Ni wakati wa kuwa na House of Common iliyo juu ya Bunge ili kusimamia Taasisi ya Rais

Sioni mahusiano ya hii mada yako na hiyo picha hapo juu.

Una mapendekezo mazuri sana, lakini tumeshakosea kama nchi kwani mfumo ccm umeshateka kilankona. Ili haya mapendekezo yako yafanye kazi, ni aidha machafuko, ama mapinduzi ya kijeshi ili tuweke huu mfumo unaoupendekeza.
 
Punguza utoto dogo.
 
Lakini tukiwa na katiba ambayo yote hayo yataangazwa tusiogope.

Ila kusema ukweli tabia za hawa CCM zimelichelewesha Taifa kupiga hatua, wanatabia ya unyumbu wa kisiasa.

unyumbu wa kisiasa ni tabia ya watu wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumika kundi fulani kwa masilahi binafsi ama uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data ama kuahirisha kufikiri kizalendo
 
Nakubaliana na hoja hii maana itaepusha Nchi kuongozwa kifamilia. Ule utaratibu wa MIHIMILI umeshindwa kwani inaonekana mmoja ndio unawafadhili wengine. Utaratibu huu wa ushirikishwaji uhimizwe uanze mapema maana deni la Taifa linakuwa kwa kasi kubwa na ni mzigo kwa wananchi wote waliowaamini Viongozi wao waamue badala yao lakini inaonekana inatumika kwa maslahi binafsi ya kujihakikishia kuendelea kuwepo madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…