Jamal Akbar
JF-Expert Member
- Oct 9, 2014
- 413
- 471
Kitabu cha Biblia, kinatanabaisha kuwa msingi mkubwa wa kutenda dhambi ni tamaa. Biblia inawataja binadamu wa kwanza Adam na Hawa kuwa kilichowafanya kutenda dhambi ya uasi kwenye bustani ya Eden ni tamaa ya kutaka kuwa sawa na Mungu.
Licha ya Mungu aliyewaumba kuwapa kila kitu, lakini aliwapa sharti la kutokula matunda ya mti wa katikati, lakini kutokana na tamaa na kushindwa kutii mamlaka, walidanganywa na kula tunda hilo walilokatazwa wakiamini maneno ya mwovu shetani aliyewaambia kuwa pindi mtakapokula tunda la mti huu, mtakuwa sawa na Mungu. Matokeo yake walitupwa nje ya bustani na kuishi maisha ya jasho na uchungu.
Ni ukweli usiopingika kuwa tabia za baadhi ya wanasiasa nchini wana tamaa ya kutaka mambo kwa haraka na baadhi yao hawaridhiki. Ndiyo wanasiasa wenye hulka mithili ya Tundu Lissu, mbunge wa zamani wa Singida Mashariki na Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) si sahihi. Kwa hulka ya Lissu hata ukimbeba mgongoni bado atafurukuta ili tu amnyime raha mbebaji na hataacha kutoa lawama kwamba mbebeo imekaba.
Hivi ni nani anayeweza kusimama kuipinga kazi kubwa ya ujenzi wa Taifa hili anayoifanya Rais Samia Suluhu Hassan, mwenye moyo wa pekee kabisa na mapenzi makubwa kwa Tanzania? Nani huyo alijipa likizo ya kufikiri na kujipa jukumu la kufikiri kwa muktadha wa uharibifu anayeweza kuhoji dhamira njema ya maridhiano ya kisiasa iliyoasisiwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan?
Nani huyo anayeweza kuubeza mwenendo mpya na mtazamo mpya wa kisiasa ambao Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amekuwa nao tangu alipokutana kwa mara ya kwanza na Rais Samia na kukubaliana kujenga Taifa lenye maridhiano na umoja wa kitaifa?
Ni mkwamishaji tu wa maendeleo ndiye anayeweza kusimama na kubeza dhamira hiyo njema. Ndiyo maana nasema kwamba ukiona mtu yupo kinyume na watu wengine kwa jambo jema ambalo lina sura ya kuistawishi jamii, mtu huyo anatakiwa kutazamwa kwa iicho la tahadhari.
Wengi tungali na kumbukumbu ya wapi tulikuwa miaka michache iliyopita. Tunajua na hatuna haja ya kusimulia tena. Ni ukweli usiopingika na si kwa lengo la kutafuta nani mchawi, kisiasa nchi yetu ilikuwa inakwenda pabaya.
Chuki zilitamalaki, siasa zetu zilikuwa za vitisho, kukamiana na matusi. Hatuwezi kujenga Taifa linalolea mipasuko ya kisiasa.
Taifa hili lililorithi misingi ya umoja, mshikamano na udugu kutoka kwa waasisi wake linapaswa kuendelea kujengwa katika misingi, kwani ndiyo iliyotufikisha hapa tulipo. Licha ya Taifa kuwa kubwa lenye makabila na matabaka tofauti, lakini limebaki kuwa ni Taifa moja. Tanzania inapaswa kujengwa kisiasa na kiuchumi kwa kuulinda kwa nguvu zote umoja wa kitaifa ambao msingi wake ni maridhiano.
Ni ajabu kuona Lissu ambaye kwa muda mrefu alikuwa nje ya nchi akipatiwa matibabu ya kushambuliwa kwa risasi takriban 16 wakati wa utawala wa Rais John Magufuli kwa sasa kujitokeza na kubeza maridhiano. Katika maelezo yake aliyoyatoa hivi karibuni Lissu alisema walishaandika mapendekezo ya maridhiano na kuyakabidhi serikalini, lakini mpaka sasa hayajafanyiwa kazi.
"Tunachokiona sasa ni picha zetu kwenye mabango kuwa tumeridhiana, kivipi? Wapi tumeridhiana? Kuridhiana ni utekelezaji wa mapendekezo tuliyotoa na si kuwekana kwenye picha," alisema Lissu kwenye mkutano wake na wananchi wa Morogoro hivi karibuni.