Nimekula chumvi nyingi hivyo najua mihemko ya Taasisi ya Rais, imekuwa ni utaratibu wa tawala zetu hapa nchini kuja na mihemko na kutoa ahadi nyingi ili kuongeza mapambo katika sanaa za siasa.
Nakuja na mapendekezo yafuatayo ili kuepuka majoto:
1. Ni wakati sasa ianzishwe taasisi ya House of Lord ili kulainisha mihemko ya wanasiasa wanaokuwa madarakani na wale wanaotarajiwa kuwa madarakani.
2. Uuzaji au ukodishwaji wa mali kubwa za nchi lazima house of lord wapite kwa wananchi kupata one to one vote kuruhusu hilo kufanikiwa. Mf, ukodishwaji wa Bandari kwa Kampuni za kigeni na kuiacha serikali na ugonjwa wa kukopa mikopo kusaidia bajeti ni swala gumu kulielewa.
3. Rais anapokuwa na jambo lazima house of lord waruhisiwe kufanya dialogue na maamuzi kufikiwa. Baraza la mawaziri wanamuogopa raisi sababu wote ni wateule wake. Mawaziri pia iwe ni nafasi huru either mbunge au mtaalamu aweze kuomba kuwa waziri na house of lord washirikiane na raisi katika kumhoji mhisika na sio nafasi ya fadhila.
Pia soma: Kauli ya Rais Samia na Musatakabali wa Jeshi la Polisi, TISS na Vyombo vingine vya Usalama
4. Mabadiriko yoyote yanayohusu Muungano lazima house of lord wafanye questionare kwa Watanzania na kuja na referandum. Kwa mfano Tanganyika kuongeza asilimia ya gawio la makusanyo ya kodi kwa unguja lazima kuwe na kura ya pamoja na ihusishe watu huru sio wanasiasa peke yao.
5. Siasa za uchumi ziwe wazi haiwezekani wananchi wapambane wagundue madini au gesi lakini kwa maamuzi ya mtu mmoja analeta taarifa yenye utata eti mabeberu walishaichukua hili linahitaji kula ya wazi kuweza kuafikiana,hii lonaleta shida nchi ina gesi lakini nchi inakuwa na bajeti inayotegemea wahisani Hili pia linaleta ukakasi. Maendeleo ya vitu yaambatane na maendeleao watu,haiwezekani Kodi ilipwe lakini huduma ziwe chini ya kiwango.
6 .Natamani paper ya kilimo kwanza iweze kupitiwa upya na kufanyiwa kazi kama wataalamu wameshindwa kumaliza kero za masoko na hata majukwaa ya wanasiasa wanakosa majibu sahihi kwa wakati sahihi.
7. Napendekeza pia Tanzania ipime uzito na kuona kama kuna ulazima wa kutumia Dola kwa manunuzi katika nchi yetu.
8. Kuhusu Ardhi, watu wanauwana sana sana hili nalo linahitaji kutizamwa kwa namna nyingine.
Tanzania haiwezi kufa kama vile walivyosema " Serengeti will never die!"
Ahsanteni.