Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 301,577
- 754,412
Kuna mchezo kama si wa kijinga basi ni wa kitoto unachezeka hapa..!
Watekaji mahiri hukuteka kwa lengo maalum kama si kisasi basi ni mambo ya kisiasa ama kikomboleo (ransom)
Sakata la Shadrack kwa mazingira yote ni la kisiasa.. Ni kijana fukara hana visasi na watu wanaoweza kumteka..labda kama kisasi kitokane na yeye kulipiwa faini na watanganyika wenzake kwenye kesi iliyokuwa inamkabili
Alilipiwa faini na akatolewa gerezani na mambo yakaishia hapo.. Lakini mara ghafla akatekwa na kupotea kusikojulika licha ya kelele zote kila kona ya nchi. Baba yake mzazi alishaomba apewe hata kama ni maiti ya mwanae amzike kama imeshindikana kumrudisha, lakini bado imeshindikana.
Sasa hivi karibuni kuna watu wamempigia baba yake wakimtaka awapatie milion 3 ili wamrudishe mwanae(pengine akiwa hai) Sasa hapa kuna maswali ya kujiuliza
Hawaogopi police? Hawaogopi kujulikana? Mbona hawakumpa masharti yoyote kama ya kutoripoti polisi?
Cha kushangaza zaidi baba mtu kaenda polisi, katoa taarifa na mawasiliano yote.. Lakini hakuna kilichofanyika hadi sasa
Je ni watekaji wenyewe ama ni matapeli walitaka kumpiga Mzee wa watu hela?
Soma Pia: Baba Chaula: Nimepigiwa simu na namba ngeni, kaniambia nitoe Tsh. Milioni 3 ili Chaula apatikane