Ni wakati Mwafaka sasa wa kufanya amendment kwenye sifa ya elimu kwa mgombea ubunge, badala ya kujua kusoma na kuandika, twende mbali zaidi

Mtu kuwa Mbunge, unadhani awe na walau kiwango gani cha elimu?

  • Darasa la saba

    Votes: 0 0.0%
  • Kidato cha nne

    Votes: 0 0.0%
  • Kidato cha sita

    Votes: 1 12.5%
  • Diploma yoyote

    Votes: 0 0.0%
  • Shahada ya chuo kikuu

    Votes: 7 87.5%
  • Sijui

    Votes: 0 0.0%

  • Total voters
    8
  • Poll closed .
Hata wazee mbona ndo vinara wakusifu taifa lolote hujengwa na vijana wenye nguvu,na mawazo mapya na chanya
Hili mimi sikubaliani nalo na mifano ninayo mfano taifa la marekani je hilo Taifa wanao liendesha ni Vijana au wazee? Hatukatai uwepo wa vijana ila hizi top positions hata wazee ni muhimu sana vijana bado wako emotionally sana na pia Ujana ujana unaweza haribu mambo, Kuishi kwingi kuona mengi
 
Kwa vile elimu bure ni mpaka kidato cha nne, manadiliko haya yaanze uchaguzi wa 2030 wakati elimu bure wa Magufuli watapiga kura kwa mara ya kwanza.

Ukianza sasa huu utakuwa ni ubaguzi.
P
Mkuu ebu tupe maana ya Elimu bure..Aya maneno ya Kiasa sio mazuri ata siku mmoja..Elimu inagharamiwa na watanzania wote ata ambao awana watoto au ata kufikia umri wa kua na familia. Ingawa unaweza ukawa sahihi kwakua upo kisiasa laghai zaidi ila nisingependa uwe mtu wa hivyo.
 
Mbona kina Nyerere hawakuharibu pia usiseme Marekani wao kule taasisi Kama mahakama, bunge na Uraisi ziko strong haziingiliani na Wala haihusiani na ujana au Uzee, ni vijana gani walipewa Jambo wakaharibu, shida ni mifumo na siasa plus mtu akiwa kiongozi lazima awe fisadi
 
Kutokana na mjadala unaoendelea sasa, unadhani mtu anaetaka kugombea ubunge anapaswa awe na walau elimu ya kiwango gani?
 
Kipaji bila elimu efficiency ni 40%
Na pia, ili wabunge wafanye vizuri kazi yao ya ubunge bila kujipendekeza kwa watawala, nashauri mawaziri wasitokane na wabunge.

Wakianza kujipendekeza kutafuta uwaziri, elimu yao wanaiweka pembeni na inakuwa haina maana.
 
Habari za Muda huu Wana JF,

Nimekuja na Mawazo haya Baada ya kutafakari na kuona yanayoendelea bungeni,pamoja na Uhalisia wa Maisha tuliyonayo Watanzania KWA wakati huu Ambapo Taifa lina wasomi wengi lakini linaongozwa na Watu baadhi yao wenye uwezo mdogo wa kupambanua mambo,huku Wakiwa hawajali pia matatizo ya Watu.

Sasa KWA Msingi huo napendekeza Tume ya Taifa ya Uchaguzi pamoja na Vyama viwe na mwongozo huu kama Ifuatavyo angalau tuweze Kupata wawakilishi Bora..

1.Madiwani...Elimu iwe kuanzia ngazi ya Cheti na kuendelea.

2.Wabunge...Kigezo kiwe kuanzia Diploma na Kuendelea.


Ni mtazamo wangu...
Nawasilisha!!!!!
 
Mbunge walau awe na bachelor aise itamake sense na fujo walau zitapungua mule ndani na hoja zitaeleweka kwa muafaka mzuri siyo kina pigameza tu lolote kwao sawa.
 
Mbunge walau awe na bachelor aise itamake sense na fujo walau zitapungua mule ndani na hoja zitaeleweka kwa muafaka mzuri siyo kina pigameza tu lolote kwao sawa.
Hahahahaa eti piga mezaa....Ngoja tuone wenzetu Wana mtazamo gani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…