Ni yupi kati ya hawa wahusika wakiingia kwenye ndoa hutulia?

Aliyefanya uhuni sana katika ujana wake halafu akaingia katika ndoa, na yule ambaye hakufanya uhuni katika ujana wake akaingia kwenye ndoa. Ni yupi akiingia katika ndoa utulia? na ni kwanini utulia?

Mwanaume mwenye kutulia kwenye ndoa ni yule mwenye hofu ya Mungu, asie na pesa nyingi na mwenye upungufu wa nguvu za shetani aka nguvu za kiume.

Mwanamke wa kutulia kwenye ndoa ni yule mwenye hofu ya Mungu na mume mwenye pesa.

Kwa kila jinsi kutulia kwenye ndoa lazima mambo mawili yaambatane au kuwa na uwiano wa moja kwa moja.
 
Hakika mkuu maana kuna jamaa alisema funguo iliyofungua makufuli mengi huonekana yenye maana kuliko kufuli linalofunguliwa na Kila funguo, maana ukiliweka mlangoni halitafaaa kabisa!
ha ha ha ha ina maana kufuli lililofunguliwa na funguo nyingi...kwa usalama wa hicho chumba utakuwa ni mdogo?
 
Mimi nimeshaoa.
Nilichoangalia mke wangu akili ipo na huwa anafanya rational judgments ana sifa zangu nazotaka(kila mtu anajua anachotaka)
Sawa mkuu,sasa kuhusu mada unashauri ni wa aina gani utulia kwenye ndoa?
 
Mkuu,utajuaje sasa uliyenaye ana hofu ya mungu..wengi huwa wanaigiza tu
 
ha ha ha ha ina maana kufuli lililofunguliwa na funguo nyingi...kwa usalama wa hicho chumba utakuwa ni mdogo?
Yani mkuu hilo kufuli litakufanya ulizwe Kila Mara, maana mtu akitaka kuingia ndani chap tu anazama kiulani kabisa mkuu!!
 
Hakuna formula yeyote, kuna wanawake walikuwa wazururaji haswaa, lakini wametulia kwenye, ndoa, pia kuna wanaume ni wazinzi kuanzia ujana mpaka uzeeni ni kuzalisha na kulea wanakimbia
 
Hakuna formula yeyote, kuna wanawake walikuwa wazururaji haswaa, lakini wametulia kwenye, ndoa, pia kuna wanaume ni wazinzi kuanzia ujana mpaka uzeeni ni kuzalisha na kulea wanakimbia
Kwa hiyo mkuu unashauri tutumie njia gani kupata mtu sahihi?
 
Hakuna unafuu ni tabia ni tabia labda mtu aamue kuiacha, hujawahi ona Baba kazaa hovyo hovyo mpaka anafika uzeeni hajawahi kuwalea watoto, ukisikia wababa wanalalamika hawatunzwi na watoto wao, uliza kwanini? Walikula ujana wao wakapitiliza sasa malipo uzeeni
 
Kweli mkuu wapo wanaume ambao huyumba lakini asilimia kubwa akiwa amekula ujana akamaliza akioa mke ambaye anajielewa na Hana Mambo mengi hujikuta wakitulia maana anaona hakuna mpya...

Kimbembe huja kwa ambao wanaonja asali wakiwa kwenye ndoa Sasa anaanza kushangaa kua Ni tamu anaanza kugeuka chovya-chovya
 
Mwanamke mhuni hawezi kutulia ila mwanahme mhuni anaweza.


Mwanamke mhuni ataficha tabia zake kwa muda mfupi sana halafu atarudia zama zake. Wanaume tukiamua jambo tunaamua moja kwa moja

Sikushauri uoe mwanamke mhuni kwa kudhani kuwa atabadilika... utaumia sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…