kulyunga
JF-Expert Member
- Oct 19, 2011
- 230
- 423
Waalimu wote wa nchi hii ya tanganyika hii inawahusu. CWT au chama cha waalimu Tanzania kwa muda sasa kimekuwa chama cha kinyonyaji kwa kisingizio cha kutetea haki za waalimu kitu ambacho sio sahihi. Unyonyaji na ubadhilifu wa chama hiki ulitokana na ukweli kwamba hakukuwa na chama mbadala cha waalimu kwa muda mrefu sana na hivyo wao wakaendeleza ukiritimba huu kwa muda mrefu.
Mwalimu unapoanza kazi kabla ya kusign makubaliano ya uamuzi wako wa kuingia kwenye chama unaanza kukatwa michango ya chama ambayo ni asilimia 2 ya mshahara kama vile kujiunga na chama hiki ni lazima. Hapa CWT imekuwa ikifanya mchezo na baadhi ya waajiri kwa kushitikiana na maafisa utumishi na kuingiza makato haya kwenye mishahara ya waalimu kwa mtindo wa "check off" bila mwalimu kuwa mwanachama kwa kusign au kujaza form za uanachama.
2. Makato haya ya asilimia 2 ni makubwa sana na mzigo kwa waalimu kwa sababu ni makato ambayo unakatwa kwa maisha yako yote kama mtumishi na unapostaafu chama hakikupi hata mkono wa kwaheri au bonasi yoyote ile. Kwa taarifa ambazo sijathibisha makato haya kwa tanzania nzima ni takribani billion 3 pesa ya kitanzania kwa uendeshaji wa chama tu hii ni pesa nyingi sana.
Yawezekana kiwango hiki cha makato kilikuwa ni halali mwaka 1994 wakati chama kinaanzishwa lakini leo miaka 21 baada ya kuanzishwa chama tayari kina miradi ya majengo makubwa ya kupangisha katika mikoa kadhaa hapa nchini nadhani pesa ya kodi ingetosha kabisa kwa shughuli za kawaida za kuendesha chama.
3. Ufisadi mwingine ni kutafuna asilimia 15 ya michango ya mwanachama inayotakiwa kurudi kwa mwanachama kupitia tawi lake au taasisi anayofundisha mwanachama mchangiaji. Hii ni haki ya kikatiba ya kila mwanachama lakini utoaji wa pesa hii umekuwa ni tatizo na baadhi ya sehemu hii haitolewi kabisa na viongozi wa wilaya wanakula pesa hizi kinyume na sheria na taratibu za chama.
Hakuna asiyejua umuhimu wa chama cha watumishi katika kuunganisha unoja wa watumishi husika katika kudai na kutetea haki na maslahi ya watumishi husika ila vyama hivi vinapotumika kama vitega uchumi vya watu binafsi hili linakuwa tatizo kubwa na sasa kuna vyama mbadala wa CWT vimeanza kuzaliwa ambavyo vimeangalia mapungufu haya ya cwt na kuyatekebisha. Mwisho nasema waalimu kwa pamoja tuungane kuupinga unyonyaji huu wa CWT.