Nick wa Pili na mbwembwe za usomi

Nick wa Pili na mbwembwe za usomi

Hahahahahhahahaha
h mbavu zangu mie.
Doctor shika part two
ndugu watu wana hela....usichukulie poa...BAADHI YA WATU JF WANA HELAAAA....Mimi nimewahi kudate staff wa UN tulionana hapa JF. usiichukulie poa JF
 
eeeniwei. najua ukimalizana na Nikki utakuja kwa Masoud Lipanya nae useme awe anatucholea hivi: badala ya kikuku ndani tenga lenye kisu juu japo mlango umefunguliwa....aseme CCM imetuteka
Mkuu, nadhani wote tunajua msingi wa sanaa. Huwa inabebwa na mambo mawili ambayo ni fani na maudhui. Hizi ni kama pande mbili za shilingi huwezi ukazitenganisha na bado ikaitwa shilingi. Sasa sijagusa sana kuhusu sanaa (ambayo hata hivyo nina mashaka nayo) yake bali nimegusa vile anavyotumia kilemba cha usomi kufanyia watu manipulation. Hayupo straight kwenye hoja zake, huwezi kujua anasimamia kipi, hayupo clear na bahati mbaya watu hawaoni kasoro katika hilo maana kafanikiwa kuwaaminisha watu kuwa yeye ni msomi na watu wanadhani namna ya uwasilishaji wa hoja za Nick inatokana na usomi wake.

Kuhusu sanaa yake, yupo vizuri upande wa fani japo sio sana ila upande wa maudhui nadhani ajiongeze zaidi.

Tatizo siku hizi ukiongea ukweli unaitwa hater....
 
Watanzania tuko na mawazo hasi sana....na hayo mawazo hasi ndio yanayotudumaza akili na mwili......

Tunatumia muda mwingi sana kutafuta makosa na namna ya kukosoa baada ya kujifunza yale mazuri ya mhusika......hali hii mpaka huwa inaathiri maisha yetu ya kawaida kuwa kama tulivyo.......
Mkuu heshima yako,
Naamini ili uweze kudadavua au kutafiti jambo lolote kiuyakinifu yakupasa usihusishe hisia bali fikra huru. Kuwa na mawazo hasi juu ya jambo fulani si vibaya na kuwa na mawazo chanya juu ya jambo fulani si tatizo...

Tunachoangalia je wazo ulilonalo kuhusu jambo fulani limejengwa juu ya msingi gani? Je unasifia hicho kitu kwa sababu tu ya mahaba binafsi au kuna sababu fulani ya msingi inayokufanya wewe usifie!

Kwa upande wa Nick kiukweli anazingua, hajasingiziwa hata moja kwenye uzi huu.
 
huyi ndiye aliyeimba I am sorry JK?
Hapana huyu ameimba NATAKA NICOME, NALIAMSHA DUDE, BABA SWALEHE na nyimbo nyingine nyingi.... huyo aliyeimba kuhusu JK anaitwa NICK MBISHI
 
uwa anataka kuandika kama msomi lakini anashindwa.
kuna siku nilisema Niki ana akili zilizopitiliza.
mwisho Wa siku anaonekana ovyo.
 
nick mwepesi tu, namshangaa na maswali yake yakitoto, jamaa wakawaida sana na ni bingwa wa kuongea mambo nje ya mada
 
Hapana!!!! Na hili ndo tatizo la jamii forum unachat na mtu ambaye humjui,mzee ni V8 mbili Mimi,nina 600 million bank,nina uhakika wa 4.5 million kila mwezi,tusichukuliane poa kiasi hicho
Mkuu ukinipa kaajira hata ka kuosha hizo gari zako utakua umenisaidia na Mungu atakubariki
 
Hapana!!!! Na hili ndo tatizo la jamii forum unachat na mtu ambaye humjui,mzee ni V8 mbili Mimi,nina 600 million bank,nina uhakika wa 4.5 million kila mwezi,tusichukuliane poa kiasi hicho
Nimependa tu jibu lako, Mungu akubariki katika hayo.
 
Sina tatizo na nick kwenye kazi yake ya mziki ila huku kwingine kwakweli kwa upande wangu mimi anaboa

Na huko kusoma kwake SOCIOLOGY ndio amekuwa akijifanya mjuaji kupita kiasi sipati picha jamaa angesoma AFYA, ENGINEER, LAW

Jamaa kwenye hoja waga haeleweki, muulize swali liko open kabisa ila jibu atakalokupa hadi unaonea huruma elimu yake

juzi kati kaulizwa swali na msanii mwenzake (WAKAZI) kule kwenye uwanja wake wa kujichukulia points (Twitter) aisee jibu alilotoa na kama huo ndio waga ujibuji wake sijui ata chuo alikuwa anafaulu vipi maana ni zaidi ya opposite
 
Back
Top Bottom