Ni wakati wa kuipongeza CHADEMA ni wakati wa kuuonya Upinzani

Ni wakati wa kuipongeza CHADEMA ni wakati wa kuuonya Upinzani

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Nichukuwe nafasi hii kuipongeza Chadema kwa mambo kadhaa .

Kwanza kwa kujuwa nafasi yake ya kuwa chama kikuu cha upinzani na kuwa chama kiongozi miongoni mwa vyama vya upinzani Tanzania. Nawapongeza kwa kuonesha siasa mbadala.

Nawapongeza kwa kuanza kukomaa na kutoendeshwa kwa matakwa ya watawala. Chadema mmeprove kukomaa hasa baada ya hii miaka minne ya dhoruba na kuzishinda hila za Mtawala. Tunajuwa mlitegwa sana ili chama kipate hatia ya vurugu, fujo na kutotii sheria. Pongezi ziende kwa jopo la wanasheria, wazee wa chama na viongozi wote kwa kuruka viunzi vyote. wabaya wenu wanatahayari mpaka muda huu.

Niwapongeze kwa niaba ya vyama vya upinzani kuuwakilisha upinzani kwa kutoa mwelekeo wa siasa za nchi. Dunia nzima inafuatilia mwelekeo wenu na mmetuonesha njia.

ONYO KWA VYAMA VYA UPINZANI.
Umoja ni muhimu kuliko wakati wowote ule wa historia za vyama vingi. Kamwe msitoe mwanya wa kuvurugana upinzani wenyewe.

Chadema na vyama vyengine vikubwa viwe walezi wa umoja wa vyama na muungano mpya kuelekea uchaguzi wa 2020 na kamwe viongozi wasitumie mianya kubomoana wenyewe.

Vyama viache kutumiwa na CCM kwa maslahi yake. Upinzani uwe na mwelekeo mmoja hata kama kuna mambo wanatofautiana.

Vyama vijuitathmnini na kuweka msingi wa maridhiano kwanza kabisa kuelekea umoja wao ili kupambana na CCM ambayo imejipambanuwa haina rafiki wa kweli kwenye maslahi yake. Hilo walione CUF ya sasa, TLP na vyama vyengine ambavyo vimetuhumiwa kutumika kuuvuruga upinzani.

Nawaaasa CHADEMA specific baadhi ya wakati kujishusha na kuwa mlezi mkuu ili mambo yaende na hii haina maana wazembee wakiona mambo yanaharibika ilimradi tu iwe kwa nia njema.

Ni hayo kwa sasa.


Kishada.
 
Ushindi wa viongozi wa chadema una walakini sana

Kura zimechezewa

Kuna mwingine kapewa cheo wakati yupo nje ya Nchi
 
Ushindi wa viongozi wa chadema una walakini sana

Kura zimechezewa

Kuna mwingine kapewa cheo wakati yupo nje ya Nchi
Tunajuwa kwamba kuna watu wanakesha kutafuta hitilafu kwenye mchakato wa uchaguzi wa Chadema ili kuendeleza hujuma.

Tunajuwa kuna watu hawakufurihishwa na coverage ya CHADEMA kwa wiki mbili sasa.

Jaribio la Polisi kushusha bendera za Chadema ilikuwa lengo ni kuvuruga uchaguzi na mood ya viongozi.

Endeleeni kuipa umaarufu chadema kwa mikono yenu.
 
Kuelekea 2020 CDM imaarishe jopo lake la Sheria na kuwe na mfuko wa kufungua na kuendesha kesi mahakamani. Kuna washenzi dawa yao ni kuwasimamisha mahakamani kwa vitendo vya kuhujumu michakato halali. Pia kuna haja ya kutoa elimu ya kisheria kwa wagombea na walinda kura wao hasa kuhusu ushahidi unaoweza saidia chama pindi wakifanyiwa figisu.
 
Tunajuwa kwamba kuna watu wanakesha kutafuta hitilafu kwenye mchakato wa uchaguzi wa Chadema ili kuendeleza hujuma.

Tunajuwa kuna watu hawakufurihishwa na coverage ya CHADEMA kwa wiki mbili sasa.

Jaribio la Polisi kushusha bendera za Chadema ilikuwa lengo ni kuvuruga uchaguzi na mood ya viongozi.

Endeleeni kuipa umaarufu chadema kwa mikono yenu.

Nami nimeliona hilo. Sio kila matendo ya polisi ni uharibifu jumla LA hadha, mengine yana maumivu lakini ni kama uenezi. Yaani Jeshi LA polisi linakuwa idara ya Uenezi ya Chadema in a hardway.
Na hakika kama Magufuli angejua ni kwa kiasi gani katika miaka hii minne Polisi wamesaidia kuitangaza na kuiinua Chadema hakika angewaagiza waachane nao kabisa kwani hakuna mahali wanavunja sheria.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati ule umoja wa vyama ukiongozwa na Chadema kusitisha Maandamano ya Ukuta, kuna watu waliwapima Chadema kuwa wamekuwa waoga. Walisikiliza ushauri wa taasisi za Dini na wataalamu. Chadema imekuwa sasa kwa kujuwa kufanya siasa mbadala.
Chadema waliyasoma mazingira ya sasa na kujuwa njia za kupita. Hio mikesi iliyoko mahakamani ilikusudiwa kuwatoa nje ya ulingo. Jipangeni na mazuiyo na maamuzi msiyoyatarajia na hapo muwee tayari kutumia njia inayofaa kwa wakati sahihi.
 
Wakati ule iliyokuwa CUF Zanzibar ilikuwa ikilaumiwa eti wamesusia uchaguzi, watu walisahau kuwa walishatumia mbinu zote ikiwemo kupambana na CCM kwa njia ya makabiliano na kunyanganyana masanduku ya kura na Polisi. Ilisaidia kwa wakati fulani na haikusaidia kwa baadhi ya wakati. La msingi ni kusoma wakati.

Wakati mwengine kususia ni bora kuliko kushiriki. Angalia hio Globe attention iliytengenezwa na CUF wakati huo kuelekea chaguzi zilizofuata za 2000, 2005 na 2010? walitumia " Multiple Approach kufikia hapo walipofika hadi kukawa na miafaka ya kitaifa Zanzibar.

Naiona Chadema ikijifunza kitu kuhusu Upinzani wa Zanzibar ulioongozwa na Maalim Seif gwiji wa siasa kule.

Kuna approach za maandamano, kususia, kushiriki, kupinga na kutoa matamko, kupambana n.k.

Ishu ni wakati gani ? itumike njia ipi. Ona sasa Mfalme alivyo uchi.

Chadema imeimarika. Hongereni.
 
Sasa chadema imeacha siasa za uharakati. inahitajika utaalamu kutengeneza taswira ya taasisi isionekane ya ubabe na fujo ndani na nje ya nchi.
Wakati fulani iliyokuwa CUF ilipotumia njia za mapambano kudai haki, CCM ilitumia mwanya huo kuitangaza CUF kuwa chama cha Kigaidi. CUF ilikuja na mikakati ya kuimarisha siasa za kimataifa na kujijenga, ikatumia ustaarabu wa kususia na kugoma na kufanikiwa kuishawishi Dunia. Hilo ni somo.
 
Back
Top Bottom