Nianze na kipi kati ya nyumba, gari au mke?

Nianze na kipi kati ya nyumba, gari au mke?

thegreat1510

JF-Expert Member
Joined
Mar 2, 2021
Posts
1,523
Reaction score
4,040
Samahani kidogo kwa usumbufu. Naomba ushauri hapa

Nianze kujenga nyumba then nioe kisha ninunue gari

Nioe, ninunue gari kisha nijenge au

Ninunue gari, nijenge kisha nioe, au vyote.

Upi ni mlolongo mzuri?

⒨⒴ ⒡⒰⒯⒰⒭⒠.
 
Kama una circle nzuri ya fedha fanya kisicho muhimu uje kwa vya umuhimu.

Kama unabangaiza anza na mambo muhimu.

Wakati naanza maisha, nilianza na vitu ambavyo si muhimu na njia hii ilinisaidia kupambana.

Nilianza kumiliki gari kabla hata sijajenga.

Nilianza kumiliki kabati kabla sijawa hata na kitanda wala godoro.
 
Kama nina mtu sahihi ningeanza na kuoa, mengine yakafuata. Kama ni hao ma pisi kali wa mjini then ningejenga kwanza, kuwa na gari inaweza kukutanisha na wrong person katika mahusiano yako, mtu anaweza kukupenda tuu kwa sababu anapata lift kila akitaka kwenda mahali
 
dah!
 
Zamani nilikuwa napinga mtu anaenunua gari kabla ya nyumba, kwa sasa nina mtizamo tofauti.

Kama hilo gari linakusaidia kuingiza pesa zaidi nunua gari.

Kama ni kwa ajili ya starehe tu anza nyumba.

Nb.mjini kuna baba/mama mwenye nyumba tu na sio mwenye gari.
 
Mawazo yote uliyo sema ni mwendelezo wa mawazo ya kimasikini na fikra za kuendelea kua tegemezi, wewe utakua ni muajiriwa

Any way kiufupi acha vyote ulivyosema na wekeza pesa kibiashara,ktk kile unachokijua ili pesa izae na kuongezeka,kisha hayo uliyosema utakuja kuyafanya baadae kwa urahisi zaidi.

Hata kuoa usitoe kwa kisingizio cha kuchelewa kuzaa, maana tupo kwenye dunia ambayo unaweza kuoa leo kwa mbwembwe na baada ya mwaka ukaja kuweka bandiko hapa jf kua tukupe ushauri mke wako anakusumbua.
 
Kama nina mtu sahihi ningeanza na kuoa, mengine yakafuata. Kama ni hao ma pisi kali wa mjini then ningejenga kwanza, kuwa na gari inaweza kukutanisha na wrong person katika mahusiano yako, mtu anaweza kukupenda tuu kwa sababu anapata lift kila akitaka kwenda mahali
Wewe wanawake hawapendi wanaangalia maisha.
 
Dogo anza na kamjengo kwanza maana magari hata ya Uber na Bolt yapo, hilo lingine kama una uwezo wa kununua maziwa huna haja ya kufuga ng'ombe siku ukihitaji kamata pisi yako moja ya chuo kula sepa maisha yaendelee, utakuja kunishukuru ukikua
 
Back
Top Bottom