Nichukue gari ipi kati ya Toyota Voltz, Harrier, Rav 4 old na Premio?

vumiliag

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2018
Posts
413
Reaction score
764
Habari zenu wakuu

Nmejichanga changa nikapata milion 12 za kuvuta kausafiri, nategemea kuvuta kutoka mkononi mwa mtu. Sina hela yakuongezea kuagiza gari mpya sina uwezo huo.

ili niondokane na kero za usafiri wetu wa Dar es Salaam wa daladala.

Naomba mnishauri kati ya gari hizi ipi itanifaa.

Toyota voltz
Rav 4 old model (hii siipendi kivile)
Premio ya cc 1490
Harrier yenye engine ya 5s

Nataka kujua unafuu wa gharama za service na bei ya vipuli, yaani gari ipi kati ya hizo vipuli vyake si vya bei ghali

Katika gari hizo nilizotaja nimependa sana muundo wa toyota voltz (nahitaji kuijua zaidi hii gari.

NOTE: Nakaa sehem yenye njia mbovu mvua ikinyesha ni mtihan kupita.

Nikifanikiwa nitaleta mrejesho.
 
Nunua gari ya juu tu
 
Mkuu, yanini kujipa jakamoyo kununua vitu vya mkononi mwa mbongo!, hiyo 12M agiza Japan.
 
Kiongozi kama kwa maelezo yako uliyotoa bora uvumilie kidogo uchange uongeze ifike 14M chukua IST tu show room utakuwa na angalau mpaka miaka minne ya kuendesha gari bila kujuana na mafundi kama ni muendeshaji mzuri. Haya magari ya kununua kibongo bongo wengi wanauza likiwa limemshinda linaweza kukusumbua ukajuta. Na pia kwa magari haya utanunua ambalo limeshatumika kwa muda mrefu kwa Tanzania
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…