Nichagulieni gari kwa bajeti ya Milioni 10

Mkuu mimi kuna sehemu umeniacha kidogo.
10M kwa miaka 2 inamaanisha ni zaidi ya laki 4 kwa mwezi na wewe kipato chako ni laki 5 kwa mwezi. Maana yake unafanya saving zaidi ya 80%. Au hiyo laki 4 ipo nje ya laki 5 kwa mwezi??? Kama unauwezo wa kusave 80% ingependeza kutupa technics unazotumia maana inaweza kuwafaidisha wengi sana.

Tukirudi kwenye mada kuu, maana yake unauwezo wa kutumia 400k bila kuharibu mambo yako mengine.
Hivyo basi nakushauri ununue ist kama wengi walivyoshauri.
Kama utaamua kuagiza unaweza tembea mitandao ya bf, sbt, tcv n.k
1. Angalia cif +
2. Makadirio ya tax tra +
3. Port & bima ~ 300000
Ukishalipata kuna gharama za ziada za kijinga kuwa makini nazo (kuchora vioo, reverting, tint, alarm nk).
Mwisho kuwa makini barabarani, ukiachana na ukweli kuwa usalama wako ni muhimu sana pia unaweza ukajikuta unaingia katika mikono ya wazee wa fedha au mafundi ya garage bila sababu za msingi
 
Nikipata hela ya mauzo, natunza 15,000/= kila siku mkuu.

Zaidi ya hiyo sina chanzo kingine cha kipato.

Hiyo IST nitaizingatia, ila kuna waheshimiwa humu wameshauri kuwa kwa hiyo bajeti yangu ni vema niongeze kama Milioni 1.5 ya emergency,
Hivyo yabidi nidundulize tena mpaka mwezi Machi ili kuongeza hicho kiasi tukijaaliwa uzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaomba ushauri wa gari we unamshauri biashara.Nadhani we ulikuwa offpoint

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu kijana kaomba ushauri aina gani ya gari Anunue lakini kuna watu wanamwambia hafanye biashara Come on watanzania
 
Duka la dawa utahitaji mfamasi asajiliwe kwa ajili ya duka lako. Utamtafuta mtakubaliane umlipe kiasi fulani kutumia cheti chake.
 
Duka la dawa utahitaji mfamasi asajiliwe kwa ajili ya duka lako. Utamtafuta mtakubaliane umlipe kiasi fulani kutumia cheti chake.
Hivi hii sio kosa kisheria?
Na ikitokea shida kwa hilo duka mwenye cheti atakuwa salama?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…