubaliano mengine na kampuni ya biolojia na chanjo ya Misri VACSERA kuhusu kuzalisha chanjo yake. Kwa mujibu wa mpango, kama dozi bilioni 1 zinaweza kuzalishwa kila mwaka, Misri itakuwa mzalishaji mkubwa zaidi wa chanjo barani Afrika. Vile vile, kampuni ya dawa ya Morocco Sothema ilitia saini makubaliano na kampuni ya Sinopharm ya China kuhusu kuzalisha dozi milioni 5 za chanjo hiyo kwa mwezi.

Kutoka kutoa dozi moja moja ya chanjo hadi kuzindua mlolongo wa uzalishaji, michango iliyotolewa na China kwa nchi za Afrika inaonekana wazi. Marekani ikiwa ni nchi yenye kampuni nyingi kubwa za chanjo inatakiwa kuongozana na nchi za Japan, Australia na India zilizounda mazungumzo ya kimkakati ya pande nne Quad na kutangaza kuzindua “uhusiano wa wenzi wa chanjo” kuruhusu chanjo zao kuzalishwa barani Afrika.

Kwanza, wakuu wa Quad kwenye taarifa yao waliyotoa mwezi Septemba walikiri kuwepo kwa usambazaji mbaya wa chanjo na kuahidi kutoa msaada wa dozi bilioni 1.2 za chanjo kwa dunia. Kama nchi za Afrika zitaweza kupata sehemu za dozi hizi, itakuwa ni mchango mkubwa kwa ushirikiano wa kimataifa wa kupambana na ugonjwa huo.

Pili, kwa mujibu wa mwenyekiti wa shirikisho la kuzalisha dawa la Afrika Emmanuel Mujuru, mbali na miundombinu, Afrika pia inahitaji fedha nyingi na za muda mrefu ili kuunga mkono uzalishaji na utafiti wa chanjo barani humo, na pia kuhakikisha wadau husika watanunua chanjo kwa kufuata ahadi zao.

Katika mambo hayo, nchi nne za Quad zina uwezo mkubwa wa kutoa misaada ya kifedha na kiteknolojia.

Tatu, eneo la biashara huria la Afrika AfCFTA lililozinduliwa mapema mwaka huu limeunganisha masoko ya watu bilioni 1. Kwa kampuni za dawa za nchi hizi nne, hapa kuna fursa muhimu za kibiashara.

Umoja wa Afrika na Kituo cha Kudhibiti na Kukinga Magonjwa cha Afrika CDC hivi karibuni kimezindua utaratibu wa wenzi wa uzalishaji chanjo wa Afrika PAVM, ukitoa wito kwa wenzi wa kimataifa kusaidia kufanya chanjo zinazozalishwa na Afrika duniani kufikia asilimia 60 ifikapo mwaka 2040 kutoka asilimia 1 ya sasa.

Kwa mujibu wa hali ya sasa, nchi hizi nne kwanza zinapaswa kuunga mkono uzalishaji wa chanjo hiyo barani Afrika, kwani hii sio tu inaweza kuongeza fursa ya watu wa Afrika kupata chanjo hiyo, pia kuithibitishia dunia nzima kuwa utaratibu huo sio wa kijeshi kama nchi hizo zilivyosisitiza na pia kuonesha sura yao kama ni wenzi wanaoaminika wa maendeleo
 
Mathanzua wa ma debunked consiparicies akiusoma uzi wako machozi yatamtoka kwa hasira
 
Mathanzua wa ma debunked consiparicies akiusoma uzi wako machozi yatamtoka kwa hasira
Ni mjinga tu anayeweza kuamini kwamba kuna Corona na kwamba chanjo ndio solution ya matatizo ya mfumo wa upumuaji.Solution
ya tatizo hilo sio chanjo ni Ivermectin,Hydroxychloroquin,Vitamin D,K na C.

Corona mnayo ninyi agents wa TPTB/CIA na Mainstream Media ikiwa supported na Mockingbird Media.

Hii iko wazi hata ukitembea mitaani Dar.,huoni Barakoa.Utaona mtu kavaa barakoa pale tú ambapo watu wanalazimishwa kuvaa.Watanzania wanajua it is all nonsense and con.
 
Back
Top Bottom