Ni yupi mchezaji bora kuwahi kutokea Tanzania?

Ni yupi mchezaji bora kuwahi kutokea Tanzania?

Nimekaa na wazee hapa, wanabishana kuwa Sunday Manara "Computer" ndiye mchezaji bora kabisa kuwahi kutokea nchini Tanzania.

Ila miongoni mwao wapo wanaosema hakuna kama Edibily Jonas Lunyamila. Wakakosoa Lunyamila amecheza timu gani Ulaya? Mashabiki wa Lunyamila kimyaaa...

Mimi nimekaa zangu kimya, maana jina linalonijia kichwani ni Mbwana Samatta. Kwangu nafikiri ndio mchezaji bora wa muda wote kutoka Tanzania.

Haya wanajukwaa, tujadiliane hapa nani ni mchezaji bora kuwahi kutokea hapa Tanzania?

Karibuni kwa mjadala...
Mbwana Samata. Simpo.
 
Lunyamila hana mpinzani hapa. Kucheeza ulaya sio kigezo pekee cha mtu kuwa bora. Wapo wachezaji wengi wazuri lakin hawakupata hiyo fursa ya kucheza ulaya kwa sababu mbalimbali mf lunyamila, mohamed Hussen, athuman machupa na wengine wengi. So leo hii ninja aingie kwenye all times best player kwa kuwa yuko US anacheza na Ibra?
Kuna rasta mmoja kitaani anaupiga sana. Hajacheza ulaya, ni ni bora?
 
Athuman Machupa alicheza Denmark akashindwa akarejea baadae akaenda Uarabuni sijui yaliyotokea
Lunyamila hana mpinzani hapa. Kucheeza ulaya sio kigezo pekee cha mtu kuwa bora. Wapo wachezaji wengi wazuri lakin hawakupata hiyo fursa ya kucheza ulaya kwa sababu mbalimbali mf lunyamila, mohamed Hussen, athuman machupa na wengine wengi. So leo hii ninja aingie kwenye all times best player kwa kuwa yuko US anacheza na Ibra?
 
Takwimu zinaonyesha Mrisho Ngasa kacheza mechi 100 na taifa stars kafunga magoli 25
Wengine sijui
Samatta ana kipaji, ana uwezo kutembea na kijiji bila shida,
Msuva ana kipaji, ana speed, mshapu, mbio ndio silaha yake kubwa.
Hakuna bora wa muda wote kati ya hawa wawili labda hao Akina Lunyamila na Manara.
 
Kiuno spidi Kama msuvaaa... Kwako napooona. Kiuno laini tena jojoooojoo aaaaaa gogaga fanya Kama unataga..
Tuzivunje chaga ongeza mazagazaga.

Suvan ni noma saana.
 
Kipindi hicho "computer" zilitamalaki kweli hapa bongo !? Na hilo jina alipewa kipindi kile cha ujima !?
 
Kama ulibahatika kumuona GiGGS katika ubora wake basi umemuona Lunyamila, Sitosahau Lunyamila alipo wafunga Kagera Sugar goli sita kutoka mguuni mwake pale shamba la bibi katika ushindiwa 8-0 walioupata Yanga.
Hizi zilikua hasira za Lunyamila baada ya kutoitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa kilichokua chini ya Marehemu kocha Zacharia Kinanda ambaye pia alikua akiifunndisha Kagera Sugar kwa wakati huo.
Kinanda alidai Lunyamila alikua mchezaji wa kawaida kama wengine ambao hakuwajumuisha katika timu ya taifa aliyo ichagua.
 
Kumbe Lunyamila alikuwa baharia kiasi hicho
 
Bora ni Mbwana Ally Samata alichukua uchezaji bora wa wachezaji wanaocheza ndani ya Africa hakuna kiumbe kutoka Tanzania atafanya hivyo karibuni labda mwaka 3000 na kuendelea ,penye ukweli tuseme kuzunguka zunguka sio kabisa
 
Back
Top Bottom