Kicheche mkali
JF-Expert Member
- Nov 3, 2021
- 290
- 266
🏠 MDau ameuliza:
“Nianze na nyumba ndogo ya kuanzia maisha, au nianze moja kwa moja na dream house yangu?”
Jibu langu kama mtaalamu wa ujenzi ni hili 👇
Kama tayari una ramani na maono ya nyumba unayotaka kuishi kwa muda mrefu, usikimbilie kujenga nyumba nyingine pembeni ya kiwanja.
Kwa nini? 🤔
Kwa sababu unaweza kutumia pesa nyingi kujenga nyumba ya muda, halafu baada ya miaka kadhaa ukalazimika kuanza tena kutumia pesa, nguvu na muda kujenga nyumba ya ndoto Yako
💡 Badala yake, anza nyumba ya ndoto Yako kwa hatua.
✅ Anza na msingi wa nyumba yote kulingana na ramani.
✅ Kisha jenga sehemu unayoweza kumudu kwa wakati huo.
✅ Unaweza kuanza na chumba kimoja au viwili, pamoja na sehemu muhimu za kuishi kulingana na mpangilio wa ramani.
✅ Fanya finishing ya kawaida kwenye sehemu hiyo na hamia.
✅ Baada ya hapo, endelea kujenga vyumba na sehemu nyingine taratibu kadiri kipato kinavyoruhusu.
🔥 Mfano rahisi:
Kama una Tsh 10M ambayo ungeitumia kujenga kajumba pembeni, jiulize:
“Je, hiyo Tsh 10M inaweza kuinua sehemu gani ya dream house yangu?”
Kama inaweza kukuwezesha kujenga chumba kimoja, sitting room, jiko au sehemu nyingine muhimu, anza hapo hapo kwenye nyumba yako ya malengo.
Hivyo kila pesa utakayowekeza itaendelea kujenga nyumba ileile utakayoimalizia.
⚠️ Lakini kuna jambo muhimu sana:
Usianze kujenga sehemu kiholela TU hakikisha Msingi, columns, beams na structural arrangement vinajengwa kwa kuzingatia nyumba nzima tangu mwanzo. Hii ndiyo sababu ramani na ushauri wa kitaalamu ni muhimu.
🏗️ KUMBUKA:
Nyumba ya leo iwe mwanzo wa nyumba yako ya kesho isiwe nyumba nyingine utakayoiacha baadae.
Wewe ungekuwa kwenye nafasi ya huyu mdau, ungejenga nyumba ndogo ya kuanzia au ungeanza nyumba ya ndoto yako kwa hatua? 👇
KELVIN HK BUILDERS — THE BUILDING MASTER
Tunajenga kwa UBORA.
📞 Call & WhatsApp:
0789 005 562
0765 005 562
📐 Ramani | Makadirio | Ujenzi | Renovation | Tiles | Gypsum | Painting | Finishing na huduma nyingine za ujenzi