Ni wazi mchuano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu umeipasua CHADEMA, na kuibua mgawanyiko wa kikanda, kikabila, na kimikoa

Ni wazi mchuano wa Freeman Mbowe na Tundu Lissu umeipasua CHADEMA, na kuibua mgawanyiko wa kikanda, kikabila, na kimikoa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hata hivyo, sura zaidi ya sekeseke hili zinatarajiwa kujitokeza ikiwa ni pamoja na sura ya kizalendo na ile ya ukibaraka, nazo zitachukua mkondo wake kwa wakati muafaka.

Mpaka sasa,
tayari kuna kanda, makabila na mikoa yao imeonyesha wazi wazi kumuunga mkono mwenyekiti wa wa sasa wa Chadema, na zipo kanda, kabila na mikoa ambayo tayari imejipambanua kumuunga mkono makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa wa sasa.

Kwa mtazamo wako kisiasa,
kati ya mafahali hawa wawili wa Chadema, wanao mezea mate nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa,

Ni nani kati yao,
anaungwa mkono na kanda nyingi zaidi na zenye wajumbe wengi zaidi, na ana nafasi kubwa zaidi ya kuukwaa uenyekiti wa Chadema Taifa kirahisi zaidi ya mwingine?

Mathalani,
Kanda ya Pwani na kaskazini, tayari zimeonyesha sura ya ghafla wazi wazi kabisa ya kumuunga mkono mwenyekiti wa sasa wa Chadema katika ujumla wake bila kupepesa macho.

Lakini pia,
Kanda za Serengeti, Nyasa Magharibi na ile ya Viktoria zenye jumla ya mikoa zaidi ya15, wajumbe wake wamegawanyika kulingana na makabila na mikoa yao, na baadhi yao walionekana katika siku ya kutangaza nia ya kugombea uenyekiti, makamu mwenyekiti wa Chadema anaemaliza muda wake.

Kwa ujumla,
wapo wanamunga mkono Mbowe lakini pia wapo wanaomuunga mkono Lisu.

Friends, ladies and gentlemen,

Uchaguzi ni numbers na mipango.
Nani ana mipango mikakati na numbers kubwa zaidi, kuliko kukurupuka, makelele na mdomo?🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Wekeni bango Moja basi. Maana hatujamaliza kusoma hili mnaweka jingine.

CCM yenu hamfanyi uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa lakini mpo Siti ya mbele kushadadia uchaguzi wa CHADEMA.
Pole sana bongo lala injini moja dah!
samahani sana gentleman,

tunafanya haya yote kwa nia njema tu wakati huu wa kutangaza nia, ili hatimae tumalizane na jambo hili na tuanze rasmi sehemu ya kampeni ambayo kwakweli ni ya moto sana, kwa wakati muafaka.

tuvumiliane tu ndrugu zangu wadau wa siasa za vyama vya siasa 🐒
 
Kitemdo cha media kubwa za humu ndani kushadidia kusudio la Lissu ilikuwa ni kumuingiza kingi ili ije propaganda ya kwamba CHADEMA imepasuka mapande mapande ya kikanda, mikoa na kabila na kuifanya ccm ndiyo chama cha kitaifa au ilikuwa na kumpamba Lissu tu?
 
Hata hivyo, sura zaidi ya sekeseke hili zinatajitokeza ikiwa ni pamoja na sura ya kizalendo na ile ya ukibaraka, nazo zitachukua mkondo wake kwa wakati muafaka.

Mpaka sasa,
tayari kuna kanda, makabila na mikoa yao imeonyesha wazi wazi kumuunga mkono mwenyekiti wa wa sasa wa Chadema, na zipo kanda, kabila na mikoa ambayo tayari imejipambanua kumuunga mkono makamu mwenyekiti wa Chadema Taifa wa sasa.

Kwa mtazamo wako kisiasa,
kati ya mafahali hawa wawili wa Chadema, wanao mezea mate nafasi ya uenyekiti wa chama hicho Taifa,

Ni nani kati yao,
anaungwa mkono na kanda nyingi zaidi na zenye wajumbe wengi zaidi, na ana nafasi kubwa zaidi ya kuukwaa uenyekiti wa Chadema Taifa kirahisi zaidi ya mwingine?

Mathalani,
Kanda ya Pwani na kaskazini, tayari zimeonyesha sura ya ghafla wazi wazi kabisa ya kumuunga mkono mwenyekiti wa sasa wa Chadema katika ujumla wake bila kupepesa macho.

Lakini pia,
Kanda za Serengeti, Nyasa Magharibi na ile ya Viktoria zenye jumla ya mikoa zaidi ya15, wajumbe wake wamegawanyika kulingana na makabila na mikoa yao, na baadhi yao walionekana katika siku ya kutangaza nia ya kugombea uenyekiti, makamu mwenyekiti wa Chadema anaemaliza muda wake.

Kwa ujumla,
wapo wanamunga mkono Mbowe lakini pia wapo wanaomuunga mkono Lisu.

Friends, ladies and gentlemen,

Uchaguzi ni numbers na mipango.
Nani ana mipango mikakati na numbers kubwa zaidi, kuliko kukurupuka, makelele na mdomo?🐒

Mungu Ibariki Tanzania.
Naona umeona uweke post ya cdm wangalau upate wachangiaji wengi kwenye post zako.
 
Lissu hawezi kuipasua CDM. Hajafikia nguvu aliyokiwa nayo Dr. Slaa - lakini yupo.wapi leo.
Gentleman,
hata mimi siwezi kuamini ikiwa Lisu anaweza kuipasua chadema, ispokua mpaka sasa, wafuasi wao wameshaanza kujikusanya kulingana na kanda zao, makabila na mikoa yao, tayari kujibu mapigo kadiri yanavyokuja 🐒
 
Hakuna ukanda hapo, wewe elewa hata Mbowe akitaka kuondoka hana ubavu wa kuipasua CDM sasa iwe Lissu.
Aliondoka Dr Slaa mfalme wa CDM ni msingi chama kikasonga..

Cha msingi ukitaka madaraka ndani ya taasisi kubwa basi fuata utaratibu.
 
Lissu anajifagilia kama mtoto yatima.
Lakini kama kuna uchafu wa siasa za kikabila ndani ya chama,nadhani umefika wakati Chadema though supportes na financials wengi ni wakati wa mlima kufungua ukurasa mpya.
Tusaidiane kufanya siasa na tawala bola bila ubaguzi.
 
Lissu anajifagilia kama mtoto yatima.
Lakini kama kuna uchafu wa siasa za kikabila ndani ya chama,nadhani umefika wakati Chadema though supportes na financials wengi ni watu wa mlima kufungua ukurasa mpya.
Tusaidiane kufanya siasa na tawala bola bila ubaguzi.
Acha propaganda wewe...

Siasa zipi za ukabila zilizoko CHADEMA?
 
Kitemdo cha media kubwa za humu ndani kushadidia kusudio la Lissu ilikuwa ni kumuingiza kingi ili ije propaganda ya kwamba CHADEMA imepasuka mapande mapande ya kikanda, mikoa na kabila na kuifanya ccm ndiyo chama cha kitaifa au ilikuwa na kumpamba Lissu tu?
Gentleman,
hushangai wiki hii muungwana anatangaza kugombea umakamu mwenyekiti wa chadema, halafu wiki ingine anabadili gia angani, anaachana na umakamu mwenyekiti, anautaka uenyekiti kamili Taifa, unadhani hili lilitokea kwa bahati mbaya?

hisabati ya siasa iligoma kabisa, na akaona picha kamili kwamba umakamu mwenyekiti hawezi kuupata kwa namna yoyote ile, Lakini pia ugombea urais ndio kiza kinene kabisa kupitia chadema.

akaona nini kifanyike sasa, ili apate fursa ya kugombea urasi na kutimiza azma yake?

ni kupambana na uzibe kile kigingi kinachomzuia asitimize ndoto zake. Na ikishindikana, tayari kuna destination ameandaa na kuandaliwa atakwenda kujaribu bahati yake huku 🐒
 
Back
Top Bottom