Ni wakati wa Ali Kiba

Ni wakati wa Ali Kiba

Hata mimi siku hizi hata nikisikia katoa wimbo sihangaiki kuutafta mpaka niusikie bahati mbaya yani ni tofauti ni kipindi cha nyuma.
Uwa nazisikia kwa mabodaboda mfano kuna wimbo unaitwa baira ndiyo nausikia mabodaboda hapa wanaupiga sana ila bado hata sijatatfuta hiyo album.
Zamani yani nilipokuwa nasikia anatoa nyimbo nahesabu masaa lazima nkausake.
Ila kuna radha naimiss ile ya ukimuona, lala salama, mawazo, nalia, my number 1 sijui ni kuzoea uimbaji wake au vipi lakini ndiyo hivyo.
Ila jamaa namkubari maana ni hustler wa ukweli
Huu ndio ukweli ambao mashabiki zake uchwara hawapendi kuusikia!
Ile radha ya zamani nakosa kiukweli
 
Kuna mahali nimesema hivyo?
Kwahiyo kwa diamond hiki ndio kinaweza kuwa TAMATI ya kilele chake cha mafanikio...
Huenda sijakuelewa vizuri ila katika kutanguliza matatizo yanayomkumba Diamond kwenye thread ya mafanikio ya Kiba kumetoa taswira kana kwamba Diamond anampisha Kiba, na ndo nikasema mafanikio yao sio 'mutually exclusive'.
 
Mzeee mi naona ungeeendeleaaa tu kutuaaandikaaa makala za kiroho na kichawi hizi habari za kidaku zinashushaaaa hadhiiii yako[emoji2]
 
Huenda sijakuelewa vizuri ila katika kutanguliza matatizo yanayomkumba Diamond kwenye thread ya mafanikio ya Kiba kumetoa taswira kana kwamba Diamond anampisha Kiba, na ndo nikasema mafanikio yao sio 'mutually exclusive'.
Ok labda ni aina ya uandishi niliotumia lakini tamati ya kilele cha mafanikio haimaanishi ndio anguko la hasha ni kwamba unabaki palepale.... Ni kama gari yenye mwendokasi wa 180 ukifika hapo huendelei
 
Ali Kiba amewahi kuwa juu lini? Acheni kumpa sifa za kijinga huyo jamaa. Alikuwa kawaida kama wasanii wengine na wala hakuwahi utawala muziki wa Bongo fleva.
Kuna kipindi alikuwa na ushindani na Marlaw sema naona Marlaw nyota ilikuwa inawaka zaidi, hata tuzo za Kili alikuwa anachuka Marlaw wakiwekwa kwenye category 1, peak ya Kiba ilikuwa pale alipoenda kuimba na R.Kelly then alipotoka huko akamkuta Diamond anakimbiza mtaani ikambidi ajifanye ka-quit muziki, baadaye akarejea tena kwa mtindo wa bifu na Diamond, hiyo ndo imemboost kupiga hatua aliyonayo hivi sasa
 
Huenda sijakuelewa vizuri ila katika kutanguliza matatizo yanayomkumba Diamond kwenye thread ya mafanikio ya Kiba kumetoa taswira kana kwamba Diamond anampisha Kiba, na ndo nikasema mafanikio yao sio 'mutually exclusive'.
Hapana mkuu hakua na maana hiyo ispokuwa Diamond anahitaji kupata mshauri mzuri kwa sasa ili aendelee kufanya vema.
 
Mkuu umesahau kuwa wasanii wengi wakubwa duniani wanafeli katika maisha ya mahusiano,na wengi walishafika mahakamani kwa usuluhishi wa malezi ya watoto,macelebrity wana ndoa na mafans,ndio maana maisha ya ndoa yanawashinda sababu siku zote wanataka kuwafurahisha mafans wao kwanza na kuwasahau wenza wao!..so kwa bwana kiba huu ni mtihani mkubwa kwake,achague kulala studio ili kuwafurahisha mafans au kulala nyumbani na mama!
 
Ni mtu wa pili unanisoma vema... Wengine wote ni watu waliochangia bila kuelewa muktadha wa mada
 
Marlaw mkewe mwenyewe ni besta ambaye alikuwa msanii maarufu, kwa marlaw nadhani alikuwa na plani tofauti za kimaisha mbali na mziki ila kupotea ktk gemu msiseme kisa ni ndoa yake
Halafu kiba alipotea kwenye gemu kipindi mama wa mtoto wake walipoacha ilibidi aache mziki alee mwanae

Mkuu Ali alifungiwa ndani na madam Rita
 
Back
Top Bottom