Nichukue ipi Kati ya TVS 150, 125 na BOXER BM 150, 125 au Hunter Hero

Unafika vizuri ila utafika tofauti na muda uliopanga
Mtalaam, inakuwaje boxer 150 mara engine inakuwa na mlio mhubwa mara mlio uliokuwa smooth yaani kama ume hit ile sweet spot kitu kimetulia u a cruize tuu?

Jengiine hivi unawashaje harzards kwenye boxer?

Kwa nini fuel gauge inasoma juu zaidi wakati pikipiki umeiwasha tuu na baadae gauge kushuka kidodo ukiwa upo kwenye misele
 
Hazard haijawekwa kwenye boxer, ila unaweza ongeza mwenyewe ikawa inapiga hazard fresh kabisa
 
Ni ushauri tuu hata mini nilishariwa hivyohivyo alienishauri namshukuru hadi leo πŸ™
Hatakuelewa mpaka limkute jambo jamaa yangu nilimshauri sana now anatembelea magongo kawa chiba
 
Mimi kama mlevi wa pikipiki ndogo sina cha kukupinga. Ila kwa mbio atampisha boxer.
 
Million 2.5 bora uendelee kujichanga ununue hata Vitz spana mkononi ... pikipiki itakupeleka ahera mapema..
Acheni kutisha watu. Ninatembelea pikipiki tangu 2003. Nidhamu na kuzingatia sheria ndio ngao ya huo woga wako.
 
nimeendesha zote, TVS ina sauti ya bass kuliko boxer, pia kwenye kuchemka TVS injini yake inachemka haraka kuliko boxer, ila boxer inahitaji kubadilishiwa oil filter mara kwa mara
Nimekubaliana na mchangiaji aliyechambua mzunguko wa oil lakini kama mtoa mada hatajali, boxet ni bora ISIPOKUWA achague halisi/original na awe mzingatiaji. Boxer haihitaji subiri nijichange. Ji delicated sana kwa vijitatizo vidogo-hazna uvumilivu kama ukoo wa kinglion, san/sun lag and co.

Boxer ukiipa inachostahili utaipenda hadi utafinga nayo ndoa. Simaanishi brands nyingine sio bora.
 
Hizi Watco sijuw wengine wanaziita CG nimeziona nyingi sana Tanga.
Inaonyesha zinatumia vizur Mafuta na zinavumilia sana shida.
KAma vip Mdau chukua hiyo kwaajilia ya kutembelea /mishe mishe za hapa na Pale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…