Ni wakati sasa kutengeneza maeneo mapya ya kibiashara ili kuiondolea nguvu Kariakoo. Kariakoo ibaki kama mji wa kale

Ni wakati sasa kutengeneza maeneo mapya ya kibiashara ili kuiondolea nguvu Kariakoo. Kariakoo ibaki kama mji wa kale

chiembe

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2015
Posts
16,859
Reaction score
28,112
Serikali inabidi Sasa ifikirie kuunda maeneo mapya ya kibiashara, nje ya kariakoo.

Ni ajabu mpaka leo, kariakoo ndio eneo pekee la kibiashara Dar es Salaam, na hicho ndio chanzo cha msongamano mjini.

Uwepo mkakati wa makusudi kuwekeza maeneo kama ubungo, kimara, bunju, tegeta kwa kujenga satellite towns huko, ikiwa na miundombinu yote ya kisasa. Ni wakati Sasa kuifinya kariakoo kwa kutengeneza kariakoo nyingine pembezoni, hivyo kuwaondoa watu mjini kati.

Hata hao wakwepa Kodi wanaogoma, wanatumia advantage hivyo kwamba mbadala wa uhakika hakuna.
 
Inawezekana! Maofisi mengi na wizara nyingi zipo mjini!,asubuhi kunakuwa na foleni kubwa kwenda mjini, tungetanua mji,masoko makubwa,baadhi ya wizara,Hospital,Airports zote zingekuwa nje ya mji ili kupunguza msongamano town.
 
Ili kuwafikia wananchi kuna haja ya kuongeza sehemu za kibiashara, ila siyo rahisi kuiua Kariakoo
 
Miaka 5 ijayo kariakoo itabaki na appartments za wanaofanya kazi posta kwa kile kinachofanyika sasa ubungo terminal.

Ubungo terminal inajengwa shopping city kubwa sana, bidhaa nyingi zinazotoka nje ya nchi chimbo litaamia hapo. Wanajenga hadi hotels hapo hapo. Storage facilities hapo hapo or nearby places zipo nyingi hazitumiki.

Washaanza uza flames, wakimaliza ujenzi fujo zote za kariakoo zitaamia Ubungo Terminal.
 
Kariakoo ilijijenga yenyewe
Wacha hayo maeneo tajwa yajijenge yenyewe muhimu miundombinu iboreshwe.

Leo hii ukipeleka hiyo miundombinu Mbagala na kupunguza viwanda pale nyuma niamini mimi Ile sehemu Ina potential kubwa ya biashara.

Ubungo well sio kubaya ila tayari wachina si wanapaendeleza pale na hakuwezi kuwa na potential kubwa kupita maelezo.

Mwenge sawa ila pia tuangalie tunataka soko la aina gani.
 
Na huko utitiri wa kodi ukibaki matokeo yatakuwa ni yale yale
 
Inajengwa hapo ubungo stand ya zamani,kila kitu kitapatikana hapo,complex ya wachina..... Kkoo inaweza kufa natural death kama Mpango utaenda sawa kama ilivyo
 
Ndio maana kama nchi tulipinda uelekeo sio,hizi suburbs zote za Dar zilitakiwa ziwe na shopping malls zao,na ofisi zote za kijamii, mkazi wa Tegeta haina haja ya kwenda kariakoo au ilala, hawa walitakiwa wajengewe mall na ofisi za serikali kule kule,jiji la Dar ni uchafu, linabidi tulijenge upya..tembelea pale kariakoo kuna flats zimekaribiana mno hata mnaweza to exchange coffee mugs!hii ni craze, jiji halina drainage systems, njia zote za uokoaji zimezibwa!angalia yule crocodile aliyejenga mitaa ya kinondoni A,magomeni yaani akifufuka leo ataamua kujirudia tena kaburini, hii nchi mbona stories zipo nyingi kuliko utendaji?
 
Hapa ishu sio KARIAKOO ishu ni KODI na HUDUMA za KIONEVU zinazo tolewa na TRA kwa WAFANYABIASHARA ( kimsingi ndio mabosi wao ila hawawajali kabisa )
 
Back
Top Bottom