Ni zipi faida za kutoa mahari?

Ni zipi faida za kutoa mahari?

Kuna kijana wiki iliyopita kafiwa na mkewe wakati wakujifungua mtoto katoka salama ila mama kafariki.
Kimbembe kimeanzia hapo kijana kanyag'anywa maiti ya mke wake Lisa hana uhalali wa kumzika Lisa hajatoa mahali walikuwa wanaishi kiholela
 
Kuna kijana wiki iliyopita kafiwa na mkewe wakati wakujifungua mtoto katoka salama ila mama kafariki.
Kimbembe kimeanzia hapo kijana kanyag'anywa maiti ya mke wake Lisa hana uhalali wa kumzika Lisa hajatoa mahali walikuwa wanaishi kiholela
Kwani akizika yeye kunakitu chochote ananufaika labda?
 
Mahari ni heshima
Ni kutengeneza kutambulika na kujipendekeza kwa muoaji.

Ila ni ujinga kutoa mahari zaidi ya laki 5 kwa miaka hii hasa kwa kijana muoaji ambae hana hata nyumba yake mwenyewe ya kuishi
Mmmh,hiyo hera kwa wazazi wa sasa hivi ukiwapa wanakutupia nayo usini kwa kweli, bila millioni kadhaaa, sidhani
 
Mwanamke ni bidhaa iliyo dukani ndio maana unatoa pesa ili uipate, zamani ukiishi na mwanamke bila kuoa/kutoa mahari wazazi wake wanasema umemuiba mtoto wao, hiyo ikimaanisha kwamba umekuta bidhaa dukani na umeichukua bila kupewa (wizi)
 
Habari za jioni wapendwa katika bwana.

Jamii nyingi za Kiafrika wanao utaratibu wa mwanaume kutoa mahari ili aweze kumuoa binti.

Baadhi ya watu husema mahari ni kama shukurani kwa wazazi wa mke, je hawa wazazi wamume ambao wamezaa kichwa cha familia mbona hawapewi shukurani?

Naomba kuelimishwa mahari ninayotoa inamsaada gani kwangu, Mkewangu na watoto.

Kulingana na ugumu wa maisha haswa bara la Africa kuna haja ya kuendelea na huu utaratibu?

 
Mabadilishano ya jina. akiolewa atatumia jina la mumewe kwa kila kitu anzia mtoto etc
 
Back
Top Bottom