Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Kitu kilchotokea Israel ni kibaya zaidi katika historia ya nchi hiyo.Na yote ni kutokana na siasa za ubabe wa Benjamin Netanyahu.
Siasa zake hizo imekuwa sababu ya kuwakasirisha zaidi wapalestina ambao sasa wameamua kujitoa muhanga kupambana badala ya kulia lia na kuomba kuhurumiwa.
Wananchi wa Israel kwa upande wao wana sababu ya kuendeleza maandamano yao kumuondoe kiongozi huyo na sio kumuunga mkono katika matangazo yake ya kulipiza kisasi kwa makosa ya kiongozi wao.
Kuendelea kwa mikakati ya vita ijapokuwa Israel ina nguvu kubwa ya kijeshi lakini huenda ikaleta msuguano wa kivita wa muda mrefu kuyavuta mataifa mengine ya Kiarabu na ulimwengu wa kiislamu kuamua kuingilia kati kuwatetea wapalestina.
Hilo la kubadilika kwa mawazo yaliyolala ya mataifa hayo mengi yao yakiwa ni jirani na Israel ni jambo linalochochewa na kauli za kuunga mkono kwa nguvu zinazotolewa na mataifa ambayo yana urafiki na Israel kama vile Marekani,Ufaransa,Canada,Uiengereza na Ukarine ambao bila kificho wamesema wanaiunga mkono Isreael na wataipa msaada ili kujilinda.
Umuhimu huo wa kujiuzulu unaongezeka kutokana na afya yake ya moyo ambapo mambo yakienda kombo zaidi yanaweza yakamzidishia matatizo hayo ya kuifya na kulazimika kuachia katikati ya vita jambo litakalowapa ushindi Hamas mara mbili zaidi.
Ni ushauri tu.