Nick Mbishi & One 'The incredible' mpaka wafe?

John Rogath Nguzo

Senior Member
Joined
Dec 31, 2011
Posts
148
Reaction score
52
Imezoeleka hadi mtu afe ndo sifa zake zinatamalaki na nyimbo zake kupigwa redioni muziki unabadilika watu wanakuja na kuondoka katika Industry ya Hip Hop ya Bongo kwa sasa Nick Mbishi & One(uno) na Tamaduni Music kwa ujumla ndiyo wanaoifanya game hiyo vizuri kwa sasa nchini Tanzania.

Lakini Medias zinajifanya haziwaoni au inaumiza sana mtu anajituma,anaandika vizuri kwanini asisapotiwe? Kwa mtindo huu tusitegemee maendeleo katika industry ya Hip hop ya Bongo ni upuuzi,sijawahi kusikia wame be nominated katika aina yoyote ya tuzo hasa KTMA kila siku ni wale wale utasikia Joh Makini,Fid Q,Prof J,hadi Nick wa pili siku hizi kaingia.

But Mbishi ni kama haonekan hivi huu ni upuuzi first class tuthamini aisee wanachofanya hawa jamaa kama hujabahatika jitahidi kupata kazi za hawa jamaa itakuwa rahisi kuelewa nini?Namaanisha kwa Bongo kwa sasa hakuna kama hawa jamaa ni HAKUNA.
 
Unachosema mkuu ni kwli tupu. Jamaa wanatoa jiwe baada jiwe mpaka nashangaa na kudhani kuwa wanagundu. Lakin pia kwa upande mwingine Tatizo wana fanya ngumu ngumu sana. Wajaribu kubadirika kidogo. Angalia nyimbo za job makin na weusi utanielewa ninachosema. Hata prof. Jay nae anaimba laini.
 
Lakin ndo hip hop sasa kwa mfano nyimbo ya joh makini hii mpya Nusu nusu ni aina gani ya muziki?...kweli ngoma kali stle kali bt which kind of music is that?...lakin utashangaa mwakani inaweza chukua tuzo ya wimbo bora wa hip hop hahahahahaaa
 
hizo tuzo zao zenyewe kamati wamejigawa makund. Nawakubali sana hawa jamaa wako vyema hebu check ishu ya banza mitanzania ndivyo tulivyo
 
Lakin ndo hip hop sasa kwa mfano nyimbo ya joh makini hii mpya Nusu nusu ni aina gani ya muziki?...kweli ngoma kali stle kali bt which kind of music is that?...lakin utashangaa mwakani inaweza chukua tuzo ya wimbo bora wa hip hop hahahahahaaa

kwenye huo wa nusu nusu kuna mstari joh makini anasema wao wanatafuta punche line yeye anatafuta hit song.
 


Ile ndo hip hop ndugu haifanywi kuvutia watu ni mziki unaopaswa kubaki ulivyo ni kama vitabu vya bibilia vitabaki vile milele haviwezi kubadilishwa kuvutia watu
 
kwenye huo wa nusu nusu kuna mstari joh makini anasema wao wanatafuta punche line yeye anatafuta hit song.



Joh makin alishaachana na hip hop zamani sana tangu wakati wa ulimwengu wa wapendanao joh alitupilia hip hop kushotoo
 
Joh makin alishaachana na hip hop zamani sana tangu wakati wa ulimwengu wa wapendanao joh alitupilia hip hop kushotoo

kwahiyo sa hivi anafanya mziki wa aina gani? JOH yule wa kipinde alikuwa noma
 
jamaa co mainstream rappers wanajua wanachokifanya na wana mashabiki wao kwa wanachokifanya, music industry inamilikiwa na watu Tanzania so ukitaka wapate attention unayoitaka ni lazma waendane na industry inavyotaka
 
kuwaelewa hao jamaa inbidi uwe mvuta bangi.
 
JOH right now ni mfanyabiasha anatengeneza mziki wa kuuza atengeneze pesa ila hana tamaduni za hip hop tena
 
John Rogath Nguzo

"wakati wakidunduliza kupata punch lines mi nafululiza kufanya hit song" by joh makini.
 
Last edited by a moderator:
kwahiyo sa hivi anafanya mziki wa aina gani? JOH yule wa kipinde alikuwa noma


Sure Joh mziki anaoufanya now sijui ni style gani ila kawa mfanyabiashara sio hip hop tena
 
Ile ndo hip hop ndugu haifanywi kuvutia watu ni mziki unaopaswa kubaki ulivyo ni kama vitabu vya bibilia vitabaki vile milele haviwezi kubadilishwa kuvutia watu

Mbona nyimbo za 2pac zinavutia na still anaendelea kuheshimika sikuzote kama legend wa Hip hop?
 
1. Niki Mbishi alisema ameacha mziki

2. Wenyewe wana msemo wao "Hip hop ya kweli haipo redioni" , so wasiwalaumu watu wa media wasipopiga nyimbo zao coz wakizipiga itaonekana sio hip hop ya kweli (hiyo ni kwa mujibu wa msemo wao)

3. Jamaa wanafanya Hip hop ngumu sana, kuanzia beat hadi mashairi, Nikki akitaka nyimbo zake zichezwe afanye kama alivyofanya kwenye 'playboy' Mbona ulibamba sana, wakiendelea kufanya ngumu wataendelea kutusikilizisha masela tu geto kama Mimi hapa, nawakubali sana na nawasifia sana but hizi sifa nazowapa kwenye social network haziwafikishi popote. Tatizo letu masela ndo hivyo tunajua kusifia sana but CD zao hatununui, tunataka kupakua bure mtandaoni, hata kwenye show zao hatuendi. Kilingeni enzi zile ukienda unakuta mashabiki wako 30, tena kwa kiingilio cha buku jero, sasa hapa msanii anapata nini?

4. Hip hop ngumu kupata nafasi redioni ni tatizo, sio radio friendly. Na hili tatizo sio bongo tu hata unyamwezini ulikoanzia huu mziki, wanaotawala redioni/kwenye TV ndo hao kina Lil Wayne,Drake,Minaj,Young Thugs,etc wanaoimba kuhusu (f*ck,nigga,p*ssy,ass)

5. Ili ufikiriwe kuingia kwenye tuzo lazima nyimbo zako ziwe zinachezwa kwenye redios & tv, mashabiki wawe wanakufahamu, so sio kosa LA waandaaji tuzo, wenyewe wanaangalia ni wasanii gani wanatrend kwenye medias. Kuna kipindi nilikuwa Bukoba msimu wa pasaka, nilihudhuria kwenye mashindano fulan ya kuimba na kucheza yaliyokuwa yanafanyika beach. Sikuhiyo Songa aliambatana na wasanii wengine (hawana majina) kufanya show kwenye ukumbi maarufu unaitwa linas, sasa walikuja huko beach kupromoti show yao ya usiku maana kulikuwa na watu nyomi sikuhiyo aisee nilishikwa na huruma RAIA hawamjui kabisa Songa, MC alisema 'wangapi wanamjua Songa wanyooshe mkono, ilionekana mikono kama sita tu ukijumlisha na wakwangu, hili ni tatizo.

6. Wasanii hawa wanaofanya ngumu hasa wa Tamaduni hawako karibu na wadau wa media. Wanawatukana kwenye nyimbo zao/social network, usitegemee mtu unayemtukana apige nyimbo zako, mfano huyu wa kuitwa Nash MC anawatukanaga vya kutosha huko fb.

7. Media Redio/tv zinafanya biashara, hawawezi kupoteza mda wao kupromote kitu kinachopendwa na wachache, inaeleweka Hip hop ngumu zinapendwa na sisi 'masela', kundi kubwa ambalo ni (wazee,watu wazima,mabitoz, masista duu, watoto) ni ngumu kuwakuta wanasikiliza nyimbo dizain hiyo ya kina Nikki Mbishi, kama ni rap redio zitapiga hiphop laini za kina Bonge La Nyau coz hata masista duu wanaweza kusikiliza. Fid Q aliwahi kuanzisha kipindi chake kinaitwa 'FidFreestyle Friday' kinachohusu mambo ya Hip hop ila kilikufa kutokana na kukosa wadhamini, hii inadhihirisha kwamba Hip hop ngumu sio nzuri kibiashara

8. Nitaendelea....
 
Mi kwa upande wangu naona cha msingi ni good selection of beat. Beat inaweza ikafanya nyimbo yako iwe kali au ionekane ya kawaida. Ushawahi kujiuliza Songa angepita kwenye ile beat ya Joh makin i see me kwa ile ile kingetokea nini?! Kuwa na mistari punch haitoshi kama huna mdundo mzuri... Imefika muda lazima tukubali kuwa nyakati zinabadilika na wabongo wanapenda vya kuchezeka. Ila kama hiyo dhana ya Hip hop ukombozi ikiendelea kujengeka vichwani mwenu tutaendelea kuwasikiliza magetoni tu. HIP HOP sio lazima utolee video kwenye gofu, rangi black en white hakuna video queen mara mwingne jicho moja kajiziba, kichwani ana usongo. Lazima ukumbuke Hip Hop ni muziki na lengo la Muziki ni kuelimisha na kuburudisha sasa kama Muziki wako unaelimisha tu bila kuburudisha ni tatizo pia lazima iwekwe kapuni.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…