[Mwanzo] Rudi Table
Solemba - JUWATA JAZZ(Nico Zengekala)]
Ulinipa ahadi tukutane kwenu,
Nikitumaini nimewahi,
Nilichopata kwako ni matusi ooh, ooh na
dharau tele
Ungenieleza ukweli solemba,
Kuliko kunidanganya ooh,
Najuta kuitimiza ahadi ooh ambayo si ya
kweli.
(Chorus)
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Nilichomwa na jua toka asubuhi,
mpaka saa nane Solemba sababu ya
kukungoja wewe
Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani
Nimeshituka Solemba ,
Nimeshituka Solemba
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
[Zengekala]
Sikutaki tenaaa, sina haja nawe,nimeshapata
mwingine atakaye nipenda kwa roho moja,
Tafuta bwana mwingine utakae mbabaisha
kama mimi
Huna huruma Solemba.......Aloi I love you
baby
[Wote]
Nilikupenda kimapenzi Solemba eeh,
ila dharau uliweka mbele solemba.
Rudi mwanzo
[TUMA - Nico Zengekala]
Nilisimama kwenye kona, ya uhuru na
msimbazi,
Natizama wanaopita , wanaorudi mamaaaa,
Huenda nikaiona sura yake tuma.
Nasimama nikiwaza, ahadi yetu tuliopanga,
Tukutane Darisalama, Tuma mama,
Nia na madhumuni wazazi watuone.
Nilishikwa na mnutsuko shoga yake
aliniponiejia na kunieleza
Tuma ee tuma ee keshaolewa
Nilishikwa na mshituko mapigo ya moyo
enda mbio
Sikutegemea Tuma, kama angevunja ahadi
yetu ama kweli penye uzia hupenyeza rupia
CHORUS:
Usinione nimekonda ewe Tuma, hakuna
lingine mama
Ila ni wewe Tuma.
(Usiku wote nalala nikikuwaza nakuita jina
lako oh oh Tuma)
Repeat: Usinione nimekonda ewe Tuma.
Rudi mwanzo