Ni wakati muafaka kwa Mhe. Ismail Aden Rage kuwaomba mashabiki wa Simba msamaha

Ni wakati muafaka kwa Mhe. Ismail Aden Rage kuwaomba mashabiki wa Simba msamaha

Ona sasa ndani ya miezi miwili tu, uongozi unamtimua kocha aliyeshinda mechi zote mbili za ligi!

Halafu mashabiki nao wanaridhika tu. Yaani hawana hata ujasiri wa kuwahoji viongozi wao. Wanapelekwa pelkwa tu.
Amepata timu mpya huko Misri, kaona bora akale mema huko kwa farao.
 
Mimi siafiki RAGE kutuomba msamaha!!!!! wakati utakuja lakini sio sasa....!
 
Kwa heshima na taadhima naomba huyu Mheshimiwa ajitokeze hadharani kuwaomba mashabiki msamaha kwa kuwaita mbumbumbu wakati alipokuwa kiongozi mkubwa tu wa Simba Sports Club.

Ni vizuri akalifanya jambo hili wakati bado akiwa hai. Hata kama alighadhabika kiasi gani, bado hakutakiwa kuwaita mashabiki wa timu mbumbumbu! Yaani hawana chochote wanacho kijua!

Binafsi nilikuwa najua hili jambo wanamsingizia tu! Ila siku nilipoona kipande cha gazeti humu jukwaani, ndipo nilipoamini kuanzia siku ile.

Kiukweli naomba mashabiki wote wa Simba mniunge mkono katika hili. Hii kauli siyo nzuri hata kidogo. Na kwa kweli wengi mnachukizwa na hili jina! Maana imesababisha mpaka Watani wenu Yanga wawaite MBUMBUMBU FC!!

Uungwana ni kitendo. Mheshimiwa Ismail Aden Rage, jitokeze kokote ulipo. Omba msamaha kwa kuwakosea mashabiki wenzako wa simba. Usisubiri mpaka siku uko hoi kitandani, ndipo uombe huo msamaha.

Naomba kuwasilisha.
Naunga mkono huu uzi kwa 100%
 
Back
Top Bottom