Udochi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 787
- 1,056
- Thread starter
-
- #61
Mkuu,We Udochi naona kuna watu wanakushauri vizuri wengine vibaya. Sasa fuata ushauri wangu.
Toyota Ist 1490cc itakufaa kwa sababu kwanza bajeti yake ndio hiyo milioni 9.5 mpaka 10.5m
Kwa ulaji wa mafuta utaiweza na Ac pia unawasha.
Kwa vile ni mjasiriamali hata bidhaa zako za dukani unaweza kununua kutoka labda pale kwa Moshiro Kinyerezi kuzipeleka huko mjini kwako unakouzia bila tabu na petrol ikatumika ya wastani tu.
Usinunue Noah, Brevis, Mark 2 Grande zitakufilisi wala Vitz pia usinunue.
Na hiyo Ist mil 9.5 mpaka 10.5 unazipata hapahapa Dar wala usihangaike kuagiza.
Sent using Jamii Forums mobile app
Ushauri wako ni mzuri na nakushukuru sana.
Umesema kwa bajeti yangu itatosha kununulia hapahapa-
Je ni ya kwenye showroom ambayo haijatumika hapa Tanzania au ni iliyotumika hapa kwetu kisha mwenyewe akaamua kuiuza?
Sent using Jamii Forums mobile app