Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Tumbiliwaulaya

JF-Expert Member
Joined
Nov 22, 2020
Posts
278
Reaction score
435
Ninalia tena msiba unaanza upya pale Mnapo nikumbusha enzi za kupishana angani! Mzee Kikwete alisafiri takribani safari za nje 421 kwa wastani wa siku tatu kila safari alikaa nje ya nchi kwa jumla ya siku 1263 katika miaka kumi, miaka 3 na miezi 4 hakuwepo nchini, ukiongeza siku zake za rikizo 28x10 = siku 280 ukijumlisha na miaka 3.4 unapata mzee hakuwepo ofisini kwa miaka 4 katika kumi, mwisho watu wakamwita Vasco da Gama wa Tanzania, ukiacha yeye mawaziri na watendaji wengine walikuwa wanapishana angani kwa safari za ulaya na nyingi zilikuwa za kwenda kuomba misaada kwa wafadhiri mpaka ya kujenge vyoo vya shule, hakuna tulichokuwa tunakiweza hadi kulipa mishara ya wafanyakazi wa serikali ilikuwa kitendawili '' kasungura kadogo.''

Ni kweli serikali haikuwa na hela za kuwahudumia raia wake kwani walikuwa hawakusanyi kodi misamaha ya kodi ilitamalaki nchi ikawa ya wapiga dili, misheni town misamiati ambayo leo imetoweka! Nakumbuka na bado nakumbuka bodi za wakurugenzi zikikaa nje ya nchi kudadavua ya nchini kwetu! mikataba inayotuhusu ikifungwa nje ya nchi bila ya kuwa na masilahi kwetu hakika zilikuwa enzi za bata bin batani kwa wale wasiofaidi wakati huo Mh.

Kwa sasa acheni tulinganishe kule na huku wapi tumefanikiwa ingawa ni kwa miaka mitano kwa kumi ya wenzi wake ni wapi tumefanikiwa zaidi kama taifa? Hili liko dhahili na hata wao Ma Rais wastaafu wanakili na walishakili mara nyingi kuwa mafanikio ya mwenda zake yameenda mbali kuliko vipindi vyao vya utawala kwani kati ya mengi yaliyowashinda yeye alifanikiwa kwa muda mfupi sana kuyapa ufumbuzi na nchi kuanza kupiga hatua za kimaendeleo. Amin amin nawaambia hakika mtamkumbuka kwa mema na si kwa mabaya.

Bado nakumbuka bajeti zetu za maendeleo na matumizi za kipindi kile, na alizoacha mwenda zake! napata shida moyoni je nitarejea kule au nitasonga mbele machozi yananitoka bado nalia na huenda nikalia zaidi, ila najipa moyo kwa kuwa mama alikuwepo jikoni wakati pishi hili likitengenezwa nina hakika anaijua njia sitarejea kwenye tembele la chukuchuku kwa kuwa eti sisi ni masikini, hatuna hela ya kununua viungo,msiba wangu utadumu milele kama mama atazisikiliza nyimbo za wapiga zumari wa eti ''umasikini wetu haushindiki''
 
Tatizo ni moja Tuu, jiwe alihubiri jinsi alivyoipigania nchi hii, Ila ule upande wa shilingi alioumiza watu hausemwi, Ila wahusika walioumizwa wanausema sasa.

Alichokifanya ni nothing dhidi ya maumivu aliyowapa watu, mi mwenyewe ni mhanga, usitegemee nikamsifu jiwe Kwa lolote kabisa.

Kikwete alichukiwa Sana na watu Kwa ubadhirifu wa Fedha na ufisadi, ila Leo hii ukimuuliza mtu Kati ya Jiwe na Msoga atakuchagulia Msoga chap.
 
Jiwe alikuwa mwizi kama wezi wengine tu. Bora hata ya hao wezi wengine walijiweka wazi kuwa wapigaji. Bw. Jiwe alijitwika umalaika mtu, mtiifu kupita kikomo kumbe nyuma ya pazia anatuchapa tu.
Kwa kifupi alikuwa kibaka mbabe. Anakuibia na mikwara juu.
 
Tatizo ni moja Tuu, Jiwe alihubiri jinsi alivyoipigania nchi hii, Ila ule upande wa shilingi alioumiza watu hausemwi , Ila wahusika walioumizwa wanausema sasa... Alichokifanya ni nothing dhidi ya maumivu aliyowapa watu , mi mwenyewe ni mhanga , usitegemee nikamsifu jiwe Kwa lolote kabisa .... Kikwete alichukiwa Sana na watu Kwa ubadhirifu wa Fedha na ufisadi , Ila Leo hii ukimuuliza mtu Kati ya Jiwe na Msoga atakuchagulia Msoga chap .....
Ni kweli wapo watu walio umizwa unadhani kwa nini hata yeye binafsi aliwahi kutamka ''Mtanikumbuka kwa mema na si kwamabaya'' alijua wazi katika kufyeka njia iliyo kuwa poli lazima viumbe wengine wataumia. Kwa jinsi nchi ilipokuwa imefikia ilihitaji shujaa kufanikiwa na ndio maana marais wastaafu wanakiri kushindwa kuirejeshe nchi kwenye mstari wa kuanza kupiga hatua.
 
Kinachotakiwa ni ku-balance mambo yote. Sio kuacha hiki na kufanya kile tu.
Mfano: Ni kweli sio vyema kwa kiongozi kupenda anasa na kimiliki vitu vingi vya thamani kupitia uongozi, lakini haikuwa sifa ya maana kwa marehemu Sokoine kusifiwa kumiliki suruali sijui mbili tu.
 
Tumeibiwa ktk kivuli cha uzareendoo
Wakati wa enzi zile kila mwenye mamraka alikuwa na kisu na alikuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na kujikatia pande analopenda, wakati wa mwenda zake walio wengi hawakuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na ndio maana ya haya matokeo unayoyaona leo, sio kweli kwamba wizi uliisha kabisa bali ulipungua kwa kiasi kikubwa,kufungia uhuru wa habari kulitoa mwanya panya kujinyakulia vipande vidogovidogo bila kusikika.
 
Wajumbe wenye ID's mpya mmeingia kwa kasi sana humu jukwaani ndani ya muda mfupi kumtetea magufuli!

Nilitamani sana kumfahamu kiongozi wenu anaye simamia hili zoezi la kumsafisha mtukufu wenu! kutokana tu na madudu yake lukuki aliyo yafanya tangu alipoingia madarakani mwaka 2015!
 
wakati wa enzi zile kila mwenye mamraka alikuwa na kisu na alikuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na kujikatia pande analopenda, wakati wa mwenda zake walio wengi hawakuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na ndio maana ya haya matokeo unayoyaona leo, sio kweli kwamba wizi uliisha kabisa bali ulipungua kwa kiasi kikubwa,kufungia uhuru wa habari kulitoa mwanya panya kujinyakulia vipande vidogovidogo bila kusikika.
Jiwe amejitajirisha sana kwa ufisadi huu
 
wakati wa enzi zile kila mwenye mamraka alikuwa na kisu na alikuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na kujikatia pande analopenda, wakati wa mwenda zake walio wengi hawakuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na ndio maana ya haya matokeo unayoyaona leo, sio kweli kwamba wizi uliisha kabisa bali ulipungua kwa kiasi kikubwa,kufungia uhuru wa habari kulitoa mwanya panya kujinyakulia vipande vidogovidogo bila kusikika.
Hakuna mema aliyo Fanya zaidi ya kutekeleza miradi yoote iliyo anzishwa na mh kikwete
 
Wajumbe wenye ID's mpya mmeingia kwa kasi sana humu jukwaani ndani ya muda mfupi kumtetea magufuli!

Nilitamani sana kumfahamu kiongozi wenu anaye simamia hili zoezi la kumsafisha mtukufu wenu! kutokana tu na madudu yake lukuki aliyo yafanya tangu alipoingia madarakani mwaka 2015!
Kila binaadam ana mapungufu yake,lakini pia ni binaadam wa hatari sana asiyeweza kuthamini mema ya wengine kwa kisingizio cha ubaya ''yatupasa kushukuru kwa yote ndipo tunapoweza kupata kibari machoni pa bwana''
 
Kila binaadam ana mapungufu yake,lakini pia ni binaadam wa hatari sana asiyeweza kuthamini mema ya wengine kwa kisingizio cha ubaya ''yatupasa kushukuru kwa yote ndipo tunapoweza kupata kibari machoni pa bwana''
Natamani sana kumfahamu huyo mfqdhili wenu anaye isimamia hii show mwanzo mwisho!

Maana nyuzi za kumfagilia marehemu na kumponda JK, zimetamalaki sana humu jukwaani kutoka kwa members wapya kabisa!
 
Mtu anapiga 1.5 trilioni kimya kimya haijulikani ziko wapi

Kampuni yake unapata tenda za ujenzi kila Kona ya nchi.

Bado Kuna midege iliyonunuliwa mkataba wa manunuzi haijulikani ulipo hatujui alitupiga kiasi gani Cha juu.

Bado mishe mishe nyingi kazipiga na hakuna alieyeweza kumuhoji ukihoji unaishia jela au mochwari.


Hapo hapo !!

Watoto wa maskini waliomaliza vyuo kwa maelfu wanalalamika ajira hawaoni Wala hasikii.

Anakwapua hela za wastaafu kwa kigezo Cha vyeti feki Kama si uonevu Ni Nini?

Hakuna ongezeko la mishahara miaka 5 Wala madaraja

Pesa anatafuna yeye na cycle yake .

Kumuona Huyo mtu shujaa Ni uchizi,uwendawazimu na uduanzi labda Kama ulikuwa mnufaika na ufisadi wake

Hapo sijaongelea kubana Uhuru wa kujieleza na habari,mauaji ya wakosoaji wake ,kesi za kubumba,na mengine kedekede.

Binafsi nitaaahadithia wanangu tuliwahi kuwa na rais wa ovyo aitwa Magufuli
 
Back
Top Bottom