Ni wapi bado tunahitaji sauti zaidi za wanawake? Je, ni katika Siasa, Elimu au Biashara?

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Wanawake wanaposhiriki katika maamuzi, huleta mitazamo mipya yenye nguvu za kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu.

Ushiriki wao unaleta uwiano wa kijinsia unaohitajika katika kila sekta – iwe ni siasa, biashara, jamii au elimu.

Tunapozingatia changamoto nyingi zinazokumba jamii zetu, kama vile ukosefu wa haki, ukatili wa kijinsia, na maendeleo duni, ni wazi kwamba sauti za wanawake zinahitajika zaidi kuliko wakati wowote.

Wanawake wanapopewa nafasi ya kuchangia katika meza ya maamuzi, tunaona mabadiliko ya kweli, kuanzia sera bora za kijamii hadi maendeleo ya kiuchumi.

Swali ni, je, ni wapi bado tunahitaji sauti zaidi za wanawake? Ni katika siasa, ambapo ushiriki wao unaweza kuleta sera zinazojali usawa wa kijinsia?

Au ni katika biashara, ambapo uongozi wao unaweza kuchochea ubunifu na ufanisi?

Tuchague kushirikisha na kuimarisha wanawake katika maamuzi ili kuleta mabadiliko chanya kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Wewe unaona ni wapi tunahitaji kuongeza juhudi zetu kuhakikisha sauti za wanawake zinasikika zaidi?”
 
Kwa mtazamo mimi naona Tanzania usawa wa kijinsia upo sana hata kwenye sekta hizo ulizozitaja. Hata kama uwiano sio sawa nadhani hakuna kinachomfunga au kumzuia jinsia KE kuingia katika sekta hizo tajwa hapo juu !!

Kitu ambacho hakiwezekani kuwa na usawa ni kwenye suala la ndoa.
 
Kwa kutizama mwenendo wa kiuongozi na kimaendeleo hasa ktk awamu hii ambayo wanawake wamepewa dhamana za juu kimaamuzi, ni dhahiri wakina mama wanapaswa kubaki kuwa walezi wa watoto na wapishi wa chakula kitamu jikoni.
 
Wanawake wanaposhiriki katika maamuzi, huleta mitazamo mipya yenye nguvu za kuleta mabadiliko chanya na ya kudumu.

Ushiriki wao unaleta uwiano wa kijinsia unaohitajika katika kila sekta – iwe ni siasa, biashara, jamii au elimu.

Tunapozingatia changamoto nyingi zinazokumba jamii zetu, kama vile ukosefu wa haki, ukatili wa kijinsia, na maendeleo duni, ni wazi kwamba sauti za wanawake zinahitajika zaidi kuliko wakati wowote.

Wanawake wanapopewa nafasi ya kuchangia katika meza ya maamuzi, tunaona mabadiliko ya kweli, kuanzia sera bora za kijamii hadi maendeleo ya kiuchumi.

Swali ni, je, ni wapi bado tunahitaji sauti zaidi za wanawake? Ni katika siasa, ambapo ushiriki wao unaweza kuleta sera zinazojali usawa wa kijinsia?

Au ni katika biashara, ambapo uongozi wao unaweza kuchochea ubunifu na ufanisi?

Tuchague kushirikisha na kuimarisha wanawake katika maamuzi ili kuleta mabadiliko chanya kwa vizazi vya sasa na vijavyo.

Wewe unaona ni wapi tunahitaji kuongeza juhudi zetu kuhakikisha sauti za wanawake zinasikika zaidi?”
Wabaki kwenye burudani tu
 
Kwenye elimu na ajira hasa za masomo ya sayansi na degree zake kama Engineering , teknolojia,geology ,udaktari,pharmacy ,Architecture nk uwiano wa wanawake na wanaume bado uko chini mno hasa viwango vya degree kwenye ajira sekta ya umma na binafsi wanaume bado ndio dominant population
 
Nadhani nimefikia hatua katika maisha yangu, naona bora ningekuwa mama wa nyumbani.

Nikisema hivi napata uzito sababu naona ninaangusha watu walionyuma yangu (wadogo zangu, binti yangu) na wanaonitazama na kutamani kuwa nilipo, lakini hawajui tu yaliyomo moyoni. Mimi roho yangu bwana ipo nyumbani kuhudumia familia yangu. Niache bwana mkubwa apambane kwaajili yetu
 
Back
Top Bottom