mazaga one
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 2,514
- 4,042
Wadau wa Michezo na Watanzania wote kwa ujumla,kama mlivyosikia ya kuwa uwanja wa Mkapa umefungiwa na CAF na timu yetu ya Simba hivi karibuni ina mechi ya Robo fainali ya mashindano ya CAF,kama Taifa,tunahitaji kuona serikali ikisimama na Simba kupigania maslahi ya Simba.Tarehe 20/03/2025.Nimeona ya kuwa CAF watakuja kukagua uwanja.Ombi letu ni Serikalai na TFF kuhakikisha wanapigania hili jambo na Simba icheze mechi yake ya marudiano nyumbani.Ukiangalia kwa jicho la mbele ni kwamba Simba inaenda kuchukua hili Kombe na ni kama figisu zishaanza mapema kulidhoofisha Taifa letu.Tupiganie uwanja wetu ufunguliwe mapema na 09/04/2025 mechi ya Robo fainali ichezwe kwa Mkapa na sio ugenini.
Serikali na TFF tuna imani nanyi.
Serikali na TFF tuna imani nanyi.