Habarini wana JF
Mimi ni kijana wa miaka 20. Nilimaliza form 6 mwaka huu combination ya PCB nikapata div II. Ni kwamba hali yangu imekuwa ngumu mno hasa ktk kipindi hiki cha chuo kwa sababu mzee wangu binafsi ana uwezo wake mzuri tu wa kunisomesha hata miaka kumi sema alikataa kunisomesha na kuona kama ni mzigo kwake na kuamua kufanya biashara zake.
Sio hilo tu, hata matumizi yenyewe shule illikuwa mbinde na hela zipo. Sasa kiukweli binafsi inauma mno nikiona tu anatoa kwa watu wengine ambao sio wa kifamilia; sijui ni limbwata hata sielewi!
So nikapata bahati tu ya kusomeshwa na msamaria mmoja tu ila tu ana condition kali kinoma. Yani ni kwamba anakusomesha kwa mkopo ili baadae nije kumlipa nikiajiriwa na hapo hela inayotolewa ni ada tu maswala ya hostel na matumizi juu yako mwenyewe na kama ilivyo mzee hataki kunisaidia hata na mia yake.
Kwahiyo nilikuwa naomba ushauri wanaJF kwamba hii hela ya ada ya huyu jamaa anaenlipia ada niikate kidogo kama robo niweke kwenye biashara ya kujiajiri mwenyewe ili nijipatie hapo visenti vya kuishi?
Maana hapa naogopa mno nikifikiria ni hela ya watu nkianzisha biashara ikifa inakuwa jau tena au labda nianze biashara kama ipi yenye uhakika hela yke itarudi na faida kubwa?
NISAIDIENI WADAU HAPA CHUO SIWEZI KWENDA KWANZA NATAFUTA HIYO HELA YA HOSTEL KWANZA NA YA MATUMIZI!