Ni wakati wa kusema "no" kwa CWT na unyonyaji wao

kulyunga

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2011
Posts
230
Reaction score
423
Waalimu wote wa nchi hii ya tanganyika hii inawahusu. CWT au chama cha waalimu Tanzania kwa muda sasa kimekuwa chama cha kinyonyaji kwa kisingizio cha kutetea haki za waalimu kitu ambacho sio sahihi. Unyonyaji na ubadhilifu wa chama hiki ulitokana na ukweli kwamba hakukuwa na chama mbadala cha waalimu kwa muda mrefu sana na hivyo wao wakaendeleza ukiritimba huu kwa muda mrefu.

Mwalimu unapoanza kazi kabla ya kusign makubaliano ya uamuzi wako wa kuingia kwenye chama unaanza kukatwa michango ya chama ambayo ni asilimia 2 ya mshahara kama vile kujiunga na chama hiki ni lazima. Hapa CWT imekuwa ikifanya mchezo na baadhi ya waajiri kwa kushitikiana na maafisa utumishi na kuingiza makato haya kwenye mishahara ya waalimu kwa mtindo wa "check off" bila mwalimu kuwa mwanachama kwa kusign au kujaza form za uanachama.

2. Makato haya ya asilimia 2 ni makubwa sana na mzigo kwa waalimu kwa sababu ni makato ambayo unakatwa kwa maisha yako yote kama mtumishi na unapostaafu chama hakikupi hata mkono wa kwaheri au bonasi yoyote ile. Kwa taarifa ambazo sijathibisha makato haya kwa tanzania nzima ni takribani billion 3 pesa ya kitanzania kwa uendeshaji wa chama tu hii ni pesa nyingi sana.

Yawezekana kiwango hiki cha makato kilikuwa ni halali mwaka 1994 wakati chama kinaanzishwa lakini leo miaka 21 baada ya kuanzishwa chama tayari kina miradi ya majengo makubwa ya kupangisha katika mikoa kadhaa hapa nchini nadhani pesa ya kodi ingetosha kabisa kwa shughuli za kawaida za kuendesha chama.

3. Ufisadi mwingine ni kutafuna asilimia 15 ya michango ya mwanachama inayotakiwa kurudi kwa mwanachama kupitia tawi lake au taasisi anayofundisha mwanachama mchangiaji. Hii ni haki ya kikatiba ya kila mwanachama lakini utoaji wa pesa hii umekuwa ni tatizo na baadhi ya sehemu hii haitolewi kabisa na viongozi wa wilaya wanakula pesa hizi kinyume na sheria na taratibu za chama.

Hakuna asiyejua umuhimu wa chama cha watumishi katika kuunganisha unoja wa watumishi husika katika kudai na kutetea haki na maslahi ya watumishi husika ila vyama hivi vinapotumika kama vitega uchumi vya watu binafsi hili linakuwa tatizo kubwa na sasa kuna vyama mbadala wa CWT vimeanza kuzaliwa ambavyo vimeangalia mapungufu haya ya cwt na kuyatekebisha. Mwisho nasema waalimu kwa pamoja tuungane kuupinga unyonyaji huu wa CWT.
 
HII HOJA NIMEIPENDA SANA .MIMI NPO HALMASHAUR FLANI NIMEANDIKA BARUA YA KUOMBA NISITISHIWE MAKATO YA CWT KWA SABABU SIKUWA NA MKATABA NAO NILIIANDIKA BARUA KWA KUREJELEA SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO YA KAZI YA 2007, ibara ya 61:1MKURUGENZI NA OFISA ELIMU WALIKOMENT NITOLEWE ILA OFISA UTUMISHI NAONA ANAMASLAH NA KUKATWA KWANGU.SIKATI TAMAA NITAENDA TENA
 
Ila kwel,makato wanayochukua kwenye mishahara yetu hailingani na huduma yao,nonsense!..
 
HII HOJA NIMEIPENDA SANA .MIMI NPO HALMASHAUR FLANI NIMEANDIKA BARUA YA KUOMBA NISITISHIWE MAKATO YA CWT KWA SABABU SIKUWA NA MKATABA NAO NILIIANDIKA BARUA KWA KUREJELEA SHERIA YA AJIRA NA MAHUSIANO YA KAZI YA 2007, ibara ya 61:1MKURUGENZI NA OFISA ELIMU WALIKOMENT NITOLEWE ILA OFISA UTUMISHI NAONA ANAMASLAH NA KUKATWA KWANGU.SIKATI TAMAA NITAENDA TENA

Hii ndo elimu tunayotakiwa kutoa mkuu manake wengi tumeingizwa humo bila mikataba wala makubaliano..
 
naomba tusaidiane kwa mwenye ufahamu khs CWT kushughulikia suala la walmu kutorekebshiwa mshahara baada ya kpanda daraja
 
pia CWT hiyo kushughulkia walmu wanaodai klipwa mshahara ambayo hawaklpwa.mwenye lakhsiana na hayo atoe mwanga kwa walm
 
mimi ni mdau wa cwt na declare interest,cwt sasa inaelekea kubadilika kwa katiba mpya ya cwt wastaafu wote watapewa mkono wa kwaheli,pia katika kila ngaz ya uongoz wameweka nafasi ya vijana ili kuleta mabadiliko katika utendaji lakini pia kuna kitengo cha dharura wewe mwl kama umefiwa na mtu wa karibu unauguliwa nenda kwenye tawi la cwt ukiwa na kitambulisho utasaidiwa.kama kuna swali niulizeni ila ctokuwa hewani muda wote
 
cwt mwalimu akifariki wanatoa rambirambi elfu 50 hata km alikatwa miaka 30 au 2 daaaaah na huo uwizi wa kunzisha bank ya walimu eti kuwasaidia walimu wakati hisa za hiyo bank zishanunuliwa na wafanyabiashara huku nyuma mwalimu mdau wa bank share holder hajui chochote kuhusu share ila wanaambiwa wakanunue hisa za bank eti kila mwalimu ana ofa ya hisa 100 loooo
 
hadi na wafanyakazi wa BOT? ha!ha!

kumbe mnajua kuwa kila aina ya wafanyakazi ni lazima wawe na chama cha kuwasemea,sasa wewe mwl unataka tuongozane wote kwa waziri kudai stahiki zetu?cwt inamapungufu ila kinasaidia sana,hapa nilipo mimi kuna walimu 7 walitakiwa kufukuzwa kazi ila cwt ikasimama imara kuwatetea wote wamerudushwa kazin,sasa wewe unaoshawishi wenzako kusema no kwa cwt bado halijakukuta
 
Binafsi naona serikali inatafuta namna ya kuwagawa waalimu. Ningekuwa mwalimu nisingekubaliana na mbinu hii chafu. Kuweni makini sana nyie Walimu. Mkifikiri mmepata mkombozi mtakuwa mmepotoka. Serikali inawagawa ili iweze kuwatawala vzr. Tumieni akili na tafakarini kwa kina kabla ya kufanya maamuzi. Ingekuwa vyema kama mgejikita kutengeneza cwt iimarike zaidi. Kuanzisha chama kipya naweza kusema ni kupotoka na ipo siku mtajutia huo uamuzi.
 
kumbe mnajua kuwa kila aina ya wafanyakazi ni lazima wawe na chama cha kuwasemea,sasa wewe mwl unataka tuongozane wote kwa waziri kudai stahiki zetu?cwt inamapungufu ila kinasaidia sana,hapa nilipo mimi kuna walimu 7 walitakiwa kufukuzwa kazi ila cwt ikasimama imara kuwatetea wote wamerudushwa kazin,sasa wewe unaoshawishi wenzako kusema no kwa cwt bado halijakukuta
Mnufaika wa chama cha matapeli utamjua tu kwa utetezi wake. Hao walio fukuzwa kazi hata usinge kuwa wewe kama wanajitambua wangerudi tu kazin maana sheria za utumishiwa uma zipo wazi kabisa wala hazipo CWT pekee. Nakama makosa yao yalikuwa lazima wafukuzwe kazi kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umaa CWT hamna uwezo wa kulizuia hilo, acha kurubuni watu ukidhani hawajui haki zao. CWT ni wezi sana mama watoto wangu akiwa mwalimu kabla hajahama kada ya elimu tuliandika barua ya kusitisha makato hayo na nakala ikaenda hadi kwa mwenye kiti mkoa na akasitishiwa makato baada ya kutaka kupeleka shauri mahakamani. Soma sheria za utumish wa umaa utaelewa ninacho sema acha kurubuni watu , chama gani kinakata makato kila mara lakini anaye katwa hanufaiki na makato hayo? Zaid ya viongozi kibadili magari kila siku??
 
Na wewe utakuwa mnufaika wa chama kipya au unatafuta kupewa kitengo ili uwe mnufaikaji. Kama unania njema na chama cha walimu, kwa nini usipiganie kuboresha chama kilichopo? Acheni kuwafanya watu mbumbumbu, nyie ni wachumia tumbo na vibaraka wa serikali aka ccm.
 
ndugu sheria hizohizo za ajira ndo zinazounda vyama vya wafanyakazi ikiwemo na cwt, ebu soma historia kidogo hivi vyama havikuanza leo wala jana toka enzi za chatism na judism.kumbuka kila penye mkusanyiko hata wa watu wawili ni lazima pawe na kiongoz hata dini zinasema hivyo,kuhusu maisha mazuri ya viongoz hii ni kawaida hata kidini ama kisiasa raia hafanani na kiongoz kutokana na hadhi yake
 
Na wewe utakuwa mnufaika wa chama kipya au unatafuta kupewa kitengo ili uwe mnufaikaji. Kama unania njema na chama cha walimu, kwa nini usipiganie kuboresha chama kilichopo? Acheni kuwafanya watu mbumbumbu, nyie ni wachumia tumbo na vibaraka wa serikali aka ccm.

upo sawa kabisa,wtz kwa kuanzisha vyama vipya hatujambo lengo ni tumbo tu hakuna lolote,
 
kumbe mnajua kuwa kila aina ya wafanyakazi ni lazima wawe na chama cha kuwasemea,sasa wewe mwl unataka tuongozane wote kwa waziri kudai stahiki zetu?cwt inamapungufu ila kinasaidia sana,hapa nilipo mimi kuna walimu 7 walitakiwa kufukuzwa kazi ila cwt ikasimama imara kuwatetea wote wamerudushwa kazin,sasa wewe unaoshawishi wenzako kusema no kwa cwt bado halijakukuta

Nadhani hujaelewa hii post na umereply kabla ya kuelewa. Hakuna alosemanhakuna umuhimu wa vyama vya wafanyakazi kinazungumzwa hapa ni cwt kupunguza ukiritimba wao wa makato sababu tayari wana vitega uchumi, kuacha kuwaingiza watu kwenye makato automatic kwa sababu sasa hivi kuna vyama vitatu vya kutetea walimu, walimu wawe huru kuchagua chama wanachotaka kutokana na sera za chama husika kama tunavyochagua mifuko ya pensheni...
 
mimi ni mdau wa cwt na declare interest,cwt sasa inaelekea kubadilika kwa katiba mpya ya cwt wastaafu wote watapewa mkono wa kwaheli,pia katika kila ngaz ya uongoz wameweka nafasi ya vijana ili kuleta mabadiliko katika utendaji lakini pia kuna kitengo cha dharura wewe mwl kama umefiwa na mtu wa karibu unauguliwa nenda kwenye tawi la cwt ukiwa na kitambulisho utasaidiwa.kama kuna swali niulizeni ila ctokuwa hewani muda wote

Katiba mpya ya mwaka gani unayozungumzia hapa??
 
Back
Top Bottom