Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Niacheni nilie maana bado sijasahau yaliyonipata jana yasije kunikuta tena

Jiwe alikuwa mwizi kama wezi wengine tu. Bora hata ya hao wezi wengine walijiweka wazi kuwa wapigaji. Bw. Jiwe alijitwika umalaika mtu, mtiifu kupita kikomo kumbe nyuma ya pazia anatuchapa tu.
MWAMBIENI CAG, SISI TUMERIDHIKA!!

1. Mwambieni CAG kwamba sisi wenyewe tumeridhika, tumezoea kuibiwa. Mwambieni tofauti ya wizi wa zamani na huu ni kwamba wizi wa sasa unafaida kwa Wananchi wala asiumize kichwa. Mwambieni sisi Wananchi hatuna tatizo na hasara au wizi uliofanyika wakati wa JPM. Sisi tumeridhika hivyohivyo kwa sababu tuna macho ya kuona!!

2. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa kupitia EPA. Pesa bilioni 135 zikaliwa na watu wachache, wakati huo elimu bure ilikua bado kuja. Mikopo ya elimu ya juu ilikua ni songombingo kwa hiyo hatuoni hatari kuibiwa sasa huku elimu bure ikiwa imeanzishwa na mikopo ikitoka kwa wakati. Sisi tumeridhika kabisa na hasara au wizi wa JPM!!

3. Mwambieni CAG kwamba tuliibiwa hapa bilioni 300 Serikali ikilipa Makampuni hewa katika kashfa ya MEREMETA. Mwambieni hapakua na tatizo lolote na wakati huo bajeti ya Dawa ilikua chini ya bilioni 30 lakini sasa na wizi wa JPM umepandisha bajeti ya DAWA zaidi ya mara tisa; yaani bilioni 270. Mwambieni kwa wizi huu Mungu atupe nini? Tumeridhika sana na wizi wa JPM.

4. Mwambieni CAG kwamba tulishaibiwa sisi kwenye mauzauza ya uwekezaji wa Bulyanhulu na Buzwagi na hata leo hakuna maelezo ya yanayoeleweka. Kodi hazikulipwa na pesa zikapigwa na wajanja wachache. Wakati huo wote madini na migodi yote ilikua ni mali ya wawekezaji wasiolipa kodi, Wananchi ilikua ni marufuku kukaribia migodi katika nchi yao. Kama JPM ameiba halafu wananchi wanachimba madini wenyewe kwa uhuru, ninaumia kwamba atakua ameiba kidogo sana. Wizi wenye manufaa kwa umma una maana zaidi kuliko wizi usio na manufaa. Sisi tumezoea kuibiwa, lakini kwa huu wa JPM tumeridhika.

5. Mwambieni CAG kwamba sisi tumezoea kuibiwa. Tumeshaibiwa haswa, ilikuja hapa tukaibiwa katika Mkataba wa kijinga wa DOWANS. Nchi ikalipa bilioni 111 kwa sababu ya maslahi ya watu wachache. Wakati tunaibiwa kupitia DOWANS, Mv. Victoria ilikua inalaza watu siku mbili ziwani kwa ubovu wake. Maisha yao yalikua hatarini kila safari, leo JPM akiiba au akitutia hasara ya bilioni 60 huku Mv. Victoria ikiwa MPYA kuna tatizo gani? Meli mpya tele kuanzia ziwa Nyasa, Tanganyika na Bahari ya Hindi Kilwa. Tunapenda wizi wa namna hii, angeiba kabisa za kutosha akajenga nyumba nzuri kama wenzake, akamiliki magari za mizigo meupe kukuki na sheli za kumwaga. Au akamilika supermakert za Da'slam kama wenzake. Sisi kuibiwa tumezoea, wizi wa JPM una manufaa, tumeridhika.

6. Mwambieni CAG kuwa sisi tumezoea kuibiwa asijiumize bure na ma-press ya kutangaza vi-wizi vya kitoto hivyo. Tulipigwa hapa pesa TAKATIFU katika Mkataba maarufu wa RICHMOND ulioondoka na Serikali ya mwaka 2008 hadi sasa hakuna kilichofanyika. Wakati tukipigwa pesa za Richmond daraja la Mfugale lilikua halipo, Daraja la Ubungo (Kijazi Interchange) haikuwahi kufikiriwa, Daraja la Tanzanite (Salender) lilikua katika ndoto, lile la Busisi halikufikiriwa kabisa. Kama tumeibiwa leo na mambo yote haya yamefanyika mwambieni CAG sisi roho kwatu, tumeridhika riport zake tupa kule hatusikii la mwazini wala mnadi swala. Tumefunga masikio!!

7. Mwambieni CAG sio hata siku nyingi zilichotwa BOT bilioni 306 kwa kilichoitwa kashfa ya TEGETA ESCROW. Nchi ikaibiwa tena na wajanja wachache, wakabeba pesa kwenye masandarusi. Wakati tukiibiana bilioni 306 za Escrow umeme vijijini ulikua unaunganishwa kwa Tsh. 454,000 ila kwa wizi wa JPM umeme vijijini unaunganishwa kwa Tsh. 27,000; asilimia zaidi ya 70 umeme umefika vijijini. Wizi mzuri kiasi gani huu!? Sasa tunajenga megawati 2400 kutoka Bwawa la Nyerere ili umeme ushuke zaidi. Ingalikua uwezo ni wangu ningalimrudisha mtu huyu aendelee kuiba na kutia hasara zaidi kwa sababu wizi na hasara zake zina manufaa kwa watu. Mwambieni CAG sisi tumeridhika hivyohivyo, atuwache!!

8. Mwambieni CAG sisi tumewahi kuibiwa Twiga mzima akabebwa na shingo yake akaondoka zake. Hii nchi tunaibiana na Wanyama yeye anahangaika na vipesa vidogo vidogo vya matengenezo ya ATCL. Mwambieni wakati tukiibiana TWIGA upatikanaji wa maji Vijijini ulikua ni asilimia 47 na sasa kwa wizi na hasara za JPM upatikanaji wa Maji vijijini umefikia asilimia 70.1 huku mijini upatikanaji ukitoka asilimia 74 hadi 84. Ni mtu mjinga pekee anaweza kuchukizwa na wizi wa JPM, mwambieni CAG sisi tumeridhika tunatamani angekuwepo aibe tena. Hatutakagi ujinga!!

9. Mwambieni CAG kuwa tumeibiwa sana nchi hii. Wakati wote tuliibiwa huku Nchi ikiwa haina Ndege hai hata moja. Mwambieni leo tuna Ndege 11 za kwetu wenyewe. Hizo hasara za ATCL zisimuumize kichwa, hakuna biashara isiyo na hasara, JPM keshawawekea mtaji na heshima ni wajibu wao kutafuta akili za kupata faida sio kuua mtaji. Mwambieni CAG, sisi tunampenda mwizi anayeiba halafu akanunua Ndege kwa ajili ya Nchi nzima, akajenga reli ya kasi, stend kibao za kisasa, masoko kwa ajili ya biashara nk. Kwakweli sisi tumeridhika sana na wizi huu!! Mungu amlaze mahala pema JPM, ametutoa tongotongo!!

10. Mwambieni CAG asipoteze nguvu zake bure kwa sababu hata hao wezi huwa hawafanywi kitu. Mwambieni tumezoea na zaidi tumeridhika na wizi au hasara za JPM. Mwambieni CAG nchi hii imeongozwa na wezi wengi lakini huyu alikua ni mwizi wa heshima. Tunampenda, tutammiss hivyohivyo na yeyote mwenye kumchafua atachafuka kwanza yeye. Tutakua Taifa la kijimga sana kuacha ALAMA za mtu huyu zifutwe na watu wajinga, wavivu
wasio na lolote walioachiwa Nchi wasiongoze wakihangaika na umbea, udaku na ushambenga.
Kwa taarifa yenu #SISI TUMERIDHIKA HATA ANGEIBA NCHI YOTE AIUZE!! Tuna macho ya kuona, tusichoshane.
#TutakukumbukaDaimaJPM.
MenukaJr,
Da'slam-Tanzania.
 
Lakini deni la taifa kipindi chake liliongezeka maradufu,hivi alikuwa anakopakopaje huyu mwendazake.
 
Rais samia ikatokea safari itakayokuwa na manufaa nje ya nchi nenda mama yetu akili za kukaa hapa na kusigishana sometimes sizo na mwishowe kuumizana tu,nchi hujengwa na generations ya viongozi mbalimbali just imagine h
ata uingereza na marekani na ufaransa bado zinajengwa mpaka Leo hii,na bado zitaendelea kujengwa tu POINT HAPA NI JINSI GANI UTAWAPA RAIA WA TAIFA LAKO HUDUMA BORA NA MAISHA MAZURI YA RAHA STAREHE HUKU WAKIFANYA KAZI KWA BIDII LIFE IS TOO SHORT NO ONE CAN HANDLES ALL THINGS AT ONCE.
 
Sisi tunachojali ni kuwa shetani mtu kafyekelewa mbali mengine hayo ni porojo zako!
 
Sasa kama huyu mwendazake ndo alikuwa anaongoza kwa kukusanya kodi mbona ndio anaongoza kwa kukopa kuliko marais wote. Peke yake tu amekopa trillion 23. Wakati wengine wote kwa upamoja wao wanne walikopa trillion 36 tu? Huoni kuwa uliaminishwa ujinga tunatumia fedha za ndani
 
Endelea kulia tu....sindano inakuingia sawasawa. Tuulize sisi maumivu aliyotuachia mwenda zake kutuvunjia nyumba zetu kwa kejeli na ndelemo. Sindano ikikuingia vizuri lia kimyakimya. Nesi asijekudunga ya kichwani kabisa. Nyie ndo mlifaidi ya kibabe ya yule mwendazake.
 
Tatizo ni moja Tuu, jiwe alihubiri jinsi alivyoipigania nchi hii, Ila ule upande wa shilingi alioumiza watu hausemwi, Ila wahusika walioumizwa wanausema sasa.

Alichokifanya ni nothing dhidi ya maumivu aliyowapa watu, mi mwenyewe ni mhanga, usitegemee nikamsifu jiwe Kwa lolote kabisa.

Kikwete alichukiwa Sana na watu Kwa ubadhirifu wa Fedha na ufisadi, ila Leo hii ukimuuliza mtu Kati ya Jiwe na Msoga atakuchagulia Msoga chap.
Acha upuuzi, watu wanakufa hakuna dawa hospital ye yuko state anapiga picha na 50cent,umeme kila dakika unakatika biashara haziend madudu kama yote, walioumizwa na JPM wacha waumizwe mi ninachojua kaleta maendeleo
 
Labda kaleta mandeleo nyumbani kwenu koromitje
 
Sasa kama huyu mwendazake ndo alikuwa anaongoza kwa kukusanya kodi mbona ndio anaongoza kwa kukopa kuliko marais wote. Peke yake tu amekopa trillion 23. Wakati wengine wote kwa upamoja wao wanne walikopa trillion 36 tu? Huoni kuwa uliaminishwa ujinga tunatumia fedha za ndani
Tofauti ya mwendazake na wenzake ni hii, Wenzake walikopa ili wapate fedha za matumizi ya serikali, Mwenda zake alikopa kufanya miradi ya maendeleo ambayo baada ya muda itaanza kuzalisha na kujilipa, tunatarajia kuwa wauzaji wa umeme nchi za nje kuanzia mwakani, kwa sasa njia ya kv 400 inakamilika kutoka singida hadi namanga kuingia kenya,njia ya uganda ipo na nchi zingine za ECA, SGR ni mradi wa gharama kubwa lakini utaingiza hela na kuanza kujilipia deni, huu ni mfano wa kiongozi anaeona kesho, kwa kifupi walikopa wakala na huyu kakopa azalishe ni hivyo tu.
 
Jiwe alikuwa mwizi kama wezi wengine tu. Bora hata ya hao wezi wengine walijiweka wazi kuwa wapigaji. Bw. Jiwe alijitwika umalaika mtu, mtiifu kupita kikomo kumbe nyuma ya pazia anatuchapa tu.
Kwa kifupi alikuwa kibaka mbabe. Anakuibia na mikwara juu.
Uko sahihi sana
 
Tofauti ya mwendazake na wenzake ni hii, Wenzake walikopa ili wapate fedha za matumizi ya serikali, Mwenda zake alikopa kufanya miradi ya maendeleo ambayo baada ya muda itaanza kuzalisha na kujilipa, tunatarajia kuwa wauzaji wa umeme nchi za nje kuanzia mwakani, kwa sasa njia ya kv 400 inakamilika kutoka singida hadi namanga kuingia kenya,njia ya uganda ipo na nchi zingine za ECA, SGR ni mradi wa gharama kubwa lakini utaingiza hela na kuanza kujilipia deni, huu ni mfano wa kiongozi anaeona kesho, kwa kifupi walikopa wakala na huyu kakopa azalishe ni hivyo tu.
Kikwete amejenga sekondari za kata nchi nzima, amejenga barabara zote za kuunganisha mikoa nchi nzima, vituo vya afya, vyuo vikuu, magorofa ya nyumba za wanajeshi nchi nzima, mabomba ya gas nk, hiyo sio miradi ya maendeleo
 
Tofauti ya mwendazake na wenzake ni hii, Wenzake walikopa ili wapate fedha za matumizi ya serikali, Mwenda zake alikopa kufanya miradi ya maendeleo ambayo baada ya muda itaanza kuzalisha na kujilipa, tunatarajia kuwa wauzaji wa umeme nchi za nje kuanzia mwakani, kwa sasa njia ya kv 400 inakamilika kutoka singida hadi namanga kuingia kenya,njia ya uganda ipo na nchi zingine za ECA, SGR ni mradi wa gharama kubwa lakini utaingiza hela na kuanza kujilipia deni, huu ni mfano wa kiongozi anaeona kesho, kwa kifupi walikopa wakala na huyu kakopa azalishe ni hivyo tu.
Hiyo sio kweli ,yaani Kama udom , madaraja eg kigamboni , mloganzila , Barbara nyingi , etc huzioni ? Au hiyo miradi ni matumizi ya kawaida ( recurrent expenditure)
 
Hakuna jema alilofanya ambalo kama watamzania tunaweza kumkumbuka.
USISEME ''WATANZANIA'' sema wewe, mimi mtanzania nayaona mema mengi na hata wewe ipo siku utayaona toka kufuzilia mbali akina dowans na majizi wenzake waliotunyonya hadi tukabaki mbavu tupu hadi kuzalisha umeme wetu bila kata kata ya kutisha, huwezi kutoa shukurani hata kwa hilo tu.
 
Kila binaadam ana mapungufu yake,lakini pia ni binaadam wa hatari sana asiyeweza kuthamini mema ya wengine kwa kisingizio cha ubaya ''yatupasa kushukuru kwa yote ndipo tunapoweza kupata kibari machoni pa bwana''
Kama ni hivyo basi husingetoa andiko ili ( la kukandia JK)
 
Wakati wa enzi zile kila mwenye mamraka alikuwa na kisu na alikuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na kujikatia pande analopenda, wakati wa mwenda zake walio wengi hawakuwa na uwezo wa kuifikia keki ya taifa na ndio maana ya haya matokeo unayoyaona leo, sio kweli kwamba wizi uliisha kabisa bali ulipungua kwa kiasi kikubwa,kufungia uhuru wa habari kulitoa mwanya panya kujinyakulia vipande vidogovidogo bila kusikika.
hivi hayo unayoita matokeo ni yapi kwanza? barabara….JK alijenga, madaraja..Mkapa na JK walijenga pia.... Mwendo kasi...JK, Mloganzila na JKH institute...JK, UDOM ...JK, Ufusadi kote ulikuweko na kwa mwendazake ulijaa kama wote, haya ndege mmenunua cash hazina pa kwenda na nyingine zinatolewa pesa za maintanance lkn bado zimelala, Mishahara kwa wafanyakazi kwa JK annual increment ilikuweko lkn kwa Magu haijawahi tokea. kiwanja chandege..phase I and II mwanzoani ni JK, Songwe airport..JK, Kihansi HPP... JK, Kinyerezi Power plant ...JK hebu tuelezee hasaa nini kimefanyika ambacho wengine hakukufanyika mpaka mumuite so special mpk mtake kuweka sura yake penye noti?
 
Back
Top Bottom