Nia ya mheshimiwa Rais ni njema, turekebishe mapungufu yaliyoonekana ili DPW aanze kazi haraka hapo bandarini.

Nia ya mheshimiwa Rais ni njema, turekebishe mapungufu yaliyoonekana ili DPW aanze kazi haraka hapo bandarini.

Nchi hii ina mambo jamani, yaani kuna vita zinaendelea chini chini huko ndani ya chama Mungu amsaidie mama yetu SSH.

Nia ya uwekezaji pale bandarini ni njema kabisa, dhamira safi kabisa. Ni uwekezaji unaokwenda kukata mirija wa watoto wa mjini ambao wamekuwa wakinyonya pale kwa raha zao.

Sasa nashindwa kuelewa, kwamba wahusika walipaswa kumsaidia Mh. Rais kwenye ule mkataba/ makubaliano ni vilaza au wamefanya makusudi kusaini yale madudu ili kumchafua Mheshimiwa?? Kwamba miongoni mwao wapo watu wa ile kambi nyingine ya chama ambao wameamua kumhujumu Rais kwa makusudi kabisa??

Mama SSH usiwe mnyonge, rekebisha mapungufu machche yaliyopo kisha wawajibishe wote waliosababisha taharuki hii kwa kutokutimiza wajibu wao na kupitisha mkataba ukiwa hovyo kiasi kile. Baada ya hapo kazi iendelee, tunahitaji uwekezaji wenye tija pale bandarini. Kama DPW anaiweza hiyo kazi na watafanya kwa uaminifu na kuhakikisha wale wahuni hawaigeuzi bandari kuwa shamba la bibi, why NOT? Tuwape wapige kazi.

Usisahau kuiweka mikataba wazi, itakusaidia usichomekewe madudu na wapinzani wako wa ndani ya chama. Inaonekana mtandao wao ni mpana.
Hakuna KAZI itaanza,

Ufutwe kwanza mkataba huu BATILI na FAKE,

Tuweke Bango kubwa pale Lango la Jiji kuwa:

" MALI YA URITHI HAIUZWI Wala HAIKODISHWI". Epuka matapeli🙏🙏🙏
 
Bado tuko hatua za awali, hawajawekeza fedha yoyote pale bandarini. Tunaweza kurekebisha au hata kuuvunja kama tutakuwa tayari kusema ukweli mahakamani juu wa viongozi wetu waliopewa 'zawadi' kule Dubai.

Kuomba mazungumzo na kurekebisha ni njia nzuri zaidi.

Kwa ilipofikia haiwezekani kurekebisha kwa sababu itaonekana walisaini bila maarifa na tayari kuna ushindani na hakuna upande uliotayari kushindwa na kwa taarifa tu hawakujua kama itafikia hapa palipofikia. Huko ndani kuna mengi sana hivi nani alivujisha mkataba huu? Aliyevujisha ni kwakuwa tu hanufaiki ila upigaji wa namna hii ipo kila sehemu na ndivyo watu wanavyotajirika. Vyanzo vyote vya mapato,mapato 30% yanaenda huko sijui b.o.t ila zingine zote watu wanakula na asilimia chache wanapeleka kwenye mwamba wa msimbazi ulioanzia lusaka.
 
Back
Top Bottom