Nichukue PCM au PCB, naomba ushauri wako

Nichukue PCM au PCB, naomba ushauri wako

Nani kakuambia haina
ajira?
Tukirudi kwenye mada.PCM ina wigo mpana zaidi wa kusomea fani nyingi
kuliko PCB.Unaweza somea engineering yoyote,Computer Science au masomo
ya biashara kwa urahisi zaidi na mengineyo.Kwa ushauri wangu soma
PCM.

hapo sawa lakini wasiwasi wangu ni kwamba nitaajiliwa wapi na hiyo engineering yangu...?
 
Bora umejitambua kama una uelewa mdogo, halaf wote waliokushauri ni kama ww tu. pcm, pcb hiz ni combns tu na si ujuz, ukisema hii ina ajira kuliko hii unamaana gani?

soma unayoona utaimudu ukifaulu ndpo utachagua fani yenye ajira chuo kikuu.
 
Just a piece of advise:
A%20S%20angel.gif


Cha muhimu ni kusoma kitu (combination) ambayo unaiweza na kuimudu vizuri.

Kumbuka kusoma A-Level na kuishia kufeli (hata kama umesoma combination ngumu kiasi gani) hakukupi nafasi ya kuendelea na elimu ya chuo. Kimsingi unakuwa huna tofauti na aliyemaliza O-Level.

Kama uko vizuri kwa hesabu then kasome PCM cos kuna Physics pia ambayo inataka uelewa mzuri wa kukokotoa mambo, pia Physical Chemistry katika kemia. Mfano rahisi, kama O-Level umepata B katika B-Maths na hata darasani ulikuwa 'unastruggle' sana kufaulu B-Maths then PCM haikufai cos' A-Level mambo ni mengi na muda mara nyingi huwa hautoshi (kwa wale walio serious).

Kama uko vizuri zaidi na unapenda kudevelop career yako katika taaluma ya udaktari, then soma PCB. Ila PCB si masihara, yahitaji kusoma na kujituma kwa bidii, cos otherwise unaweza ishia kupata C flat kama utasoma evenly.

Mwisho: Kumbuka kuwa ndiyo unajenga future yako sasa, usikubali mawazo ya watu yakupoteze. Usifanye kitu 'because' watu (hasa unaowaamini) wamesema. Jiulize; Je nakiweza?
 
Nani kakuambia haina ajira?
Tukirudi kwenye mada.PCM ina wigo mpana zaidi wa kusomea fani nyingi kuliko PCB.Unaweza somea engineering yoyote,Computer Science au masomo ya biashara kwa urahisi zaidi na mengineyo.Kwa ushauri wangu soma PCM.
Siyo kweli PCB wigo kuliko PCM as long as umefauri vizuri maana unaweza soma hadi baadhi ya kozi za engineer lakin PCM huwezi soma kozi yoyote inayohusiana na PCB
 
Mimi nakushauri PCM kwasababu Mathematics itakusaidia zaidi. Tanzania inaenda kwenye biashara ya Oil and Gas na dunia nzima sasa inatafuta Engineers ambao wengi wanastaafu. Ma doctor wa Tanzania wanategemea serikali ambayo haina pesa na haitakuwa na pesa. Nakushauri chukua PCM na baada ya Form VI nenda kachukue Petroleum Engineering utapata kazi sehemu yeyote duniani.
 
ili kuondoa dialemma uliyonayo nakushauri ukasome biomedical engeneering ili uje kujiajiri!
 
swala la ajira lipo tu kama utaperform vizuri ilo lisikupe shida wala usilizingatie sana katika level yako. cha msingiangalia subject combination unayoipenda. ukichagua masomo utakayo yapenda yatakupa best results na utakuwa marketable kwenye soko la ajira hata ungekuwa umechukua KLF
 
Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....

kwani umeshapangiwa shule?halafu ujue combination zimeongezwa.
 
KOMBINESHENI YOYOTE NI NZURI iwapo utaifanya vizuri. Full stop.
Haya mambo ya kusema kombinesheni fulani ina ajira zaidi mara nyingi sio kweli sana. Halafu kumbuka mambo yanabadilika sana.. mpaka uje umalize chuo kikuu miaka mi5 ijayo, una uhakika mambo yatakua kama yalivyo sasa? We chagua kombi unayoiweza, nenda kakomae ufaulu uende chuo.
 
Kupangiwa shule na combination siyo tabu, kwani ukishafika shule Academic master wako atawapa muda wa kubadili comb.
Kuhusu uchaguzi wa comb. Malidhio na Haja ya moyo wako ndiyo jibu tosha kwani ninaamini unamalengo yako,na unaujua vyema uwezo wa akili yako juu ya masomo utakayo yachagua.
9ctme.
 
Nimemaliza kidato cha nne hapo mwaka jana.
Ninapenda sana kuchukua PCM, But kwa uelewa wangu mdogo na maoni ya baadhi ya watu inasemekana kwamba PCM Haina ajira serikalini unless kwenye makampuni binafsi (ambako kuna nepotism)... Kama kuna ajira zaidi ya hizo nijulishe tafadhali.
HILI LINANIKATISHA TAMAA SANA NA KUNIFANYA NIHISI KWAMBA NIKISOMA PCM SIPATI AJIRA TOFAUTI NA UALIMU.
Kwa upande wa PCB, INASEMEKANA kuwa kuna ajira za moja kwa moja serikalini ama kwa kujiajili mwenyewe. Na mimi ninasoma ili nipate ajira niweze kujitegemea.
MAONI YAKO NDIYO YATAKAYONIFANYA NIWE NA MAAMUZI MAZURI.
Natanguliza shukrani zangu kwa mtakao nishauri...
Karibuni kwa ushauri....
unajua inakua ngumu kidogo kukushauri maana ni vigum kuelewa na pia hujasema nini passion yako....nini unapenda!!! hapa ni lazima ujue hizi ni combi tu na kuwa dr au engineer ni lazima ufaulu fom6!!!
aalfu nani kasema PCM haina soko(baada ya kufaulu na kwenda chuo)??? serikali huwa inatoa post za ma engineer kila baada ya kipindi fulani!!! na kiukweli kwa hali ya tz kwa sasa ni lazima uwe na ndoto za ujasiriamalli,na ndio maana hata utapofika chuo utafundishwa hizi kozi na sio kungoja kuwa kijakazi!! si kweli kwamba ukisoma PCM utakua ticha labda ukasomee ualimu,je kama wewe ni injinia utaajiriwa na serikali kama mwalimu???
PCB iko fresh lakin amini usiamini inataka userios flani katika kusoma,ila kama kweli u wish to be doctor just go for it!!
my take...
PCM ni the best hasa ukiwa makini na ukitoka fresh fom6!! na ujue kusoma pcm si lazima uwe engineer,ila utakua na nafasi kubwa sana ya kua engineer kama ukitaka na pia inalipa!!!!!
 
Chukua EGM, hutakesha sana, utakuwa na wigo mpana kiasi. ECONOMICS (IS EVERYWHERE). MATHEMATICS (ALL ENGINEERING COURSES). GEOGRAPHY (ENVIROMENTAL, ENGINEERING & PLANNING ISSUES).
 
Kama unataka kuchukua chukua tuu,ila kama unataka kusoma zote ni njema isipokuwa PCB ni njema zaidi kwa maana ya afya.
 
hapo sawa lakini wasiwasi wangu ni kwamba nitaajiliwa wapi na hiyo engineering yangu...?

Unataka kuajiriwa wapi? Pcm/pcb hazitoi ajira. Hizo ni njia 2. Hata ukisoma pcmb ukipata 0 haina maana. Muhimu kwa sasa ni kufaulu mtihani wako wa mwisho 2. How? Kwa kuchagua combination ambayo unaweza kuimudu ili mwisho ufaulu vizuri. Baada ya kufaulu sasa ndo uje JF kuomba advice ukasomee fani ipi ambayo itakuwa marketable kwa kipindi hicho.
Maoni yangu:
Pcm/pcb zote nzuri. Faida ya pcm ni
- ina wigo mpana wa fani kuliko pcb.
- Msuli wake unatembea.
Kwa pcb;
- Kama lengo lako ni kusoma medicine ukikosa 1 na 2 nzuri sahau udaktari.
- Msuli ni heavy weight kimtindo (msuli tembo matokeo sisimizi)
CONCLUSION:
Zote ni rahisi kama utakuwa comitted. Soma unayoweza kumudu.
 
Kupangiwa shule na combination siyo tabu, kwani ukishafika shule Academic master wako atawapa muda wa kubadili comb.
Kuhusu uchaguzi wa comb. Malidhio na Haja ya moyo wako ndiyo jibu tosha kwani ninaamini unamalengo yako,na unaujua vyema uwezo wa akili yako juu ya masomo utakayo yachagua.
9ctme.

ahsante
 
Back
Top Bottom