Ni wapi naweza kupata nyama safi ya Kitimoto for the weekend hapa Dar

Mbona hukumwambia aende na pale ccm Lumumba na kila siku wanapikia mle ndani kama lunch yao? Pia ikulu ipo JK anawapa wakatoliki mle ndani. Jana karudi naye mzima toka songea
Hivi kuna umuhimu wowote wa posti kama hii??
 

Cafe Latino naona hakubambi sana siku hizi..halafu pamebadilika kweli pia Sisimizi sababu ya barabara!!..

Karibu siku nyingine migombani-savei mana hapazeeki pale!..jioni kama ya leo ni kufurahia weekend na nyama yetu katoliki!!
 

Mwezi wa toba kaka
 
Nenda morogoro road baada ya kituo cha polisi kwa yusufu pita shule ya mbezi high mbele kidogo kuna bango mkono wa kushoto "insalaga" sorry kama jina nimekosea kidogo ila ita-enjoy.
 
B bar pale kwa Remmi Sinza,tena hapo utakutana na batoto ba mjini
 
Elli avatar yako inanitia machungu sana na hii serikali dhalimu, siku ya kupata uhuru wa kweli kutoka ccm tutaweka movie tuangalie tulikotoka haki ya dona shahidi maharagwe ninavyowaona police hata wakija hospitali natamani hata nisiwaone ningetukana lakini naogopa ban. ila unawakilisha sana mkuu.
 
hahaaa avatar kweli naona kuna haja ya kui-modify ila nimeeipenda kwasababu inatukumbusha wajibu wetu kwa taifa, lakini pia LEO KUNA PROMOSHENI YA MATUSI WAWEZATUKANA TUSI lisilozidi herufi tano na kisitaje viungo vya mwili kama "kufikiria kwa makalio" ya kitimoto
 
Maneno yote ni Mwenge pale nyuma ya TRA karibu na magorofa ya jeshi kuna bingwa anaitwa CHUWA,kuna jamaa alinipa ushuhuda kuwa hakuwahi kula nyumbani kwake kwa siku kama 20 hivi mfululizo maana kila jioni lazima aripoti hapo, ukila rosti unaweza kumtaliki mkeo,mimi huwa nabeba na mkate kabisa wa kumalizia ile rosti.
 
Nenda pale Green Park Pub makondeko kama unaelekea Kibamba.
 
Haya nitajitahidi nikapate "mnyama" huko
 
Jamani nataka member 10 tukale sote ntalipa garama zote za mnyama,,,,,vinywaji ntachangia 20x10 ukitaka zaidi utajazia mnakaribiwa kuni pm,ntanchagua kwa mtindo wa kwanza ku pm niko dsm
karibuni,tuanze mwaka vizuri
 
Jamani nataka member 10 tukale sote ntalipa garama zote za mnyama,,,,,vinywaji ntachangia 20x10 ukitaka zaidi utajazia mnakaribiwa kuni pm,ntanchagua kwa mtindo wa kwanza ku pm niko dsm
karibuni,tuanze mwaka vizuri

Haya wee, mimi nijumuishe..lini tarehe ya kwenda? na wapi? au kila kitu utakuwa umepanga wewe?
 
Fuldoz mabibo baada ya TGNP mbele kidogo unaingia kulia kuna kitu cha ukweli pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…