Ni zipi njia za kudumu za kuondokana na tatizo la mbu?

mzeemzima

Senior Member
Joined
Apr 14, 2010
Posts
123
Reaction score
78
Wasalaam,

Moja kati ya changamoto ambayo imekuwa ikinisumbua sana ni changamoto ya mbu nyumbani kwangu, ingawa kwa sehemu kubwa hili ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Dar.

Nimekuwa nikijaribu kutafiti njia mbalimbali za kuondokana na mbu lakini mpaka sasa sijapata ufumbuzi wa kudumu.

Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa njia hizo, anisaidie na naamini wengi pia bila shaka watasaidika na njia ambazo tunaweza kuondoka na tatizo la mbu majumbani kwetu.

Natangulia shukrani zangu za dhati.
 
Mbu tunaweza kuwamaliza, ila tatizo kuna Viwanda vingi vinavyotengeneza dawa za Malaria vinavyofaidika na Mbu vitahujumu zoezi la kumaliza au kuwapunguza Mbu Nchi nzima

Tatizo lingine ni Serikali yetu,wakati wa Serikali ya Mkoloni Mbu walipunguzwa kabisa ilikuwa mpaka Mabasi ya abiria yalikuwa yakipuliziwa dawa za kuua Mbu.

Nadhani tatizo lingine ni Low IQ zetu.
 
Wasalaam,

Moja kati ya changamoto ambayo imekuwa ikinisumbua sana ni changamoto ya mbu nyumbani kwangu, ingawa kwa sehemu kubwa hili ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Dar. nimekuwa nikijaribu kutafiti njia mbalimbali za kuondokana na mbu lakini mpaka sasa sijapata ufumbuzi wa kudumu. Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa njia hizo, anisaidie , na naamini wengi pia bila shaka watasaidika na njia ambazo tunaweza kuondoka na tatizo la mbu majumbani kwetu,

Natangulia shukrani zangu za dhati.

Weka mazingira safi nje ya nyumba yako, funga madirisha ya nyavu za kuzuia umbu na pulizia dawa kwenye mitu inayozunguka nyumbani kwako kila baada ya miezi sita...( Mabwana shamba wanaijua) malaria utaisikilizia tu na utalala fofofo bila chandarua...
 
Nilidhani pale jangwani kulikuwa na mradi wa kuangamiza mbu na mazalia yake kumbe ndiyo chanzo cha kuzalisha mbu wababe kwa malaria.

Na kuhusu kibaha na kile kiwanda chao cha viuatirifu..
 
Mbu wa siku hizi hawana madhara walishapunguzwa makali
 
DDT tu, lakini ni Mission Impossible kwani wamejaa kila sehemu.
 
Pole sana, ngoja waje kukupa muongozo...
 
Wasalaam,

Moja kati ya changamoto ambayo imekuwa ikinisumbua sana ni changamoto ya mbu nyumbani kwangu, ingawa kwa sehemu kubwa hili ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Dar.

Nimekuwa nikijaribu kutafiti njia mbalimbali za kuondokana na mbu lakini mpaka sasa sijapata ufumbuzi wa kudumu.

Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa njia hizo, anisaidie na naamini wengi pia bila shaka watasaidika na njia ambazo tunaweza kuondoka na tatizo la mbu majumbani kwetu.

Natangulia shukrani zangu za dhati.
Hili suala la Mmbu Miaka ya 80s na 90s lilipata Suluhisho kwa Kupuliziwa Dawa Mitaani Dawa ya DDT (Kama Sijakosea), Shida kubwa ikaja ni ujuaji wa Wasomi wetu uchwara ambao walishauri upulizaji wa Dawa hiyo usitishwe sababu ya madhara kwa wananchi wakati huo, cha ajabu hawakuja na nini mmbadala wa walichokikataza! Matokeo yake hadi leo bado tunahangaika na Mbu! Nchi nyingi walifanikiwa kutokomeza mmbu walitumia dawa hiyo. Yaani saivi ilitakiwa hata NZi wawe Maabara tu kwa ajili ya ufundishaji na sio kuwa Sehemu ya Maisha yetu.
 
Mbu wakiisha dawa za malaria hazitouzika na sumu za kuua mbu kina rungu na wenzie hazitouzika
 
Paka rangi ndani ilichanganywa na dawa ya mbu ipo siku hizi hapo mbu utakua umewapunguza sana namanisha rangi ya ukutani
 
Ngao ya kidonge ilipotoka nilipuliza ndani kwangu, sikuona mbu, inzi, mende wala sisimizi kwa takribani miezi 6! Mda si mrefu wakaiondoa sokoni.
 
Wasalaam,

Moja kati ya changamoto ambayo imekuwa ikinisumbua sana ni changamoto ya mbu nyumbani kwangu, ingawa kwa sehemu kubwa hili ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Dar.

Nimekuwa nikijaribu kutafiti njia mbalimbali za kuondokana na mbu lakini mpaka sasa sijapata ufumbuzi wa kudumu.

Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa njia hizo, anisaidie na naamini wengi pia bila shaka watasaidika na njia ambazo tunaweza kuondoka na tatizo la mbu majumbani kwetu.

Natangulia shukrani zangu za dhati.
Yani ni shida. Huwezi hata kukaa nje ya kuanzia jioni. Goba kuna mbu balaa.
 
Wasalaam,

Moja kati ya changamoto ambayo imekuwa ikinisumbua sana ni changamoto ya mbu nyumbani kwangu, ingawa kwa sehemu kubwa hili ni tatizo la maeneo mengi ya hapa Dar.

Nimekuwa nikijaribu kutafiti njia mbalimbali za kuondokana na mbu lakini mpaka sasa sijapata ufumbuzi wa kudumu.

Naomba kwa yeyote mwenye ujuzi wa njia hizo, anisaidie na naamini wengi pia bila shaka watasaidika na njia ambazo tunaweza kuondoka na tatizo la mbu majumbani kwetu.

Natangulia shukrani zangu za dhati.
CCM wamesema tuwaache mbu wale kwa urefu wa kamba zao.
 
Nadhani huwezi wazuia mbua nje ila ndani kwako unaweza fanya baadhi ya mbinu kuwapunguza

1. Weka nyavu ply mbili unapotengenza madirisha.. kuna mbu wanaweza kupenya kirahisi kwenye nyavu ubanzi mmoja kwenye vile vitundu..nyavu mbili inafanya nafasi ya matobo iwe ndogo

2. Usifungue madirisha na milango na kuacha wazi mida ya jioni incase labda wengi wanafanya hivyo kwa ajili ya joto..incase ni joto sana unaweza weka nyavu kwenye grill la mlango kisha gril likafungwa huku mbu hawaingii.

3. Fanya fumigation ya maeneno yanayokuzunguka.. proon miti kuondoa mazalia ...fukia mashimo yenye maji..

4. Tumia neti vyumbani

5. Punguza mlundikano wa vitu kwenye compound na ndani.. magari mabovu mafriji mabovu sio tu ni mazalio ya mbu bali hata wadudu wengine hatari kama nyoka na nge.
 
Back
Top Bottom