Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 7,672
- 9,039
Japo wengi wanachukia kifo, kuna ukweli kuwa kifo ndiyo kitu pekee kinachotenda haki kuliko vingine. Mvua inaweza kunyesha lakini si dunia nzima. Kifo kipo kila mahali dunia nzima. Furahi ipo duniani lakini siyo kwa watu wote. Ni kifo pekee kinachosawazisha mambo. Mbali na kifo, kinachofuatia ni uhai ambao huanza pale mimba inapotungwa ingawa nayo huonja mauti hata kabla ya kuzaliwa kwa zilizo nyingi. Je zaidi ya kifo, ni kitu gani kinatenda haki kwa usawa duniani?