Ni yapi madhambi makubwa?

Ni yapi madhambi makubwa?

baby zu

JF-Expert Member
Joined
Nov 9, 2015
Posts
1,816
Reaction score
4,770
Ni wajibu kwa muumini kuyajua madhambi makubwa, na hii itasaidia kwake kuyaacha na kuyaepuka yale yote yatakayo mpelekea kuyatenda yale yatakayo mchukiza mola wake mlezi na kumuepusha na adhabu yake.
Madhambi haya makubwa yamegawanyika mara mbili
*kwa kuyatenda
Mfano kuzini, kuiba nk
*kwa kuyaacha
Mfano kuacha swala, kuacha kuhudhuria jamaa kwa wanaume
Je ni zipi kanuni za kuyajua madhambi makubwa?
Utafahamu kua hii ni dhambi kubwa kwa hukmu zifuatazo
*dhambi yenye adhabu ya Mwenyezi Mungu ktk dunia
Mfano Wazinifu kabla ya ndoa waadhibiwe mijeledi 100
Ulevi , adhabu yake bakora 80/nk
* dhambi yenye adhabu ya Mwenyezi Mungu akhera/ siku ya kiyama mfani muuaji
*kukanusha imani
Mfano Asie kua muaminifu (kufanya hiyana), mfano mzinifu muumini, mwizi muumini,
*dhambi yenye kukasirikiwa na Mwenyezi Mungu
itakayosababisha laana ya Mwenyezi Mungu iwe juu yako au kuwekwa mbali na rehma za Mwenyezi Mungu
Mfano kamlaani mwenye kula riba, wanaume wenye kujifanya wanawake ,
* dhambi yenye kukanushwa kuingia peponi
Mfano haingii peponi mwenye kuvunja undugu, mfitinishaji
* pia kuna madhambi yenye kumkufurisha mtu mfano dhambi ya uchawi
Ni yapi madhambi makubwa?
1-Kumshikirisha Mwenyezi Mungu
2-Kuua
3-Uchawi
4-Kuacha Swalaah
5-Kutokutoa Zakaah
6-Kuacha kufunga Swawm ya Ramadhwaan bila udhuru
7-Kutokuhiji kwa mwenye uwezo
8-Kutokuwatii wazazi
9-Kuwahama na kuwakata jamaa na ndugu; kutengana nao
10-Uzinzi (kufanya zinaa)
11-Liwati (matendo ya kaumu Luwt; watu kuingiliana nyuma) mwenye kufanya na kufanywa wote wanaingia
12-Kula ribaa
13-Kula mali ya yatima na kumdhulumu
14-Kumsingizia Allaah na Rasuli Wake uongo
15-Kukimbia vitani
16-Kiongozi kuwa mdanganyifu kwa raia wake na kutokuwa muadilifu
17-Kiburi, majivuno na kujitukuza
18-Kutoa ushuhuda wa uongo
19-Kunywa pombe
20-Kamari
21-Kumsingizia mwanamke mtwaharifu tuhuma ya uzinifu
22-Kuiba ngawira za vita
23-Wizi
24-Ujambazi
25-Kutoa kiapo cha uongo
26-Dhulma (Kudhulumu)
27-Chumo la haramu
28-Kupata utajiri kwa njia za haramu
29-Kujiua
30-Kusema uongo (kila mara)
31-Kutohukumu kwa uadilifu
32-Kutoa na kupokea rushwa
33-Mwanamke kujifananisha na mwanamme na mwanamme kujifananisha na mwanamke kimavazi, kutembea, kuzungumza na mengineyo
34-Udayuthi, ukuwadi, na kutokuwa mwaminifu katika ndoa
35-Kumuoa mwanamke aliyeachika kwa talaka tatu ili awe halali kwa mume aliyemuacha kumrudia
36-Kutojilinda kurukiwa na mikojo
37-Riyaa (kujionyesha matendo mema)
38-Kutafuta elimu kwa maslahi ya dunia, na kuificha elimu uliyonayo
39-Kufanya khiyana
40-Kutangazia na kuhesabu mema uliyoyatenda
41-Kupinga Qadar
42-Kusikiliza siri za watu
43-Kuhamisha maneno (umbea)
44-Kulaani wengine
45-Kuvunja ahadi
46-Kuwaamini makuhani, watabiri, wapiga ramli (watazamiaji)
47-Mke kutomtii mumewe
48-Kutengeneza masanamu, vinyago, na picha
49-Kupiga mayowe, kuchana nguo, kujipiga na kujikatakata wakati wa msiba
50-Kutokuwa muadilifu kwa watu
51-Kutokuwa na huruma na kuwafanyia ujeuri mke, wafanyakazi, madhaifu na wanyama
52-Kumuudhi jirani
53-Kuwaudhi na kuwatukuna Waislamu
54-Kuwaudhi na kuwafanyia ujeuri watu
55-Isbaal (mwanamme kuvaa nguo ndefu inayovuka viwiko vya miguu kwa kiburi au ufakhari)
56-Mwanaume kuvaa hariri
57-Mtumwa kumkimbia bwana wake
58-Kutokuchinja mnyama kwa ajili ya Allaah
59-Kumwita mtu kwa ubini wa baba asiyekuwa wake huku unajua (kwa makusudi
60-Kugombana na kupigana
61-Kuzuilia (watu) maji
62-Kupunja kipimo
63-Kujilinda na Aliyoyapanga Allaah
64-Kuwaudhi waja wema vipenzi vya Allaah
65-Mwanaume kuacha kuswali Swalaah ya jama’aah (Msikitini) na kuswali pekee bila udhuru
66-Kuacha kuswali Ijumaa kwa makusudi au kutotilia umuhimu na kupuuzia
67-Kubadilisha wasiyyah (aloacha mtu)
68-Kupanga njama na kufanya hila
69-Kuwapeleleza Waislamu kwa ajili ya makafiri na maadui
70-Kuwatukana Maswahaba (Radhwiya Allaahu ‘anhum)


Mwanadamu anaweza kusamehewa madhambi yote yanayohusiana na kumuasi Mola wake pindi akiamua kuacha hizo dhambi na kuendelea kufanya mema. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):


قُلْ يَا عِبَادِيَ الَّذِينَ أَسْرَفُوا عَلَىٰ أَنفُسِهِمْ لَا تَقْنَطُوا مِن رَّحْمَةِ اللَّـهِ ۚ إِنَّ اللَّـهَ يَغْفِرُ الذُّنُوبَ جَمِيعًا ۚ إِنَّهُ هُوَ الْغَفُورُ الرَّحِيمُ﴿٥٣﴾
Sema: Enyi waja Wangu ambao wamepindukia mipaka juu ya nafsi zao: “Msikate tamaa na rahmah ya Allaah; hakika Allaah Anaghufuria dhambi zote; hakika Yeye Ndiye Mwenye kughufuria, Mwenye kurehemu.” [Az-Zumar: 53]


Aayah hiyo tukufu ni mwito kutoka kwa Muumba wa mbingu na ardhi kwa wote wenye kumuasi Rabb wao, na wale waliozama na kufurutu mpaka katika maasi hata wakakata tamaa kuwa hawatoweza tena kusamehewa kwamba wasikate tamaa bali warudi haraka kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Naye yuko tayari kuwapokea kuwaghufuria na kuwasamehe madhambi yao hata yawe makubwa vipi.

Lakini kuna mashari ya kutubia kama yafuatayo:

1-Ayaache maasi hayo.

2-Ajute kwa kuyafanya maasi hayo.

3-Atie nia ya kutoyarudia tena.

Na endapo kosa hilo litahusiana na haki ya mtu hapo litaongezeka sharti la nne nalo:

4-Ni kumuomba msamaha uliyemkosea kwa ulichomkosea ikiwa ni kuhusu haki za binaadamu.

ETUGRUL BEY Nurain reymage Kazakh destroyer
 
Kwetu sisi wanasema dhambi zote ni sawa! Hakuna dhambi kubwa wala ndogo,dhambi ni dhambi tu! Aliyeua na aliyesema uongo wote adhabu yao ni kwenye shimo liwakalo moto!! Halafu mtoa mada nikuhakikishie tu,huwezi kuishi bila kutenda dhambi! Ni ngumu mnoo as long as upo humu duniani! Omba tu neema ya Mungu!
 
Mwanadamu anaweza kusamehewa madhambi yote yanayohusiana na kumuasi Mola wake pindi akiamua kuacha hizo dhambi na kuendelea kufanya mema.
Asante sana mkuu kwa mimi nilivyoelewa katika hizo dhambi kubwa 70 mbele za Allah, sijaona ikionyesha km kuvuta Moshi ni dhambi yaan dhambi ya kuvuta Moshi wa Ubani au Udi au Moshi wa Sigara hio dhambi sijaiona mkuu, kwa hio ni kwamba kuvuta Moshi sio dhambi au?!
 
Asante sana mkuu kwa mimi nilivyoelewa katika hizo dhambi kubwa 70 mbele za Allah, sijaona ikionyesha km kuvuta Moshi ni dhambi yaan dhambi ya kuvuta Moshi wa Ubani au Udi au Moshi wa Sigara hio dhambi sijaiona mkuu, kwa hio ni kwamba kuvuta Moshi sio dhambi au?!
Kuvuta sigara sio dhambi ila ni makhuruh yaan ni karaha unawakaraisha wengine na zaidi ni hatari kwa afya yako... Udi na Ubani havina shida yoyote pia sijawahi kusikia Mtu anavuta Udi/Ubani
 
Kwetu sisi wanasema dhambi zote ni sawa! Hakuna dhambi kubwa wala ndogo,dhambi ni dhambi tu! Aliyeua na aliyesema uongo wote adhabu yao ni kwenye shimo liwakalo moto!! Halafu mtoa mada nikuhakikishie tu,huwezi kuishi bila kutenda dhambi! Ni ngumu mnoo as long as upo humu duniani! Omba tu neema ya Mungu!

Muuaji anakua sawa na msema uongo!
Mchawi anakua sawa na msengenyaji!

Huwezi kuishi bila dhambi lakini zingine zinaepukika na zingine zinatofautiana kwa ukubwa wake
 
Kwetu sisi wanasema dhambi zote ni sawa! Hakuna dhambi kubwa wala ndogo,dhambi ni dhambi tu! Aliyeua na aliyesema uongo wote adhabu yao ni kwenye shimo liwakalo moto!! Halafu mtoa mada nikuhakikishie tu,huwezi kuishi bila kutenda dhambi! Ni ngumu mnoo as long as upo humu duniani! Omba tu neema ya Mungu!
Na ndio maana mwishoni nikaeka mlango wa toba nikiamini ni ngumu kuishi bila kutenda dhambi
Mungu anasema ategemewe yeye tu, je unadhani anapenda wewe ujitegemeze kwa wanadamu ikiwa yeye anajitosheleza kwa kila kila jambo ? Je kutegemea ndumba kukulinda ni sawa badala ya kutemgea Mungu? Shirki ni dhambi kubwa mno, dhambi haziwezi kua sawa
 
Na ndio maana mwishoni nikaeka mlango wa toba nikiamini ni ngumu kuishi bila kutenda dhambi
Mungu anasema ategemewe yeye tu, je unadhani anapenda wewe ujitegemeze kwa wanadamu ikiwa yeye anajitosheleza kwa kila kila jambo ? Je kutegemea ndumba kukulinda ni sawa badala ya kutemgea Mungu? Shirki ni dhambi kubwa mno, dhambi haziwezi kua sawa
Kwetu sisi dhambi zote ni sawa! Na adhabu ni ile ile
 
Mbona mimi silion hili jukwaa..nimekuwa nikilitafuta bila mafanikio
Ni kwa nini ktk huky zetu za kiakili hua tunasema huyu hajapewa adhabu i ayostahiki? Mfano mtu kalawiti mtoto wa mwaka kisha kapigwa miaka 30 jela, akili zetu tu zinakataa adhabu yake kua ndi ndogo sawa na unyama aliomfanyia mtoto, swali kwa nini akili zinakataa?
 
Back
Top Bottom