Siyo uoga! Kuna vitu unapaswa kutenga uhalisia na ndoto.
JamiiForums, ndiyo wanaweza kupata pesa ya kutengeneza AI kupitia uwekezaji (fund raising) lakini swali la kujiuliza hiyo product watakayokuja nayo itakuja kutatua tatizo gani kwa Watanzania?
ChatGPT (OpenAI) na AI nyingine tayari zinafanya vizuri kwenye soko la chatbot. JF wakitengeneza ya kwao kwaajili ya Watanzania tu huoni kama ni matumizi mabaya ya rasilimali? Je, wakiweka paid version/services kwenye product yao ni Watanzania wangapi wapo tayari kulipia?
ChatGPT kwenye development tu imetumia $100m, kwenye infrastructure: 30,000 Nvidia GPUs kila moja imegharimu kati ya $10k - $15k. Monthly operational expenses: inakadiriwa kati ya $3m - $21m, kwa siku $100k - $700k.
Microsoft kupitia Copilot wanatumia OpenAI models, wamewekeza $10b.
Mpaka hapo unaiona wapi nafasi ya JamiiForums kwenye uwanja wa AI?
Tatizo kubwa lililopo Africa na linalozikuta kampuni za Teknolojia ni kupata watumiaji watakaoweza kulipia huduma/bidhaa zao.
AI ina wigo mpana na JF wanaweza kuunda products hata kwa uwekezaji mdogo tu ila sioni haja ya wao kuwekeza pesa nyingi kwenye kitu ambacho tayari kinafanywa kwa ukubwa na kampuni kubwa za Tech, na ukizingatia kupata wateja wanaolipia huduma/bidhaa kwa soko la Tanzania ni ngumu sana.