Nick wa Pili na mbwembwe za usomi

Nick wa Pili na mbwembwe za usomi

Sina shida na Nick Ila kuna kashikaji kake na Nick kanaitwa Hassan Ngima ka kule mawingu TV yaani kajamaa kanajifanya kanajua kila kitu cha Duniani afu kwa kutegemea uteuzi kanapenda sana kumfagilia mzee baba na chama kongwe!! Daah
Much know huwa wanaboa sana
 
Serious huyu jamaa hata usomi mnaozungumziaga mie nautafta siuoni. Anajua nn huyu jamaa tuwe wa kweli!

Kusoma shule sio issue, ni suala la kuhesabu madarasa tu na kuvuka darasa sio usomi, mtu yyte anaweza hilo. je; kuna scholarly material yyte amepublish kwenye eneo lolote ambalo yupo competent?
 
Watanzania tuko na mawazo hasi sana....na hayo mawazo hasi ndio yanayotudumaza akili na mwili......

Tunatumia muda mwingi sana kutafuta makosa na namna ya kukosoa baada ya kujifunza yale mazuri ya mhusika......hali hii mpaka huwa inaathiri maisha yetu ya kawaida kuwa kama tulivyo.......
 
Leo imenipendeza kumzungumzia huyu mkali wa "kunata na biti!" Kumbuka sio kila mwenye uwezo wa kunata na biti ni mwanamuziki mzuri. Huyu ni msomi, tena miongoni mwa wasanii wachache sana waliobahatika kubukua vitabu (kumbuka kwa elimu ya Tanzania kusoma sio kigezo cha kuelimika). jamaa anatokea Arusha akiwakilisha kundi la WEUSI. ameweza kuhimili mikiki ya industry kwa zaidi za miaka kumi sasa tokea enzi zile za "NIAJE NI VIPI?" halafu akatisha sana kwenye ile ngoma ya "UJAMAA" bonge moja la collaboration akiwa na Pipi wa THT then hapa kati kati akaachia mapini mengi sana heavy na hapa juzi juzi aka "switch" akasema anataka 'kucum" hapa alikuwa na wenzake ila kabla ya hapo walisema wanataka "kuliamsha dude" yeaah wenyewe wanakuambia wame "switch"

Kwanini namzungumzia Nick wa pili?
Jamaa kafanikiwa kujinasibisha na usomi. Na amekuwa akichagiza kwa kuibua hoja kadha wa kadha huko twitter na instagram. Hapo ndipo ninapotaka nipadadavue leo. Jamaa kafanikiwa sana kuuaminisha umma kuwa yeye ni msomi na mwenye mawazo ya kiwango cha juu sana labda mfano wa akina Jenerali Ulimwengu au Issa Shivji. Kwanza kabisa hii ni violance maana anawafanya watu wawe inferior kwake watazame hoja zake kwa jicho lililojaa wenge na kushindwa kuchambua hoja hizo vizuri. Jmaa sio mzuri wa kujenga hoja ila yuko vizuri kwenye kucheza cheza na maneno na kuyarudia rudia hatimaye hata hoja dhaifu inaonekana tata, kumbe utata upo kwenye lugha ila sio maudhui ya hoja husika (kasikilize SWEET MANGI utaona hii kitu)

Ukiitazama hoja yoyote ya Nick as whole lazima ikuchanganye na utaishia kuvurugwa. Hoja ya Nick kwanza ivunje vunje katika parts ndogo ndogo kisha idadavue utaona maajabu yaani hakuna lolote. sasa Nick aache kutumia ujanja ujanja ambao unapelekea watu kushindwa kutambua msingi wa hoja zake ila aweke hoja vizuri ieleweke kisha ijadiliwe na kila mtu. yaani kuwa complicated sio kigezo cha usomi. Nick ajitafakari upya.

ni hayo tu.....
eeeniwei. najua ukimalizana na Nikki utakuja kwa Masoud Lipanya nae useme awe anatucholea hivi: badala ya kikuku ndani tenga lenye kisu juu japo mlango umefunguliwa....aseme CCM imetuteka
 
Back
Top Bottom