Ni wapi nitapata hospital au mtaalam wa kutibu tatizo la macho?

Ni wapi nitapata hospital au mtaalam wa kutibu tatizo la macho?

proxy

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
1,479
Reaction score
1,348
Habari za mchana wandugu,

Mwanangu ana tatizo la macho, akiwa anaangalia anafanya kama haoni vizuri, yaani macho anafumbua kwa mbali. Hii hali hutokea zaidi kwenye jicho moja, pia akiwa ameshika kitabu huwa anasogeza sana karibu na macho ili aweze kusoma vizuri.

Nimempeleka hospital moja ya rufaa wameniambia walikuwa na wataalamu wa macho hapo lakini kwa sasa wamerudi kwao yaani nje so mpaka wafike tena ndio wanipe taarifa ili mtoto atibiwe.

Ombi langu ni hili ni wapi unaweza pata maspecialist wa macho kwa tatizo la mwanangu?
 
Ungeandika mkoa uliopo ili iwe rahisi kwa mtu kukushauri sehemu ya wataalamu wa macho. Kama ni mkazi wa Dar, Mwanza, Arusha, Mbeya nk. sehemu zipo nyingi za wataalamu wa macho.
 
Kama upo Dar, anzia Muhimbili, kwa sasa wapo vizuri. Kama ni issue ambayo inahusu operation, usifanye mpaka umeenda CCBRT na KCMC kwa second opinion ili kama wote wakisema issue ni hiyo hiyo, afanyiwe sehemu utakayopenda.
 
Mimi mwenyewe nilitaka mwenda KCMC but watu wengi wananishauri niende CCRBT
 
Habari za Asubuhi wana jamvi mahususi wa mliodondosha michango yenu,

Naomba nilete mrejesho wa tatizo la macho nililokuja na kuomba msaada hapa kwa mwanangu ,Nimeenda CCBRT nimeambiwa mtoto ana watoto wa macho kwenye macho yote mawili so inatakiwa afanyiwe operation kwa baadae, yaani hapa nilipo nimetingwa kwa kusikia neno operation.

So naomba kuuliza kwa wazoefu wa hizi operations za macho huwa zinakuwa na ufanisi upi ili mtu arejee kwenye uwezo wake wa kuona kama kawaida?
 
wakubwa naombeni ushauri kuhusu afya ya macho yangu
Kila nikikodolea macho screen ya simu au computer yanapata joto sana na wakati mwingine yanawasha na kutoa machozi
 
wakubwa naombeni ushauri kuhusu afya ya macho yangu
Kila nikikodolea macho screen ya simu au computer yanapata joto sana na wakati mwingine yanawasha na kutoa machozi
Nenda kapime kwa optician
 
Ndugu yangu anasumbuliwa na tatizo la macho( kutoona vizuri), mchana haoni kitu chochote ni giza tu lakin usiku anaona kwambaliii sana tatizo hilo limekuwa sugu kwani tangu aanze kuumwa ni takribani miezi 6 sasa, kama kunamtu anajua tiba ya ugonjwa huu au hata ushauri pia ni muhimu sana. nawasilisha!
 
Nenda kwa specialist wa macho, Kairuki, muimbili, bugando au Agha khan
 
Back
Top Bottom