Ni wapi panafaa kwa kuanzia maisha kwa kijana anayeanza kujitegemea?

Ni wapi panafaa kwa kuanzia maisha kwa kijana anayeanza kujitegemea?

mkuu ile idea yako ya vyombo kupeleka mnadani kwa huo mtaji haifai?(Nimeiona katika moja ya nyuzi zako)
Naiona ndefu sana(anaweza anza na 400k tu)!....kuna mikoa wanapenda sana zile mambo aisee imagine kikombe unauziwa 300!sahani 500!...ni wewe tu na mwamvuli wako na mpiga debe!
 
Hiyo hela ni nyingi sana kama una nidhamu na uvumilivu. 2009 nikikaa maeneo ya Loyola nilimpa kijana Mrombo shilingi elfu 70 akaanza uza chipsi mayai na mishikaki ya 50. Sasa hivi ana duka kubwa Mabibo mwisho na vibanda viwili vya chipsi mabibo hostel. Bodaboda mbili pia.
 
Mkuu naomba idea yako ya vyombo uiweke hapa itatusaidia na wengine....nataka niingie kujiajiri rasmi

Mkuu kuna uzi niliandika humu ucjek unaweza pata abc...! Ni vile vyombo vya plastic vya bei ya chini...!minadani....! Means vikombe vibakuli sahani..chujio..miko..sufuria size ya kati nk nk!
 
Mkuu, ushauri wangu wa kwanza ni kwamba hakikisha ukiingia mjini usikae maeneo ya gharama. Tafuta chumba cha kawaida lipia miezi sita huku ukipambana hasa ukiamua kuja Dar es Salaam
 
Wakuu heshima kwenu,

Sitaki kuwachosha sana.

Binafsi nilipata kibarua cha muda mfupi ktk mkoa fulani, kibarua changu kinakaribia kuisha, na sitaki kabisa kurudi home.

Kiukweli nimekuwa nikiumiza sana kichwa maisha yatakuaje baada ya hiki kibarua kuisha, nimejibana nkakusanya milioni moja.

Lengo la huu uzi ni kuwauliza walionitangulia, kati ya mjini (majiji, mikoani) na wilayani ni sehemu gani nzuri kwa kijana anayeanza maisha?

NB: Uandishi wangu sio mzuri, lengo ni kufikisha ujumbe wangu kwenu ili mnishauri na kunipa msaada wa mawazo.

Pia unaweza kushare jinsi ulivyoanza maisha ili iwe rahisi kujifunza, naamini na wengine watafaidika pia.

Natanguliza shukrani.
mkuu hebu pitia uzi unaitwa ulianzaje kuishi geto tumetupia mambo meng bila shaka utapata kitu
 
Back
Top Bottom