Ni wakati wa Bodi ya Mkopo Elimu ya Juu (HESLB) kubadilika

Ni wakati wa Bodi ya Mkopo Elimu ya Juu (HESLB) kubadilika

Big Eagle

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2020
Posts
592
Reaction score
625
Nafahamu mpaka sasa upangaji wa mkopo kwa wanafunzi unasuasua japo mnaeleza pesa mnayo bil 570 wanafunzi nusu ya zaidi ya waliomba hawajui hatma yao (mnachelewa).

Kupanda na kushuka katika maisha ni jambo la kawaida kwa mfano familia ya mzee kiyoyozi miaka 20 nyuma ilikua nakipato kizuri na watoto wao walisoma shule nzuri za gharama lakini leo hii haiwezi kulipia hela ya mlizi shule za serikali ni ugomvi, (watakosa mkopo).

Familia ya mzee kupauka miaka 20 nyuma watoto wao walisoma shule za kata leo hii wao ndo neema imemiminika wakati watoto wao wanaenda chuo kikuu, (watapata mkopo).

Maisha yanaweza kubadilika wakati wowote yakawa mazuri au mabaya.

Ushauri wangu toeni mkopo kwa usawa kwa kila anae omba kila muomba mkopo anamahitaji maalum.
 
Hill ni tatizo kubwa haswa kama sekondari umesoma private kutoboa wakupe mkopo ni ngumu mno
 
Anayetakiwa kubadilika ni muombaji, waombaji wa bodi ya mikopo hawana tofauti na Mzee Matonya. Tafuteni hela, tafuteni hela muachane na HESLB. Ni bora usome kwa shida lakini kwa hela yako.
 
Anayetakiwa kubadilika ni muombaji, waombaji wa bodi ya mikopo hawana tofauti na Mzee Matonya.Tafuteni hela, tafuteni hela muachane na HESLB.Ni bora usome kwa shida lakini kwa hela yako.
Kwakuwa ni mnufaika was keki ya taifa sio
 
Anayetakiwa kubadilika ni muombaji, waombaji wa bodi ya mikopo hawana tofauti na Mzee Matonya. Tafuteni hela, tafuteni hela muachane na HESLB. Ni bora usome kwa shida lakini kwa hela yako.
Tajiri anaacha hela ndani anaenda kukopa bank ulishajiuliza kwanini achukui za ndani
 
Nina mdogo wangu kapata 1.7 o level na 1.5 A level masomo sayansi, na alipata udhamini feza boys, na barua ya udhibitisho walimpa kuwa alisoma bure, aliupload iyo barua, sasa mpaka batch ya 4 hakupata mkopo, hivi hii imekaaje au kwasababu alisoma feza licha ya udhamini astitaili kupata mkopo? Chuo amechaguliwa udsm
 
Kwa inavyoonekana hali ni mbaya sanaa,hizo pesa walizoongeza zipo kweli au ni porojo tu Kama ilivyo kawaida ya Tanzania...
 
Back
Top Bottom