X factor
JF-Expert Member
- Dec 18, 2022
- 1,436
- 2,298
Kisheria,sera na taratibu Iko wazi pale mtumishi anapostaafu anapaswa kupewa stahiki zake zote kama vile michango ya bima ya ustaafu (pensave scheme) kwaajili ya kusaidia maisha baadae ya kustaafu kazi.
Sasa hawa NIC wamekuwa ni kikwazo sana katika hilo,unakuta mtumishi kastaafu zake na amewasilisha nyaraka zinazohitajika lakini inachukua muda mrefu kupata mafao mpaka mstaafu anaanza kuwa ombaomba.
Kumbukeni hizo fedha siyo zenu ninyi ni mfuko tu ambao mtu anajiwekea kwaajili ya kesho yake.
Na pia ofisi yenu ya tawi la Mtwara Kuna wafanyakazi wenu siyo waaminifu,wanapokea nyaraka za wateja na kuzitupa kwenye droo bila kuzifanyia kazi mpaka mtu uhangaike mara zaidi ya moja ukihurumiwa ndo wanaziiingiza kwenye mifumo,hii ni kuleteana usumbufu usio na lazima.
Namba ya ofisi pale Mtwara haitumiki kitaalamu,muda mwingi haipokelewi na Muda mwingine inatumika kutuma meseji za kihuni.
NIC mko na Hali mbaya sana.