Nianze na kipi kati ya nyumba, gari au mke?

Nianze na kipi kati ya nyumba, gari au mke?

Mimi nakushauri anza na biashada. Changa karata zako vizuri piga biashara iwe inakuingizia faida. Hapo utaweza kujenga nyumba na kununua gari.

Kuhusu kuoa inategemea wewe ni mshabiki wa kambi gani. Ya Liverpool VPN au ya Jokajeusi
Hii nafikiri ndio la muhimu kuzingatia ni wazo zuri kujenga mkondo wa pesa kwanza!
 
Wekeza kwenye biashara hii itakusaidia kuongeza mzunguko wa pesa ambazo utazidunduliza kuja kuanza kujenga. Kama unaweza jenga nyumba hta ya vyumba2 uanze life. Ila km Mishe zako zinauhitaji wa gari kupata michongo zaidi!!! Ni vema ukaanza na gari uzidishe mzunguko wa pesa. Usinunue gari kwa ajili ya kuonekana kwamba una gari, hili ni kosa kubwa sana maana litakugharimu sana.
Ukishajenga tu hakikisha unaoa mke mzuri na anayekupenda pia yule mnaeendana hapa namaanisha michongo yako inakuendea vzr tu maana mke ni baraka tosha. Ila ukikosea kuoa kwa tamaa zako bunafsi utpata mikosi kama yotee na utakufa kifikra,maisha na hata kiafya.
Zingatia kama kweli unatka ushauri mzuri.
 
Mawazo yote uliyo sema ni mwendelezo wa mawazo ya kimasikini na fikra za kuendelea kua tegemezi,wewe utakua ni muajiriwa

Any way kiufupi acha vyote ulivyosema na wekeza pesa kibiashara,ktk kile unachokijua ili pesa izae na kuongezeka,kisha hayo uliyosema utakuja kuyafanya baadae kwa urahisi zaidi.

Hata kuoa usitoe kwa kisingizio cha kuchelewa kuzaa,maana tupo kwenye dunia ambayo unaweza kuoa leo kwa mbwembwe na baada ya mwaka ukaja kuweka bandiko hapa jf kua tukupe ushauri mke wako anakusumbua.
Sure! Bora tumkute kwenye jukwaa la ujenzi akiomba ushauri wa kufanya maintainance ya nyumba ake baada ya fundi kupopoa cement ake [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mathayo 6:33 Bali utafuteni kwanza ufalme wake, na haki yake; na hayo yote mtazidishiwa. Mathayo 6:34 Basi msisumbukie ya kesho; kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Yatosha kwa siku maovu yake.
Achana kutumia vibaya maandiko aisee, aibu sana kutumia hayo kwa uvivu wa kufikiria
 
Kwa nini watu wanaamini kwamba kuwa na nyumba na gari ndo maisha? Kama una mradi wa uzalishaji mali anza na mke ili mshirikiane kujenga nyumba mambo ya magari yatakuja baadae. Kama ni mwajiriwa jaribu miradi ya uzalishaji mali kwanza, afuate mke, ifuate nyumba.
Ukianza na hayo mengine ni kwamba nyumba na gari ndo vitamuoa mwanamke siyo wewe maana hivyo viwili vinatongoza bila hata wewe kutumia nguvu. Ukioa bila hivyo vitu utampata aliyekupenda wewe na fikra zako.
 
Jenga nyumba ndogo nzuri, Hili ni hitaji muhimu kwa mtu yeyote hata kama hujawa na mke lakini bado unaihitaji nyumba. Hivyo otesha mjengo mambo mengine yatajileta mbele kwa mbele.
 
Anza Kujenga Chief, Kimbiza Hadi Ufunike....then nunua gari then uendelee kumalizia mdogo mdogo....Bob ujenzi sio masihara ila usiogope pia inawezekana sana...i know what im saying, anza nyumba.
 
Jenga kwanza mengine ni rahisi kufanikisha kuliko kujenga
Hv hela ya kununulia gari unaweza jengea nyumba? Kujenga inabifi warau u-raise the likes of 40-50mil
Kununua gari ni ngumu kuliko kujenga ingawa gari zetu za kawaida bei ni ndogo kuliko nyumba.
Kama gari ni 15m inabidi uwe nayo yote ndio ununue. Lakini nyumba hata ya 50m unaweza kuanza kujenga ukiwa na 1m tu unanunua hiki na kile ila gari huwezi kununua vipande vipande.
 
Acha mbwembwe jenga kwanza.
Kama hela ya kujenga unayo jenga kwanza then vingine vitafuatia kulingana na hitaji lako,ila kama hela yako ya kuunga bora uweke mke kwanza ndani maana unaweza kuchukua hata miaka 10 nyumba haijaisha...
 
Samahani kidogo kwa usumbufu. Naomba ushauri hapa
Nianze kujenga nyumba then nioe kisha ninunue gari,
Nioe, ninunue gari kisha nijenge au
Ninunue gari, nijenge kisha nioe
au vyote.

Upi ni mlolongo mzuri?
⒨⒴ ⒡⒰⒯⒰⒭⒠.
Edit uzi wako, kila ulipoandika "nioe" futa.
 
Mkuu,unaanza na unachohitaji,kama unahitjai nyumba Jenga,kama gari nunua,kama mke oa.Vyovyote vile utakavoanza mziki wa maisha ni ule ule,kisu ni kile kile.Ila kwa mimi Huwa namwamia mtu anza na mke,kisha gari,kisha nyumba.Nyumba ya kujenga wakati huna wa kuishi naye huwa inakuwa Danguro lako na inakufanya uwe na dharau flani hivi.Gari ya kununua bila kuwa na mpenzi huwa nayo inakuwa hivo hivo mara nyingi.Ila ukianza na mke,kisha gari kisha nyuma /nyumba kisha gari unakuwa na stress free life.Ni mtazamo wangu tu.
 
Jenga kwanza chief...THEsE GIRLz[emoji54][emoji54]ThESe...

Then,nunua gari piga misele sana kabla hujaoa enjoy na gari yako kwanza...af utaangalia cha kufanya baada ya hayo
 
Kma una uwezo wa kujenga jenga kwanza ukiwa na familia unaishi kwako ni heshima, kupaki gari kwenye nyumba za wanaume wenzako hizo ni fedheha.
Kuoa n kma kcheza kamari unaweza ukaoa balaa ikakuvurugia plan zote za maisha, japo wapo wanawake ambao ukiwapata n kama umepata dhahabu utajikuta unafanikiwa zaid ya ulivyokua peke yako lakin hawa n wachache tofaut na wenye ushetani ambao n wengi zaid.
 
Samahani kidogo kwa usumbufu. Naomba ushauri hapa
Nianze kujenga nyumba then nioe kisha ninunue gari,
Nioe, ninunue gari kisha nijenge au
Ninunue gari, nijenge kisha nioe
au vyote.

Upi ni mlolongo mzuri?
⒨⒴ ⒡⒰⒯⒰⒭⒠.
Matumizi ya mwanamke kwa mwaka mzima ni sawa na thamani ya kujenga nyumba ya vyumba vitatu.
 
Back
Top Bottom