Ni wazi Haji Manara na Hersi haziivi tena

Ni wazi Haji Manara na Hersi haziivi tena

Kuna taarifa kutokea viunga vya corridor za Yanga kuwa Haji Manara na Mhandisi Hersi ambaye ni Rais wa Yanga haziivi.

"....hujiulizi kwa nini hata hajaposti picha za Hersi akiwa Ufaransa na boss wa Man City kwenye Mkutano wa ECA? Kwa taarifa yako, Manara amemkasirikia Hersi eti kisa usemaji wa Yanga kubakishiwa Kamwe. Jamaa ana nyongo ya kishamba sana yule!"

Duru.
Kumbe yuko Ufaransa,
Kweli Manara levo za juu saana
Tunaomchukia tuendelee tu kuumia na kumlingishia usemaji wa club
 
yanga sahivi inaenda kiprofeshino inaenda level za kimataifa haitaki mambo ya kiswahili ww si unamuona hata injinia Hersi ni kiongozi smart hawezi kuendana na mswahili na mropokaji majinuni
Yeah,ameacha kuvaa jezi za wapinzani wa simba kimataifa na haendi airport kuwapokea kama zamani
 
Hivi usemaji wa timu ni dili sana? Nilisoma mahali kuwa Manara baada ya kifunga chake alipewa nafasi ya ukurugenzi wa wanachama na uhamasihaji lakini hakuridhika alitaka usemaji tu. Huenda ni kwa vile Ukurugenzi hauwezi kumweka mbele ya maikrofoni na kamera sana kama usemaji.
 
Simba mchukueni shabiki na pia msemaji wenu wa zamani basi. Maana hana tena thamani kwenye timu ya Wananchi.
Huyu c ndo yule aliewakogesha kila aina ya matusi na kashfa,kisha mkamchukua hakika aliewaita utopwinyo aliwaza mbali sana.
 
Huyu c ndo yule aliewakogesha kila aina ya matusi na kashfa,kisha mkamchukua hakika aliewaita utopwinyo aliwaza mbali sana.
Wewe kijana wa Mangungu, huyu Haji Manara aliajiriwa na GSM! Tena aliajiriwa kwa lengo la kumlisha matapishi yake mwenyewe. Na GSM siyo Yanga kama ilivyo kwa timu yako ya Simba ambayo tayari ni mali ya Mo (kwa maelezo yake)!
 
Kumbe yuko Ufaransa,
Kweli Manara levo za juu saana
Tunaomchukia tuendelee tu kuumia na kumlingishia usemaji wa club
Unasoma bila kuelewa kilichoandikwa, aliyepo Ufaransa ni Eng. Hersi
 
Ukiishi kwa upanga, utaondoka kwa upanga, maisha yake ya mpira ameendesha kwa finna, na fitna ndio zitamuondoa.

Hana chain of command, kila siku yuko kwa GSM bila kupitia kwa immediate boss. Na huo ndio mwisho wake
 
Moja ya vitu vya kifara kuwahi kufanywa Yanga ni kumchukua huyu mzee. Eti tulimchukua kisa ana followers kibao insta. Ukiuliza hao followers ni wapi unaambiwa ni vichwa panzi kama mwasibu muanzisha nyuzi wa jf.
 
Back
Top Bottom