Ni wapi panafaa kwa kuanzia maisha kwa kijana anayeanza kujitegemea?

Ni wapi panafaa kwa kuanzia maisha kwa kijana anayeanza kujitegemea?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2016
Posts
4,701
Reaction score
11,920
Wakuu heshima kwenu,

Sitaki kuwachosha sana.

Binafsi nilipata kibarua cha muda mfupi ktk mkoa fulani, kibarua changu kinakaribia kuisha, na sitaki kabisa kurudi home.

Kiukweli nimekuwa nikiumiza sana kichwa maisha yatakuaje baada ya hiki kibarua kuisha, nimejibana nkakusanya milioni moja.

Lengo la huu uzi ni kuwauliza walionitangulia, kati ya mjini (majiji, mikoani) na wilayani ni sehemu gani nzuri kwa kijana anayeanza maisha?

NB: Uandishi wangu sio mzuri, lengo ni kufikisha ujumbe wangu kwenu ili mnishauri na kunipa msaada wa mawazo.

Pia unaweza kushare jinsi ulivyoanza maisha ili iwe rahisi kujifunza, naamini na wengine watafaidika pia.

Natanguliza shukrani.
 
Mkuu milioni ni kubwa sana trust me ilimradi huko unajifanya kibarua tayari unavyombo na vitu vya ndani. Uswazi kwenye majiji na wilayani unapata hata chumba cha elfu 15. Wazo lako la biashara inabidi lijihusishe na jamii kwaaailimia 100. Kama ni kuuza nafaka chagua mtaani kabisa. Kama ni kukaanga mihogo,kuku na viazi hii biashara inaingiza 20 kwasiku na inaweza kuwa zaidi ya hapo kutegemea na eneo.

Unaweza pia point nguo za kike za mtumba dar kwamujbu wa jooohs ni elfu 1500 mpaka 4000 then unauza eneo ulilopo kwa elfu 8 hadi 12 kutegemea na eneo.
 
Milioni 1 ni nyingi sana hiyo mkuu...ila usiwe bishoo pale mbagala kuna wamachinga walianza biashara chini ya elfu 50 now ni stori tofauti.La msingi na la kuzingatia mtafute mtu mzoefu atakusaidia hasa hizi biashara ndogo ndogo ukiwa fresh unahamia kwenye ishu zingine.

Kuna mwaka mmoja kama sikosei 2014/2015 tumekaa home akaja jamaa mmoja yeye alisema ametoka jela siku 2 zilizopita na yeye Dar es salaam hana ndugu ndugu zake wote wapo Kigoma na hataki kurudi kwao hivyo aliomba tumsaidie vitu vifuatavyo.

1. Mavazi na viatu(shuka aliomba na kanga mbili)
2. Ndoo mbili ndogo za maji
3. Mtaji wa angalau elfu 15

Alilenga kuuza maji ndo kitu alichotaka,na kama hatumuamini basi tuongozane mpaka dukani tumnunulie,,kwa kuwa aliomba hivyo vitu tukampa vyote tukampa na chakula nakumbuka mama alimuongeza jumla alipata 35k akaondoka nilikutana nae 2018 Rang 3 kule tena nilishamsahau ,yeye ndo alinishtua anauza saa,makava ya simu,earphone,cheni,pete na vitu vingine vidogo vidogo maisha yanaenda kwa sasa alikua tofauti na alivyokuja.

Pia nina rafiki yangu yeye ni Muha anakopesha vitu jamaa kazi yake ngumu kwa kua anatembea sana ila anadai mwisho wa mwezi anapiga pesa ndefu 400k -800k na kwa elimu yake ya darasa la saba sio mbaya.Akanipa mfano aliwahi nikopesha mapazia mawili kwa elfu 36 wakati yale yote alinunua kwa elfu 8 na mia 5 kwa kila moja jumla elfu 17 kwa mawili anapopajua yeye nadhani unaona hapo faida ailiingiza sh ngapi.
 
mkuu milioni ni kubwa sana trust me ilimradi huko unajifanya kibarua tayari unavyombo na vitu vya ndani..... uswazi kwenye majiji na wilayani unapata hata chumba cha elfu 15....wazo lako la biashara inabidi lijihusishe na jamii kwaaailimia 100.....kama ni kuuza nafaka chagua mtaani kabisa, Kama ni kukaanga mihogo,kuku na viazi hii biashara inaingiza 20 kwasiku na inaweza kuwa zaidi ya hapo kutegemea na eneo,

unaweza pia point nguo za kike za mtumba dar kwamujbu wa jooohs ni elfu 1500 mpaka 4000 then unauza eneo ulilopo kwa elfu 8 hadi 12 kutegemea na eneo....


Ila tuseme ukweli...kutokana na ihalisia wa maisha ya sasa! Muuza kuku za kukaanga /mishikaki nadhan atapata wateja zaidi kuliko mdaka nguo za kupoint!naona kama kaupepo kamechange!..bora kukomaa na kukaanga kuku na mishikaki
 
Wala si kile ambacho nilitaka kuandika si hicho lakin yote kwa pamoja kwa mtaji alio nao unaweza kufikisha mbali sana isipokuwa tu kama atafanya biashara ambayo itaendana na nyakati hizi,hasa biashara ya chakula kwa ujumla itamutoa kimaisha
Mleta mada...
Nakushauri uwe mwenye tahadhari sana na comments za aina hii
 
Ila tuseme ukweli...kutokana na ihalisia wa maisha ya sasa! Muuza kuku za kukaanga /mishikaki nadhan atapata wateja zaidi kuliko mdaka nguo za kupoint!naona kama kaupepo kamechange!..bora kukomaa na kukaanga kuku na mishikaki
ni kweli madam upepo ukitulia na akiwa amepata faida kwenye kukaanga kuku/mishikaki anaweza fanya zote na hiyo ya kupoint....Sahizi akomae na vyakula
 
Back
Top Bottom